Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Mheshimiwa Waziri wa Elimu, naomba kuuliza swali hili na nitaomba ama kupata majibu au kufanyiwa kazi kwa nitakachouliza.
Kwa nini wamiliki wa shule za PRIVATE za Primary wamekuwa wakiwapokea wanafunzi wa darasa la kwanza na kwenda nao mpaka darasa la SITA bila usumbufu wowote lakini wanapoingia darasa la SABA wamekuwa na tabia ya KUWATIMUA wanafunzi ambao wanakuwa hawajafikisha wastani wanaoutaka wamiliki wa shule hizi?

Mtu amelipia ada kubwa kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la SITA, akifika tu darasa la SABA mzazi anaambiwa ampeleke mtoto wake kwenye shule za Serikali.
Kwa nini kuwasumbua wazazi kiasi hiki?
Kwa nini serikali haiwachukulii hatua wamiliki wa shule hizi?
Je, shule za Serikali ni Dampo?
Naomba serikali iandike waraka maalumu kulaani vitendo hivi viovu na kutoa mwongozo na onyo maalumu kuzuia tabia hii.
Mungu ibariki Tanzania, Rais, Mawaziri na Watanzania wote. Ahsante.
 
Habarti za basubuhi watanzania wenzangu,lengo la kuanzisha thread hii maalumu sana ni ili kutoa fulsa kwa sisi wananchi kuishauri serikali yetu katika mambo mbalimbali yahusuyo taifa na ustawi wake kwa ujumla.
Naomba Mods msiufute Uzi huu isipokuwa mtafute namna ya kuuweka vizuri ili tutoe maoni kwa Taifa letu.

My take:
Naomba tuongee mambo ya msingi ya kurekebishwa na Viongozi wetu wanaingia humu watasoma na kujua wapi kuna tatizo, Waweke sawa sambamba na kuwagutusha mambo yanayoendela wasiyoyajua.

Karibuni sana;
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.

KERO ZIFUATAZO
Kuna mmiliki wa shule ya St. Patrick iliyoko maeneo ya sakina Arusha DC, ameziba njia ya nyuma ya shule hiyo ambayo amejenga jengo lake na kuziba na geti njia hiyo, vile vile anaendelea kuhatarisha maisha ya wananchi kwa kuruhusu maji machafu ya chooni kwa kuyafungulia mtaroni uongozi wa mtaa wanayajua haya lakini wamekuwa kimya pasipo kuchukua hatua yeyote na hili linaendelea kila siku.

Kuna eneo lililopo maeneo ya Sanawari ambapo limepakana kwa barabara na Jengo la ccm eneo hilo kulikuwa na nyumba zilizobomolewa na hivi sasa limezungushiwa mabati. Kuna tetesi kuna mtu anataka kupewa eneo hilo ili aweke sheli jambo ambalo ni kinyume na taratibu mkifuatilia mtakugundua ni nani anashinikiza hilo lifanyike
 
Mkurugenzi Muheza District anapanga mbinu yakuwanyanganya ardhi watu katika shamba la azimio. Kisingizio ni kuwa hawajajenga nyumba za makazi wakati mashamba hayo wamekuwa nayo miaka mingi. Kwaanayejitambua huwezi kujenga kwenye ardhi ambayo ina mgogoro. Hivyo hoja yake haina mashiko.
Tunaomba waziri Lukuvi aingilie kati kukomesha dhuruma hii inayopangwa kiujanja ujanja
 
Habari wana Bodi.
Ni muda sasa nimekuwa najiuliza inawezekanaje serikali kulipa mishahara kwa wafanyakazi wa Taasisi Binafsi alafu Mkaguzi wa Hesabu za serikali hawezi kufanya ukaguzi wowote katika hayo mashirika? Nimejaribu kufanya kauchunguzi kangu kadogo, kuna taasisi za utafiti wa mazao ambazo zinaendeshwa kama sekta binafsi lkn serikali inalipa mishahara ya wafanyakazi na mbaya zaidi sina uhakika kama Wizara ya Kilimo inafuatilia kwa umakini utendaji wao. Haya ni majipu maana sioni kama ni tofauti na wafanyakazi hewa, iwapo unalipa mshahara kwa mtu ambaye haujui kafanya kazi gani kwa siku. Swali ninalojiuliza ni kwanini serikali kupitia wizara ya kilimo isizichukue hizi taasisi za utafiti wa mazao na kuzifanya taasisi za kiserikali zisimamiwe na wizara ya kilimo ili kuwe na tija kwa kile wanachokifanya. Mfano Taasisi ya Utafiti wa Kahawa, chai, Tumbaku n.k Kwanini ziendelee kuendeshwa kama sekta binafsi?
 
