Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Pamoja na kuwepo kwa watumishi hewa pia kuna tatizo la "kubebana" ukiangalia takribani taasisi zote za serikali watumishi waliopo haswa katika mikoa/miji mikubwa wengi wao "wamebebwa" au wamekingiwa kifua kamwe huwa hawahamishwi kwenda mikoa ya pembezoni.

Kubebana au suala la vimemo ni kero kubwa inayo wasibu watumishi wa Ummma, kwani wanao teseka na kunyanyasika ni wale wasio na wa kuwabeba, wamebakia kutaabika na kukata tamaaa!

Wizara ya Utumishi wa umma ifanye uchunguzi wa kina itabaini hayo yote. Kinacho takiwa ni watumishi wate wa umma wawe sawa tofauti iliyo hivi sasa kuna matabaka; wale wenye ndugu wa kuwabeba na wasio na ndugu/jamaa wa kuwabeba.
 
Wasalaaaaaam!


Wandugu hii ni “Special Forum” kwa ajili ya sisi wananchi kutoa na kuelezea CHANGAMOTO zinazotukabili kwenye mazingira tunayoishi mahali popote hapa Tanzania na wahusika watazipata na kuzifanyia kazi kupitia hii “Forum”.

Kwa kuanza kabisa, naomba wahusika na kipande cha barabara kuanzia Sinza kijiweni kuelekea Tandale, hii barabara imeharibika sana kwa mashimo. Tafadhalini wahusika mlifanyie kazi hili kwani ni adha kubwa kwa sisi watumiaji wa hii barabara.


Karibuni.
 
Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutufikisha mpaka leo tukiwa wazima na akiendelea kukupa ulinzi na nguvu rais wetu mpendwa JPM. Binafsi napendezwa sana na mambo unayoyafanya katika hii nchi wanaobeza nadhani wanayao manufaa binafsi.

Nianze kwa kuelezea kifupi hali ya hamashauri ya wilaya ya Momba iliyopo mkoa mpya wa Songwe.Halmashauri ina zaidi ya miaka mitatu sasa, mpaka mwezi may mwaka huu ilikuwa bado inatumia majengo ya kukodi kama ofisi kibaya zaidi majengo hayo yalikuwa ndani ya wilaya nyingine ya Mbozi.

Mwezi april mwaka huu ulipotuletea mkuu wa mkoa, alitoa agizo kwamba ofisi za halmshauri momba ziende kulikopangwa kuwa makao makuu ya wilaya (kijiji cha chitete), Kwa kutekeleza maagizo mkurugenzi na mkuu wa wilaya waliopita walihamia pamoja na wafanyakazi waote.

Mheshimiwa rais ni kweli tumehamia lakini tunakuomba hata wewe mwajiri wetu mkuu uje uone mazingira ambayo umetuleta tufanye kazi na uje ujue je kazi zinafanyika? Tunatumia madarasa kama ofisi na wanafunzi wanasoma hapohapo, nyumba za walimu zimekuwa ofisi za halmshauri.

Gharama za utoaji huduma

Toka tumehamia utoaji huduma kwa wanachi umeshuka sana kutokana na eneo ofisi zilipo na watu tunaowahudumia wanapotoka.Uendeshaji wa halmashauri umekuwa wa gharama kubwa kwani mambo mengi tunatakiwa kuyafuata Mbozi, mfano mafuta ya magari yanapatikana Tunduma ambapo ni Zaidi ya km 90 toka chitete yalipo makao makuu ya wilaya.

Wananchi wanasafiri umbali mrefu kuja kupata huduma na wakifika wanafika jioni hakuna hata nyumba za kulala wageni ipo tu moja yenye vyumba saba tu. Hata watumishi tukitaka kwenda kuwahudumia wananchi tunashindwa kwani tunaambiwa halmashauri haina mafuta.

