Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

1.hataki mijadala.. Mijadala ipi mbona TAASISI nyingi tu zinaendelea na vikao kuhusu masuala yao ya kiutendaji. Mijadala Gani unataka
2.kaiba CHETI, ukiambiwa ulete ushahid unasema Gwajima KASEMA kwanini rais a deal na mambo ya mitandaoni tena mepesi kama haya. Hivi kweli upo serious una amini kaiba CHETI.
3.kuvunjia watu nyumba Unaamini anafanya yeye kabla ya mamlaka husika kufanya uchunguzi na kugundua madhara yatakayokuja.. Embu assume we ni rais na una roho mbaya je kuvunja nyumba za watu unapata faida Gani. Rais ananufaika vipi hapo.. Jamani amkeni ndugu ZANGU serikali ina vyombo vingi wakati mwingine kutimiza majukumu Yake unamuona rais anamkosea mmiliki wa nyumba inayoweza kuingiza maji na kuua watu.
4.fedha zimetumika kufanya jambo Zuri la kuchangia madawati bado tu na Hilo huhitaji kuskia ndugu
5.hivi magufuli kuwaelekeza mahakama kwamba washughulikie kesi haraka nako amekosea? Ila ikumbukwe yeye ni mkuu wa nchi anasimama juu ya mihimili mingine Ila kizuri Anatoa maelekezo ambayo kikatiba yuko sawa
6.ni kosa rais kutoa mwelekeo wa serikali Yake Kanisani.. Na wakati kanisa linakuwa linajua kuwa kutakuwa na ugeni wa mkuu wa nchi. Kosa hapo silioni
7.kumpandisha mtu cheo Utaratib wa nini wakati katiba Inasema kabisa yeye ndio amiri jeshi mkuu.. Mamlaka hiyo yapo chini Yake..
8.hataki kusoma hotuba. Kavunja sheria Kivipi na hayo unaposema madudu HAUPO sawa. Rais ni amiri jeshi HUTAKI aongoze watu Sasa nini maana ya kuwa rais. Mwelekeo wa serikali Yake atautoaje Bila kuongeza maneno anayoyamini
Mimi nasema kwamba magufuli anafanya vizuri Sana Ukitulia na ukijua kuwa tuluchelewa kupiga hatua, hutampinga magufuli.. Pamoja na mapungufu aliyonayo madogo bado anatufaa Sana

Wewe bwana JOHN utakua m.bwa kasoro mkia....huu uzi ufutwe maana alieuleta ana majibu ya ki.maandazi sana....bashite wewe.
 
Katiba ya Tanzania imeelekeza kila kitu kinachotakiwa kufuatwa na Rais wa Tanzania .

Mwl Nyerere aliwahi kusema hivi , nanukuu " HATA KAMA TUTACHAGUA ASIYEAMINI MUNGU , TUTATAFUTA NJIA YA KUMUAPISHA , NA NI LAZIMA AAPE KWAMBA ATAILINDA NA KUITETEA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA " Mwisho wa kunukuu .

Kwahiyo kinachohitajika hapa si jambo alilolifanya , anachotakiwa ni kufuata katiba ya Tanzania aliotumia kuapa .
 
Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
Aondoe kwanza double standard alioanza kuifanya coz matunda yake ni mabaya sana. Aseme ukweli kuhusu Daudi bashite either in possitive way or negative maradi tu tuelewe coz jamaaa kulia mbele za watu kuna jambo limejificha. Pili usemi wa wabunge kuwa halina linachofanya alivunje basi coz tunalipa kodi zetu bora zikajenge barabara na kazi nyingine.kwanza wabunge wote wa ccm washakuwa na say moja hawana tena uhuru wa kimawazo wanaona wanaonewa na kila mtu anajilinda kivyake ccm imekuwa akili ya mtu mmoja anakatanza mpaka wabunge kutembeleana tena kwenye matatizo[emoji36]
 
Aanze kumtaka kila mtu kujieleza mali alizo nazo amezipataje, na zilibganishwe na kipato chake, kama kipato chake hakufanani na Mali aluzo nazo basi mali hizo amezioata kwa ufisadi, ubadhirifu, rushwa, kutumia madaraka vibaya na kufanya biashara ya kulevya.
 
Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
Awarudishe kazini wale wananchi wanyonge aliowafukuza kazi kutokana na kukosa sifa ya cheti ingawa walikuwa wakichapa kazi..
 
Asimamie Mafuta yashuke bei. Ayapunguzie makodi ya kinyonyaji. Both Mafuta ya kula,diesel na Mafuta ya taa.
 
Uvuvi haramu haramu hasa mabomu bahari ya hindi, serikali wameshaambiwa sana lkn mabomu bado yanalia,kumbuka uvuvi huu ukikomeshwa samaki atapatikana kwa wingi bei itapungua hivyo kuwawezesha wafanyabiashara kuwapeleka samaki mikoa ya mbali
 
Aanze kumtaka kila mtu kujieleza mali alizo nazo amezipataje, na zilinganishwe na kipato chake, kama kipato chake hakifanani na mali alizo nazo basi mali hizo anyang'anywe maana amezipata kwa wizi wa mali za umma, amefisadi, amebadhirifu na kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
 
Hizo double standard ni yeye anafanya au vyombo husika.. Kama ni yeye anamuoenea mtu Sasa wewe unakuwa unajuaje kama ni kweli kaonewa au katenda kosa kweli.. Kati yako na rais Nani anauwezo wa kupata taarifa nyingi achilia mbali usahihi wa hizo taarifa... Na kama ni yeye anafanya double standard kutokana na KAULI zake je akiamua kuwa km bubu akawa anafanya kazi na haonekani public mara Kwa mara..je utaridhika?
Hata wakifanya wasaidizi inahesabiwa kafanya yeye maana ndio mwenye mamlaka ya juu kuliko wote.

