PONGEZI KWA MHESHIMIWA RAIS NA SERIKALI YAKE KWA UJUMLA.
Napenda kutumia fursa hii kutoa pongezi za dhati kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake kwa ujumla.
Kwa kweli mimi binafsi nampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake kwa ujumla kwa kazi nzuri sana na ngumu sana anayoifanya kwa ajili ya kulinda na kutetea rasilimali kuu za Taifa letu.
Lakini pia nampongeza kwa kazi nzuri sana ya ku deal na MAJIZI na MAFISADI yaliyokuwa yameshamiri katika nchi hii.
Baba wa Taifa mwl. Julius Kambarage Nyerere(Mwenyezi Mungu amrehemu) aliwahi kusema:
Nchi inapoingia kwenye vita kama hivi hujitokeza WAPUMBAVU/VIBARAKA wengi ambao kazi yao kubwa itakuwa ni:-
(1)Kuwatetea MAJIZI kutoka nje na hata kuungana nao.
(2)Kuifitinisha serikali na wananchi wake lengo lake likiwa ni kuifanya nchi kuwa katika taharuki muda wote.
(3)Kutengeneza matukio ya ovyo ili tu serikali iweze kulaumiwa na jamii mbalimbali zikiwemo za kimataifa.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi naomba uendelee na msimamo huu huu. Hivi ndivyo ipendezavyo. KAMWE usiwape nafasi wapumbavu niliowataja hapo juu, wasije wakatuingiza shimoni.
MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU wabariki vingozi wa nchi hii, uwalinde dhidi ya ovu lolote lile, uwajalie mshikamano na umoja wa kweli baina yao na hatimaye utujalie mafanikio makubwa ya kiuchumi hapa nchini. Amina.