Haki za watumishi

Watumishi tumekuwa wanyonge na wenye manung’uniko kwani kuna mambo hatutendewi sawa wa viongozi wetu wanaotuongoza.

Moja ya wakuu wa idara ambao wamekuwa kikwazo na tungeomba ufanye mabadiliko na uchunguzi ufanyike ni mweka hazina wa wilaya. Ni mzaliwa na mwenyeji wa hukuhuku yaliko makao makuu ya wilaya ila naona huyu hana nia ya kuona jamii yake ikiendelea ila amezidi kujinufaisha yeye.

Wafanyakazi wengi hatujapewa hela za kujikimu toka tumeajiriwa, mkurugenzi kapitisha maombi yetu lakini DT ni kikwazo.Kwa tetesi ni kuwa jinsia ya kike wengi wao wamepewa ila jinsia ya kiume ndo tunaambiwa hakuna hela wakati riport za makusanyo 2015/2016 walilipoti kuwa wamevuka lengo.

Mheshimiwa rais kuna baadhi ya wahisani watajitoa kusaidia wilaya ya Momba kwani kuna fedha walizitoa zifanye baadhi ya projects lakini bwana huyu kabadilisha matumizi, watu wanaandika riport za uongo tu. Mfano Unicef,na wengine.

Ukitaka upewe hela basi kwenye dokezo lazima na yeye awekwe la sivyo hupati kitu. Imekuwa ni kero na moyo wa kufanya kazi kwa watumishi wengi unapotea kabisa zaidi watu wanakaa tu ofisini bila kazi zozote. Inafika wakati hata wino wa printer tu halmshauri nzima hakuna? Wakati kwenye riport za fedha tunaona expenses zenye figure kubwa tunajiuliza hela zinatumika wapi?

Naomba siku moja uje na uje kwa kushitukiza kama sehemu nyingi unavyofanya. Ukija huku utajua kama tukae au tufanyanye nini? Pia Mweka hazina mimi nina wasiwasi naye kwani malalamiko yamekuwa mengi sana tunaomba tuletee mwinginge.Tutashukuru kama tutajengewa ofisi za halmashauri kwani kukaa madarasani si vema. Karibu sana halmashauri ya Momba.
 
TRA kuna nini!? Mpaka leo pale Kariakoo kuna baadhi ya maduka makubwa tu hawatumii mashine za EFDs kutoa risiti.

Pamoja na juhudi zao zote za kuibadilisha Kariakoo kuwa mkoa maalum wa kikodi lakini bado ni blablaa tu.

Jamani tumsaidie rais Magufuli kuijenga hii nchi...
 
Kama kweli TZ inataka kuwa ya viwanda hakuna namna zaidi ya kuiwezesha SIDO, itengeneze mashine za bei nafuu na kuwakopesha vijana/akina mama ili waweze kujiongezea kipato na kuajiri wenzao.

TZ inahitaji angalau viwanda 10,000 vya kuajiri watu 10 mpaka 20, hapo ndipo tutakaposonga mbele, otherwise tutaenda hatua 10 mbele tutajarudi 15 nyuma
 
Kwanza napenda kupongeza juhudi za Rais wetu kwa jitihada anazozifanya katika kuhakikisha matumizi ya pesa za Serikali yanakuwa katika taratibu nzuri na pia kuzuia mianya yote iliyokuwa ikitumika kutumia pesa ya serikali kwa kinyume cha utratibu.

Nampongeza sana kwa hilo na hasa kurejesha adabu kwa kiasi kikubwa kwa watumishi wa sekta ya umma.

Kitu ninachopenda kumshauri muheshimiwa Rais (AFYA) ni kujaribu au kutekeleza kwa haraka upatikanaji wa mahitaji ya huduma za afya.

Naona kama hili lina msingi mkubwa kwa maisha ya kila mtanzania kabla hata ya kufikiria kuwa na shirika zuri la ndege linaloendehwa kwa faida wakati mamilioni ya watanzania afya zao zikiaathirika kwa kukosa dawa na vifaa tiba.

