SALAMU ZA PASAKA 2018 KWA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Kwa wakristo wote, Heri ya siku kuu ya pasaka.
Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wote wa ngazi mbalimbali katika Serikali ya awamu hii ya tano, nawapongeza sana kwa kazi njema na ngumu mnazozifanya kila siku kwa ajili ya Watanzania.
Nitumie fursa hii kuwapongezeni kipekee kwa mambo machache yafuatayo:
(1)Kuongeza uwajobikaji wenye tija katika utumishi wa umma.
(2)Kuongeza bajeti ya madawa ya binadamu zaidi ya mara7 ya bajeti ya madawa iliyopita.
(3)Kuzuia wizi wa rasilimali zetu ikiwemo madini, wanyamapori nk.
Hayo ni mfano tu, lakini yapo mengi mazuri yaliyo na yanayoendelea kufanywa na serikali hii.
Ndugu zangu viongizi, yanapofanyika mambo makubwa kama haya, lazima tutegemee kuibuka makundi kinzani ya kila sura na kila aina kutoka ndani na nje ya nchi . Kwani, kufanya haya ni kuwaumiza baadhi ya waliokuwa wanufaika wa rasilimali zetu hapo mwanzo.
Najua wengi watapiga kelele za kila aina na watafanya njama za kila aina lengo likiwa ni kufifisha jitihada hizi.
Rai yangu kwenu viongozi ni mshikamano wa kweli baina yenu ikiwa ni pamoja na sisi raia. KAMWE, KAMWE, KAMWE tusikubali hata kidogo kuyumbishwa au kurudishwa nyuma na mtu yeyote awaye yote.
TUSIGEUKE NYUMA, TUSIJE KUWA MAWE.
Mabadiliko ni Mapambano.
Ahsante, pasaka njema.