CAG nadhani haendagi katika mashirika binafsi, hayo ya utafiti wa mazao ni serikali na yanahitaji kukaguliwa kama kawaida, ukiona mkaguzi hajaenda huko.? ujue kuna jambozi!
 
CAG nadhani haendagi katika mashirika binafsi, hayo ya utafiti wa mazao ni serikali na yanahitaji kukaguliwa kama kawaida, ukiona mkaguzi hajaenda huko.? ujue kuna jambozi!

CAG anauwezo wa kumkagua yeyote kwa maana ya taasisi,siyo lazima iwe serikali.CAG ni Auditors kama walivyoauditors wengine
 
Huu uzi ni mzuri sana kama kweli hizi kero zitawafikia walengwa itasaidia sana.
Na naomba tuendelee nao mpaka kieleweke.
Kelo yangu mabasi ya abiria kupita sheli yakiwa na abiria sheria inaruhusu na kama hairuhusu wahusika mchukue hatua, mfano stand kuu Tabora kuna baadhi ya mabasi yakishaanza kuondoka eti ndiyo yanapita stand kujaza mafuta.
 
Habarti za basubuhi watanzania wenzangu,lengo la kuanzisha thread hii maalumu sana ni ili kutoa fulsa kwa sisi wananchi kuishauri serikali yetu katika mambo mbalimbali yahusuyo taifa na ustawi wake kwa ujumla.
Naomba Mods msiufute Uzi huu isipokuwa mtafute namna ya kuuweka vizuri ili tutoe maoni kwa Taifa letu.

My take:
Naomba tuongee mambo ya msingi ya kurekebishwa na Viongozi wetu wanaingia humu watasoma na kujua wapi kuna tatizo, Waweke sawa sambamba na kuwagutusha mambo yanayoendela wasiyoyajua.

Karibuni sana;
Sawa mkuu tuendelee
 
MJipu ktk sekta ya viwanda baada ya serikalikutilia mkazo kuhusu mikataba ya wafanya kazi sasa kuna mikataba fecki wanao sainishwa wafanya kazi na hao wanao jifanya wanaenda viwandani kufuatilia wanaishia ofisini kwa mabosi na kuishia wakitoka huku wakipeana mikono huku wakisahau Nazi iliyo wapeleka kiwanda nnachokijua chenye mikataba fecki ni star ways group international kilichopo dundani kwa kibuguru istoshe hua wanaongoza kwa uvunjifu Wa haki za binaadam
 
CAG anauwezo wa kumkagua yeyote kwa maana ya taasisi,siyo lazima iwe serikali.CAG ni Auditors kama walivyoauditors wengine
Kwa hali ya sasa hivi hakuna taasisi yoyote ya umma iliyo huru kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria husika
 
Ndugu wana Geita mliopo jf ,kwa pamoja tunapaswa kushirikiana kwa pamoja kumsaidia Rais wa tanzanzani mh magufuli kwa juhudi alizo nazo na serikali yake, kuzifaham kero zetu kama watanzania kwa pamoja na tungependa zifanyiwe kazi.

Mnakaribishwa sana

MWONGOZO: kero/jipu na kama kuna ufafanuzi wa kutosha eleza

Kero zetu ,zitapelekwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji
 
Kero yangu kubwa ipo kwenye hii tabia ya kutekana tekana,kupigwa risasi,kupelekwa baharini ukiwa kwenye kiroba na kufariki..naona hivi vitendo vimeshamiri na vimeota mizizi naomba sector husika ilitilie mkazo .... Na kusambaratisha hilo genge..lasivyo tutajua kwamba ni mfumo mpya na mamlaka husika inabariki...

Hiyo ndio kero yangu kuu kuelekea nchi ya vi-wonder
 
mchezo ulioanzishwa na baadhi ya wakuu wa wilaya wa kutumia wanafunzi kuwapigia kura walimu wenye tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi ukome maana wanafunzi wanaweza kumpigia kura mwalimu anayewajibika na kuwachapa viboko huku mwalimu mzembe akionekana msafi.

Lakini pia mwalimu mwenzie au mtu mwingine mtaani mwenye chuki naye anaweza kuahamasisha upigaji wa kura hizo. Tatizo jingine wale walimu wanaopigiwa kura nyingi wanaambiwa wahamie shule nyingine, swali ni je hiyo shule anakohamia ndo wanahitaji walimu wenye tabia mbaya?