'Hapa kazi tu' ina nia njema kwa taifa letu ila wananchi wenye uhakika wa afya zao wataitekeleza kauli hiyo vizuri kabisa. Mie ningesema afya kwanza.

Dawa & vifaa tiba pamoja na watumishi wa kutosha kwenye hospital zetu.

'ELIMU' Eneo ambalo muheshimiwa angelipa uzito mkubwa baada ya kuaanza na Afya, hapa tunategemea kupata viongozi na wataalamu wa taifa hili. Wataalam walio na 'quality package' ya maarifa ya utaalamu wa walichosomea, HAPA KAZI TU, 'Quality' ya hiyo kazi ni agenda ya msingi pia sio kazi tu isiyo na tija.

Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki Rais wetu.
 
Binafsi ni mtu ambaye naunga mkono juhudi za mh Rais..

Lakini napata shida na ile kauli ya mh Rais, hawa Polisi hawakai barabarani, reflection yake hasa ilikuwa ni nini?

Nikifikiria kwa mbali kama aliruhusu wale wa kipato cha chini, kuendeleza vitendo hvi vya rushwa na ambavyo kwa mwendelezo wake hawa Polisi watakuja kushika nafsi za juu ndani ya Jeshi, hawataitwa tena wala rushwa bali mafisadi.

Hakuna mahala kwa sasa panapoleta shida kwa wananchi wa kawaida kama ofisi za Jeshi letu la Polisi na mahakama...

Kwa upande wa Rais JPM, nilipenda alifanye jeshi la polisi liwe la kizalendo, kuliko kuchochea au kuchagiza vitendo vya rushwa ndani yake.
 
Hakuna, siyo kweli. Tatizo la mkuu ni vitu vichache vinavyowafanya walio wengi kuona afadhali ya ufisadi kuliko yanayoendelea.
1. Matumizi ya hela za serikali bila kibali cha bunge- splurge
2. Kuua democrasia
3. Kukanyaga sheria na Katiba
4. Condemning suspects unheard- violation of one of the cardinal principle of natural justice
5. etc, etc, etc, etc, etc

Otherwise kukabiliana na mafisadi ni jambo jema tu!
1. Matumizi ya hele za serikali bila kibali change kwa manufaa ya nchi ni bora kuliko matumizi ya hela ya serikali iliyoidhinishwa kwa manufaa binafsi
2. Kama demokrasia ni kushinda kwenye maandamano kwa gharama ya uzalishaji mali bora isiwepo
3. Kiongozi anaetumia katiba kutuibia ni mbaya kuliko asiyekumbatia siasa za katiba kwa ustawi wa nchi
4. Ni upumbavu kuendelea kukaa na mzembe, mbaridhifu, kwa kizingizio cha natural justice. Some cases are justified by default
NO NONESENSE HAPA KAZI TU
 
1. Matumizi ya hele za serikali bila kibali change kwa manufaa ya nchi ni bora kuliko matumizi ya hela ya serikali iliyoidhinishwa kwa manufaa binafsi
2. Kama demokrasia ni kushinda kwenye maandamano kwa gharama ya uzalishaji mali bora isiwepo
3. Kiongozi anaetumia katiba kutuibia ni mbaya kuliko asiyekumbatia siasa za katiba kwa ustawi wa nchi
4. Ni upumbavu kuendelea kukaa na mzembe, mbaridhifu, kwa kizingizio cha natural justice. Some cases are justified by default
NO NONESENSE HAPA KAZI TU

Kwenye dictatorial regime your propositions are nicely applicable not in a democratic regime. We ni dictator mimi ni democrat tuna mitazamo tofauti
 