Akimuonea au kumpendelea "mtu" hua inaonekana wazi bila kificho.

Rais ndiye mwenye taarifa nyingi kuliko Mimi lakini kuhusu USAHIHI wa taarifa anazopewa sina uhakika bkoz inaonekana baadhi wasaidizi wanatoa taarifa za uongo kwa NIDHAMU YA WOGA.

Mwisho kama ameamua kukaa kimya na kulitendea kazi kibubu bubu basi shaka ondoa maana matunda ya kazi yake yatakua bayana.
Yesu alisema "Kama hamniamini Mimi basi ZIAMININI KAZI NINAZO ZITENDA" Yaani kazi yenyewe haileti maswali kwa wanaoiona. Na "zake" zikiwa wazi tutaamua kuziamini ama la!

Karibu tena!
 
Hakuna moja, kuna elfu moja na moja.

Magufuli hataki mjadala, ana hulka ya udikteta, anajiona anajua kila kitu, kasema watu watalimia meno. Kasema wasio na nauli watapiga mbizi.

Anafuga mtu aliyeiba mpaka jina na kufoji vyeti, huku akijinadi anapiga vita waliofoji vyeti.

Hana muelekeo wa kisiasa unaoleweka. Leo anaweza kuvunjia nyumba watu mabondeni bila simile (si mtetezi wa wanyonge) kesho akaachia Wamachinga wafanye biashara bila mipango (anatetea wanyonge bila mpango endelevu).

Magufuli haheshimu uhuru wa bunge, kalipangia bunge jinsi ya kutumia fedha za tafrija bila hata makubaliano na Spika.

Magufuli haheshimu uhuru wa bunge. Kaapisha wabunge wa kuteuliwa wawe mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge.

Magufuli haheshimu uhuru wa mahakama. Kahutubia mahakama na kuzielekeza jinsi ya kufanya kazi wakati mahakama ni mhimili unaojitegemea.

Magufuli hathamini utenganifu wa serikali na kanisa. Anahutubia habari za kisiasa makanisani. Hili linaweza kuleta mtafaruku na mpasuko wa nchi kidini. Nyerere alikuwa anasali St. Peters kila siku akiwa Dar. Mwinyi aliswali sana Msikiti wa Tambaza. Mkapa alisali sana kanisa la St. Immaculata. Kikwete naye pia motto wa Bagamoyo msikiti anaujua. lakini wote hawa hawakuwahi kuhutubia siasa kwenye madhabahu ya dini to my knowledge, ukiondoa maneno machache tu ya shukurani labda.

Huyu Magufuli anatoa hotuba ya siasa kabisa, kanisani!

Magufuli hatahamini utawala wa sharia. Kawaambia Polisi wakiona gari la kawaida linaenda kwenye lane ya mwendokasi, walichukue, walipeleke polisi, watoe matairi, mwenyewe akija kuulizia matairi wamwambie lilikuja hivyo hivyo bila matairi.

Magufuli hana heshima hata kwa mawaziri wake. Anawaruka bila hata uchunguzi. Mke wa Waziri wake wa karibu kaonewa/ wamepishana maneno kidogo na trafiki, jibaba kaingilia issue na kuvunja utaratibu wa mtu kupandishwa cheo polisi.

Magufuli hataki hata kusoma hotuba anazoandikiwa, matokeo yake anasema madudu.

Magufuli anapenda maamuzi ya ghafla na jazba ambayo hayajachekechwa vizuri na mara nyingine yana athari kwa taifa.

Magufuli ana kauli za kijinga kama motto anayebalehe, ona alivyomdhalilisha Mama Kikwet, mke wa bosi wake wa zamani, kwa kumwambia maneno yasiyo staha hadharani.

Magufuli hawezi mijadala ya kisiasa. Ndiyo maana kapiga marufuku mikutano ya siasa ya wapinzani kinyume na katiba.

I could go on and on and on. kwa nini unataka niseme moja tu?

Msingi mkubwa ni kwamba Mgufuli hana uwezo wa kuwa rais.

Mtu kama huyu hafai kuwa kiongozi.
Shikamoo Al Watan (Hata kama nakuzidi umri potelea mbali...)
 
Ajiuzulu tu kwa faida ya wanyonge. Kama mtu mwenyewe anajuta hata kuugombea urais, sitegemei neema yoyote katika utawala wake!
 
Anajenga uwanja wa ndege kule Chato. Ni jambo jema sana hili kwa wanyonge wa kule Chato.
 
PAYE ishuke toka 20% hadi 9%, makato ya loan board kwa wahitimu wa elimu ya juu yashuke toka 15% hadi 5%. Ajira na promotion ziendelee. Aruhusu democracy na Uhuru wa kujieleze na kuhoji kwa upana zaidi
 
Back
Top Bottom