Hali ya usalama jijini Dar bado ni ya mashaka.
Ninaomba vyombo vya dola vifuatilie maeneo ya BULULA,GOLANI na MATOSA katika kata ya Saranga.
Maeneo hayo yanasemekana kuhifadhi wahuni wanaokimbia operesheni kali za jeshi la Polisi katika maeneo mengine ya mji haswa Manzese ambapo inasemekana wengi wa wahuni hao ni mabaki ya makundi ya MBWA MWITU na PANYA ROAD.
Hivi karibuni kumeanza kuibuka uhalifu wa kupora watu,watu kushambuliwa na vikundi vya wahalifu na kukatwa mapanga huko Matosa, Bulula na Golani.
Sasa hivi kuna taarifa kwamba wahalifu hao hasa kutoka Bulula na Golani wanakwenda hadi Kimara Suka na Kimara stop over nyakati za usiku na kufanya uhalifu kwa kushirikiana na makundi ya wahuni wa Suka,Stop over na Matosa.
Taarifa zinafika Polisi Kimara na Mbezi lakini zinapitishwa defender mbili tatu kwa siku moja au mbili bila ya kukamata wahusika halafu kimyaaa, wahuni wanazidi kuvimba vichwa na kuzidisha uhalifu mitaani.
Naomba mamlaka za juu za kiserikali na vyombo vya usalama kutokupuuzia suala hili,haswa makundi yanayojiunda upya huko Bulula na Golani.
Msikurupuke,fanyeni uchunguzi wa kina kujua nini kinaendelea,tumeni watu toka mbali kwani hawa askari wenu wanaohusika na maeneo hayo (Mbezi) wako compromised.
Pia suala hili limulike Dar yote,wahuni wana syndicate zao siku hizi.
Wana mitandao ya kimaeneo jijini na wanasimamiwa na tycoons wenye pesa,maarifa,mikakati na masoko kwa ajili ya biashara zao haramu.
Wana mitandao hadi kwenye bodaboda na madereva taxi.
Pale Ubungo kulikuwa na wizi lakini tangu kituo kihamie mawasiliano na wizi nao umehamia huko na maeneo ya zile njia za pembeni kuelekea Mlimani city.
Mmeshawahi kwenda kuchunguza nini kinaendelea chini ya yale madaraja ya Ubungo?
Nasikia mali nyingi zinazoibwa eneo la Ubungo zinapatikana chini ya madaraja yale. Fuatilieni.
Haya makundi msiyape nafasi,maana watu wenye pesa na exposure kubwa ya maisha wameanza kuyageuza dili na kuyatumia,hivyo kuwapa mbinu zilizoenda shule.
Msipojipanga na mkipuuza jiji halitakalika hili huko mbele.
Halafu vita ya vijiwe vya madawa na bange inawashinda nini jamani? Watoto wanaharibika. Vijiwe vya wahuni ndio center za kuuza bidhaa hizo na niwaambie jambo moja msilolijua akina Makonda na wenzio, HOMOSEXUALITY IS VERY COMMON THERE.
Wahuni wengi wanaotumia madawa na bange wanafanyiana huu ushenzi,saaana tu, ni siri zao. Msikurupuke, fanyeni uchunguzi, mtajua meengi sana, halafu anzisheni operesheni zenye malengo,mkiwa na uhakika where to hit and how and when.
Mwisho ninawaasa wazazi wenzangu wenye watoto wenu boarding schools. Hawa wahuni na vijiwe vyao wana wateja wengi wa bangi huko boarding schools wanawapelekea. Sijui walimu na walinzi wa hizo shule wanakuwa wapi. Sasa bangi ya leo sio ile mliyokuwa mkivuta nyinyi enzi zenu. Bangi zao wanachanganya na unga humo humo. Wakikosa kabisa huchukua valium,bangi na gundi ya viatu wanachanganya humo. Huyu mvutaji wa hiyo kitu ukikutana naye usiku akikunyanyulia panga akate sikio, harudishi mkono bila sikio lako.
Kama mnajali jamii yenu basi fanyieni kazi taarifa mnazopata.