MTO NYAKASANGWE BOKO
Hili ni jipu kubwa sana na madhara yake ni dhahiri. Kuna magari yanasomba mchanga unaochimbwa kwenye kingo za mto Nyakasangwe. Mto umetanuka kupita kiwango ambapo kuta zake zimebomoka na zinaendelea kubomoka. Nyumba za watu zilizokuwa mbali na mto sasa nyingine zimeshafikiwa na mto na nyingine zinaendelea kufikiwa ambapo wengine wamezihama nyumba hizo. Tatizo ni Polisi wa kituo cha Wazo Hill ambao wamekithiri kwa rushwa. Wanashirikiana na hawa waharibifu wa mazingira kwa wao kulipwa hela mbaya zaidi wanatumia magari na pikipiki za serikali ambazo kodi zetu zinagharamia kuwalinda hawa waharibifu. Mfano ukipiga simu waje wawakamate wanakuja na kuchukua hela na wanaondoka zao. Kuna siku wameenda na lundo la askari wapya ambapo mgao wa rushwa ulienda ndivyosivyo wakaanza kugombana wenyewe kwa wwenyewe mbele ya wananchi. Imefikia sasa kila mtu anaangalia tu hana tumaini na polisi kama msaada na waharibifu hawa wanaendelea. Siamini kama watu wa mazingira hawalioni, TISS hawalioni na mamlaka nyingine au huu mgao unaenda mpk ngazi za juu??? Serikali ya mtaa wamekwama maana polisi wanashirikiana na wahalifu. Kama kuna mtu anawezasaidia na anasoma saidia maeneo haya hali ni mbaya kiwangi cha uharibifu ni kikubwa kiasi huwezi amini kama ni hatua chache kutoka barabara ya kwenda Bagamoyo.
Eneo Boko nyuma ya kanisa la KKKT au ukifika kituo cha Calfonia au Kwa Mpemba dakika mbili tu kwa miguu utafika eneo la mtu na kushuhudia kinachoendelea hapo
 
Kwanza kabisa,ninge imarisha utaifa kwanza. zen after zile serious cases like IPTL ,Lugumi,symbos(dowan's,Richmond),EPA,samaki wa Magufuli ,Malawi boundaries,......etc.

Ningejiakikishia ushindi how? ningewakusanya pamoja wanasheria wa upande wote kama vile wakina Mabere Marandu,Tundu Lissu,Kibatara,Dr. Tulia,mh Chenge. Ninge deal na manguli wa sheria, pia ningewajumuisha wanauchumi kama Zitto Kabwe,Prof. Lipumba n.k

Pia nisingewaeka pembeni wana dipromasia kama vile waziri wetu wa mambo ya nje wa sasa.

Naamini utawapaisha kisiasa watu fulani fulani lakini na wewe utakuwa umeokoa tsh yetu kutokwenda kwa wachache wanufaika.

Natambua kuna baadhi ya watu watahoji kwanini wanauchumi na wanadipromasia. Jibu rahisi, ni kwamba huwezi kupika mboga bila ya kuchanganya chumvi,vitungu,maji kiasi...nk.

Kwahiyo umoja wake utaleta ushindi wa kesi tunazozishindwa siku zote.

Naamini ukitumia 1bil kwa ajili ya kuwakutanisha na kuratibu na kuziendesha zile kesi zote tunazozishindwa kupitia wanasheria wetu wa siku zote naamini ushindi tutapata.

Pia huenda hata pesa usiwape ama wanaweza wasichukue ila wanatumia nafasi ya kujitambulisha zaidi kisiasa.

Aya ni mawazo yangu msinihukumu vibaya.

Mchana mwema nawatakia.
 
Hali ya usalama jijini Dar bado ni ya mashaka.

Ninaomba vyombo vya dola vifuatilie maeneo ya BULULA,GOLANI na MATOSA katika kata ya Saranga.

Maeneo hayo yanasemekana kuhifadhi wahuni wanaokimbia operesheni kali za jeshi la Polisi katika maeneo mengine ya mji haswa Manzese ambapo inasemekana wengi wa wahuni hao ni mabaki ya makundi ya MBWA MWITU na PANYA ROAD.