Kama ni kuwabaini walimu wenye tabia chafu serikali inavyo vyombo vingi kwa nini isitumike njia nyingine isiyoacha shaka ili kuwabaini walimu wenye tabia mbovu badala ya kutumia njia yenye ukakasi? Wanasiasa acheni tabia hizo za kutafuta kiki huku mukiacha jamii kwenye mitafaruku isiyokuwa na tija.
Shukrani sana mkuu kwa taarifa. Ni wilaya gani wakuu wa wilaya wanafanya kazi ya ovyo namna hii
 
Ndugu wana Geita mliopo jf ,kwa pamoja tunapaswa kushirikiana kwa pamoja kumsaidia Rais wa tanzanzani mh magufuli kwa juhudi alizo nazo na serikali yake, kuzifaham kero zetu kama watanzania kwa pamoja na tungependa zifanyiwe kazi.

Mnakaribishwa sana

MWONGOZO: kero/jipu na kama kuna ufafanuzi wa kutosha eleza

Kero zetu ,zitapelekwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji
Ufisadi kwenye Fedha za Elimu bure shule ya sekondari Kivukoni Geita Mji, Mkuu wa shule anafanya manunuzi hewa ya vifaa, vya kujifunzia na kufundishia! Mfano ameagiza box za chalk au ream 20, zinakuja 10 alafu 10 zingine anaenda kwa mdhabuni kuchukua pesa taslimu mkononi kwa ajili ya matumizi yake binafsi bila kushirikisha kamati ya manunuzi!

Kuwaomba wadhabuni ten percent, hii hii tabia pia inasababisha baadhi ya wadhabuni kugoma kuleta baadhi ya vifaa kufidia hiyo ten percent! (Hii ilitokea mwaka Jana wakati ameagiza vifaa kwa ajili ya mtihani wa kidato Cha nne!(mdhabuni namjua namuweka kapuni) Ni wa mwanza Jiji!

Ukiongea na kukemea unatishwa kupelekwa shule ya msingi, au kunyimwa fursa zozote za hela mfano usimamizi wa mitihani ya taifa na usahihishaji wake au semina mbalimbali!

Kuna maovu mengi tu siwezi kuyasemà yoyote hapa!
 
Jipu kubwa zaidi lipo kwa uhamiaji kuna wahamiaji haramu wanaofanya kazi bila vibali na hawana vibali vya kuishi nchini pia. Tumetoa sana ripoti kwa maafisa wa uhamiaji lakini tukageuziwa kibao tukaitwa na boss tueleze kwa nini tunataka kuua kampuni yake yeye hana pesa ya kulipia wageni maana wapo zaid ya 50 so serikali hapa imekosa zaidi ya million 100. Huyo afisa aliyetuchoma anaitwa John M jina la pili tumemstai kwa sasa tu natafuta namna ya kuakikisha tunafikisha hizi taarifa kwa Magufuli maana huyo Waziri Kitwanga nae ni mzigo tu hatumuamini.

Huu ni ujipu wa hali ya juu sisi tunatoa sapoti kwa taifa wao wanaenda kuchukua rushwa alafu wanatuchoma. Uhamiaji ni jipu jipu kubwa sana.
Mkuu taja na jina la pili na sehemu anakofanyia kazi(jina la mkoa&wilaya)
 
Ufisadi kwenye Fedha za Elimu bure shule ya sekondari Kivukoni Geita Mji, Mkuu wa shule anafanya manunuzi hewa ya vifaa, vya kujifunzia na kufundishia! Mfano ameagiza box za chalk au ream 20, zinakuja 10 alafu 10 zingine anaenda kwa mdhabuni kuchukua pesa taslimu mkononi kwa ajili ya matumizi yake binafsi bila kushirikisha kamati ya manunuzi!

Kuwaomba wadhabuni ten percent, hii hii tabia pia inasababisha baadhi ya wadhabuni kugoma kuleta baadhi ya vifaa kufidia hiyo ten percent! (Hii ilitokea mwaka Jana wakati ameagiza vifaa kwa ajili ya mtihani wa kidato Cha nne!(mdhabuni namjua namuweka kapuni) Ni wa mwanza Jiji!

Ukiongea na kukemea unatishwa kupelekwa shule ya msingi, au kunyimwa fursa zozote za hela mfano usimamizi wa mitihani ya taifa na usahihishaji wake au semina mbalimbali!

Kuna maovu mengi tu siwezi kuyasemà yoyote hapa!
Mkuu kungekuwa na uwezekano wa kupata no yako tungewasiliana
 
Back
Top Bottom