Hivi karibuni kumeanza kuibuka uhalifu wa kupora watu,watu kushambuliwa na vikundi vya wahalifu na kukatwa mapanga huko Matosa, Bulula na Golani.

Sasa hivi kuna taarifa kwamba wahalifu hao hasa kutoka Bulula na Golani wanakwenda hadi Kimara Suka na Kimara stop over nyakati za usiku na kufanya uhalifu kwa kushirikiana na makundi ya wahuni wa Suka,Stop over na Matosa.

Taarifa zinafika Polisi Kimara na Mbezi lakini zinapitishwa defender mbili tatu kwa siku moja au mbili bila ya kukamata wahusika halafu kimyaaa, wahuni wanazidi kuvimba vichwa na kuzidisha uhalifu mitaani.

Naomba mamlaka za juu za kiserikali na vyombo vya usalama kutokupuuzia suala hili,haswa makundi yanayojiunda upya huko Bulula na Golani.

Msikurupuke,fanyeni uchunguzi wa kina kujua nini kinaendelea,tumeni watu toka mbali kwani hawa askari wenu wanaohusika na maeneo hayo (Mbezi) wako compromised.

Pia suala hili limulike Dar yote,wahuni wana syndicate zao siku hizi.

Wana mitandao ya kimaeneo jijini na wanasimamiwa na tycoons wenye pesa,maarifa,mikakati na masoko kwa ajili ya biashara zao haramu.

Wana mitandao hadi kwenye bodaboda na madereva taxi.

Pale Ubungo kulikuwa na wizi lakini tangu kituo kihamie mawasiliano na wizi nao umehamia huko na maeneo ya zile njia za pembeni kuelekea Mlimani city.

Mmeshawahi kwenda kuchunguza nini kinaendelea chini ya yale madaraja ya Ubungo?

Nasikia mali nyingi zinazoibwa eneo la Ubungo zinapatikana chini ya madaraja yale. Fuatilieni.

Haya makundi msiyape nafasi,maana watu wenye pesa na exposure kubwa ya maisha wameanza kuyageuza dili na kuyatumia,hivyo kuwapa mbinu zilizoenda shule.

Msipojipanga na mkipuuza jiji halitakalika hili huko mbele.

Halafu vita ya vijiwe vya madawa na bange inawashinda nini jamani? Watoto wanaharibika. Vijiwe vya wahuni ndio center za kuuza bidhaa hizo na niwaambie jambo moja msilolijua akina Makonda na wenzio, HOMOSEXUALITY IS VERY COMMON THERE.

Wahuni wengi wanaotumia madawa na bange wanafanyiana huu ushenzi,saaana tu, ni siri zao. Msikurupuke, fanyeni uchunguzi, mtajua meengi sana, halafu anzisheni operesheni zenye malengo,mkiwa na uhakika where to hit and how and when.

Mwisho ninawaasa wazazi wenzangu wenye watoto wenu boarding schools. Hawa wahuni na vijiwe vyao wana wateja wengi wa bangi huko boarding schools wanawapelekea. Sijui walimu na walinzi wa hizo shule wanakuwa wapi. Sasa bangi ya leo sio ile mliyokuwa mkivuta nyinyi enzi zenu. Bangi zao wanachanganya na unga humo humo. Wakikosa kabisa huchukua valium,bangi na gundi ya viatu wanachanganya humo. Huyu mvutaji wa hiyo kitu ukikutana naye usiku akikunyanyulia panga akate sikio, harudishi mkono bila sikio lako.

Kama mnajali jamii yenu basi fanyieni kazi taarifa mnazopata.
Serikali mmefikia wapi katika hili?
Tunaandika na kuwasaidieni sana nyinyi wana usalama lakini hamtumii fursa hii ya faida za mitandao ya kijamii.
Angalia sasa mambo yanazidi Dar nzima,mara Panya road,mara Taifa jipya n.k
Mbona zamani tulifanikiwa kuyadhibiti haya makundi,sasa hivi kuna tatizo gani?
Je,tatizo liko ndani ya jeshi la Polisi?Je,tatizo ni jamii nzima?
Tujitafakari ila wakati wa kuzuia ni huu,tukichelewa tutajuta.
 
Tuliambiwa. kuwa mh akushinda kuna watu wataishi km mashetani mbn nawaona maskin ni wengi zaid kuliko matajiri

maskin ndio walitolewa kwa fedheha pale hananasif na jangwani

maskini vijana wao wamekosa mikopo kwan walisoma shule za kata hawaweZ kuafford.

kukosekana increment kwa wafanyakszi limewauma kwan gharama za maisha zimezidi

ajira kwa watoto wa maskin imesitishwa ni muda sasa. vijana wapo mtaani

maskini waliopaza sauti kuwa wananjaa, matokeo alieripoti anachukuliwa hatua.

watu wamepata tetemeko LA ardhi lakin kila MTU ni shahidi kilichotendeka kwa watu hawa.

bodaboda,machinga,mama ntilie bado wanataabika,traffic,mgambo wanakaza buti

lastly angalia kule srusha maskin wanajengewa hospitali serikali inafanya figisufigisu

sasa tazama matajiri walioambiwa wataishi km mashetani

LWAKATARE ANAPIGA JUICE NA JENGO HAMNA WA KULIVUNJA
HARBINDER SIGH BADO TUPO NAE
WATUHUMIWA WA ESCROW WANAENDELEA KULA NEEMA
LUGUMI AND COMPANY WANAKULA MAISHA
HOME SHOPPING CENTER WANAKULA BATA
WALIOPITISHA MAKONTENA WALIPEWA SIKU 7 WALIPE KODI WAENDELEE KULA MAISHA

JIULIZE KUNA TAJIRI KAISOMA NAMBA AU NI SISI WANYONGE?
 
Habari wanajamvi..........

Tangu uchaguzi ukamilike na hatimaye Mh Magufuli kutangazwa kuwa Rais wa awamu ya Tano nimekaa chini na kutafakari haya!!!

Kwanza,
Mzunguko wa pesa umekuwa mdogo sana mtaani pesa hazionekani na zikionekana ni kwa muda mfupi,
Kwann hali hii inatokea??

Nimewaza na kutafakari but sijapata jibu

Pili,
Hali halisi ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu,kiukweli wana hali mbaya sanaaa hii inaweza kusababisha dada zetu walioko huko kufanya biashara haramu ya kuuza miili yao ili kumudu maishaaaa

Tatu,

Kuondolewa kwa watumishi hewa umefanya mishahara iongezeke Mara dufu hii inatokana na Utumbuaji usiofuta misingi ya sheria na hatimaye kuendelea kupokea mishahara kama watumishi halali ingawa wapo nje ya ofisi

Namshauri rais akitumbua,atumbue na mshahara

Haya yote yanatokea ni kwa sababu ya Elimu bure!
Elimu bure inaigharimu sana serikali pesa nying sana

Naishauri serikali ya Mh John Pombe Magufuli ikae chini na kuangalia upya hili swala la elimu bureee

Bila kuchukua hatua dhidi ya utoaji wa elimu bure kamwe hatutapiga hatuaaaaa kwenye secta zingine Kama Afya,maji,nk

Karibuni wanajamvi....




.
 
Mtu keshaomba mitandao izimike japo kwa miaka mitano halafu leo hii unamshauli kupiti mitandao ya kijamii!!!?
 
Kiongozi wa nchi anayeijua kaziyake sikuzote atapigania wananchi wake waishi maisha mazuri...haihitaji akili kubwa kujua kwasasa wananchi wanamaisha magumu sana kuliko miaka mitano iliyopita.
- vyuo vinakosa wanafunzi na malecturers wanapoteza kazi.
- watumishi hawapewi stahili zao kwa wakati nawengi wamezidiwa madeni.
- wafanyabiashara haliyao ningumu na nyingi zinafungwa (mahoteli,bar,maduka nk)
- mashuleni pamoja na elimu bure vifaa na mazingira ya kusomea nimabovu sana. Vifaa vya elimu vitendo hamna,dawa vyooni nishida,mipira kununuliwa shida,mitihani kuchapwa tabu,ukimwagiza mwalimu inabidi aende kwapesa yake (kama nauli).
- wakulima/wafugaji nitabu,malisho shida,mvua kidogo na kilimo cha umwagiliaji ni hadithi,soko la mazao tatizo yaani tabu nyingi.
SWALI NI JE,SERIKALI KUU INAYAJUA MADHILA HAYA? LAKINI SWALI LA MSINGI NI ARE THEY PART OF THE SOLUTION OR PART OF THE PROBLEM?
 
Kiongozi wa nchi anayeijua kaziyake sikuzote atapigania wananchi wake waishi maisha mazuri...haihitaji akili kubwa kujua kwasasa wananchi wanamaisha magumu sana kuliko miaka mitano iliyopita.
- vyuo vinakosa wanafunzi na malecturers wanapoteza kazi.
- watumishi hawapewi stahili zao kwa wakati nawengi wamezidiwa madeni.
- wafanyabiashara haliyao ningumu na nyingi zinafungwa (mahoteli,bar,maduka nk)
- mashuleni pamoja na elimu bure vifaa na mazingira ya kusomea nimabovu sana. Vifaa vya elimu vitendo hamna,dawa vyooni nishida,mipira kununuliwa shida,mitihani kuchapwa tabu,ukimwagiza mwalimu inabidi aende kwapesa yake (kama nauli).
- wakulima/wafugaji nitabu,malisho shida,mvua kidogo na kilimo cha umwagiliaji ni hadithi,soko la mazao tatizo yaani tabu nyingi.
SWALI NI JE,SERIKALI KUU INAYAJUA MADHILA HAYA? LAKINI SWALI LA MSINGI NI ARE THEY PART OF THE SOLUTION OR PART OF THE PROBLEM?
Hali ni mbaya kwa kweli
 
Habari wanajamvi..........

Tangu uchaguzi ukamilike na hatimaye Mh Magufuli kutangazwa kuwa Rais wa awamu ya Tano nimekaa chini na kutafakari haya!!!

Kwanza,
Mzunguko wa pesa umekuwa mdogo sana mtaani pesa hazionekani na zikionekana ni kwa muda mfupi,
Kwann hali hii inatokea??

Nimewaza na kutafakari but sijapata jibu

Pili,
Hali halisi ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu,kiukweli wana hali mbaya sanaaa hii inaweza kusababisha dada zetu walioko huko kufanya biashara haramu ya kuuza miili yao ili kumudu maishaaaa

Tatu,

Kuondolewa kwa watumishi hewa umefanya mishahara iongezeke Mara dufu hii inatokana na Utumbuaji usiofuta misingi ya sheria na hatimaye kuendelea kupokea mishahara kama watumishi halali ingawa wapo nje ya ofisi

Namshauri rais akitumbua,atumbue na mshahara

Haya yote yanatokea ni kwa sababu ya Elimu bure!
Elimu bure inaigharimu sana serikali pesa nying sana

Naishauri serikali ya Mh John Pombe Magufuli ikae chini na kuangalia upya hili swala la elimu bureee

Bila kuchukua hatua dhidi ya utoaji wa elimu bure kamwe hatutapiga hatuaaaaa kwenye secta zingine Kama Afya,maji,nk

Karibuni wanajamvi....




.
Hiyo namba mbili wanafanya kitambo indirect sema labda wafanye direct
 
Back
Top Bottom