Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Jipu langu lipo upande wa ardhi,huko wilayani misungwi kuna watu wanadhulumu ardhi.enzi za mwalimu nyerere kulikuwa na kuamishwa vijiji unatolewa sehemu uliyokuwa unaishi unapelekwa sehemu Nyingine.cha ajabu kumetokea watu wanaojiita wamiliki wa sehemu hizo wanawaondoa waliopewa maeneo hayo miaka ya sabini na serikali ya awamu ya kwanza je haki iko wapi?naomba mlifikishe sehemu husika.wilaya ya misungwi kijiji cha ngaya
 
Kwanza nianze na kutoa pongezi kwa kazi nzuri zinazofanywa na serikali ya awamu hii inayoongozwa na JPM.
Lakini kwa upande mwingine naomba kuuliza mambo yafuatayo:-
(1)Hivi ni kweli serikali inashindwa kuwapa FUNDISHO kali wasaliti wa nchi yetu ambao wanadiriki kushirikiana na wezi wa mali zetu wanaotoka mataifa ya nje?
(2)Mheshimiwa Rais na serikali yako, kwa nini tunakuwa na kigugumizi kuwashughulikia watu wa mtindo huu?
Kwa kawaida huwezi ku deal na mtu anayefanya kazi ya kujaza maji kwenye pipa badala ya ku deal kwanza na mtu anayetoboa pipa hilo ili lisijae maji.
Hata katika nchi za wenzetu, huwa hawana utani na kikundi au mtu atakayejaribu kuungana na majizi ya mali za nchi husika.
Nchi hizo hutumia gharama zozote zile kuhakikisha wanawanyamazisha hao VIBARAKA.
Mimi naamini kuwa, KIBARAKA ni adui mkubwa mara kumi zaidi ya adui wa nje.
Hata mwl Nyerere katika hotuba zake aliwahi kusema kuwa; nchi inapopambana na majizi makubwa makubwa haya hujitokeza wananchi wasio na UZALENDO ambao huwa ni watetezi wa majizi haya.
VIBARAKA hawa wapo tayari kuona Taifa linaangamia, na hii ndiyo furaha yao.
NDUGU ZANGU, TUKICHEKA NA NYANI TUTAVUNA MABUA.
Naiomba serikali yetu ichukue hatua MUJARABU sasa.
 
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wewe ndiyo Amiri Jeshi Mkuu katika nchi hii.
Sasa unaogopa nini kuchukua hatua kali dhidi ya WAHUNI wachache wanaoisaliti nchi yetu kwa kuungana na MAJIZI?
Mara 100 ni bora kwenda The Hague kuliko kuacha watu wachache wakihangaika usiku na mchana kutaka kuihujumu nchi yetu
 
Huu ni uzi wa whistle blowers kama hamna barabara malizaeni na mbunge wenu hapa leteni nondo za mijitu inayoliibia taifa kwa namna yoyote ile au kama unafahamu mtu aliyejipatia mali kiudanganyifu au wauza ngada huu ndo uwanja wenu
Nani aliyekwambia Mbunge kazi yake kujenga barabara?
 
Uhalifu Mbezi Beach " A"

Sehemu iliyotajwa hapo juu , kiwanja cha mama Maria Nyerere pajulikanapo kama "Rungwe " kuna mabanda yamejengwa ambamo uhalifu wa kila aina unafanywa vikiwamo pombe za haramu, madanguro, uuzaji madawa ya kulevya na hivyo mahala hapa kuwa kitovu cha uharamia unaofanyaka Mbezi Beach pamoja na Goba.

Kinara wa uovu wote unaotendeka hapo ni Mlinzi wa kuwanja hicho ajulikanae kwa jina la Challe ; huyu bwana amefanikiwa kufanya maovu yote haya kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi "A" ambae hupelekewa rushwa ya pesa kila mwezi na kufumbia macho maovu haya kwa jamii. Siluhisho la tatizo la hapa ni kusafisha mahala hapa kwa kubomoa mabanda yote yaliyojengwa kuzunguka Kiwanja hiki. Kiwanja hiki ni cha makazi halali lakini kimegeuzwa danguro kwa kujengwa mabanda ya mabati mengi!!

Wakati wa Mbezi wanategemea kuwa wahusika watasikia na kuchukua hatua haraka.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
huwa anasaidiwa mtu anayetaka kusaidiwa siyo huyu Makufuli mbishi na anajifanya kila kitu anajua
 
Hiki ni kilio kwa raisi naomba ututazame huku kwetu mbozi vwawa songwe tuna pata shida sisi wafanyakaz wa chini mahofisini
Hatujalipwa mshahara huu mwezi wa nne hakuna mshahara mpaka mabinti wanaanza kuuza mwili ili wajikidhi maisha yao jamani
Hebu fikiria miezi mi nne watu hawalipwi na hao ndio watenda kazi katika mji je ? Ndugu zetu maisha yakiwa hivi tunawezaje kupona kama wajuu wana tuminya
DT mbozi vwawa songwe hawalipi wafanyakazi wa mamlaka ya mji wa vibarua ndio watenda kazi katika mji lakini leo ndio wanao ongoza kwa madeni baada ya kukosa kulipwa ndani ya miezi minne.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa Rais wetu John Pombe Joseph Magufuli, sisi watanzania wengi wetu tunaikubali kazi unayoifanya hasa katika kupambana na MABEPARI wa nje na VIBARAKA wake wa hapa ndani.
Tupo nyuma yako. Kwa pamoja tutashinda vita hivi. Kwa kuwa tumeamua kusonga mbele, basi tusirudishe nyuma majeshi.
Tusikubali hata kidogo kugeuka MAWE.
Haya mimi nimezoea kuyaita ni MABADILIKO CHANYA YA KIKEMIA (Positive chemical change ).
Tunapopita kwenye mabadiliko haya, humu njiani tutakutana na KONDOO,MBWAMWITU na MBWAMWITU WALIOVAA NGOZI YA KONDOO.
La muhimu zaidi ni kupambana mpaka mwisho. Maendeleo ya kiuchumi katika nchi yetu yanawezekana.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu umbariki Rais Magufuli na serikali yake.
 
PONGEZI KWA MHESHIMIWA RAIS NA SERIKALI YAKE KWA UJUMLA.
Napenda kutumia fursa hii kutoa pongezi za dhati kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake kwa ujumla.
Kwa kweli mimi binafsi nampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake kwa ujumla kwa kazi nzuri sana na ngumu sana anayoifanya kwa ajili ya kulinda na kutetea rasilimali kuu za Taifa letu.
Lakini pia nampongeza kwa kazi nzuri sana ya ku deal na MAJIZI na MAFISADI yaliyokuwa yameshamiri katika nchi hii.
Baba wa Taifa mwl. Julius Kambarage Nyerere(Mwenyezi Mungu amrehemu) aliwahi kusema:
Nchi inapoingia kwenye vita kama hivi hujitokeza WAPUMBAVU/VIBARAKA wengi ambao kazi yao kubwa itakuwa ni:-
(1)Kuwatetea MAJIZI kutoka nje na hata kuungana nao.
(2)Kuifitinisha serikali na wananchi wake lengo lake likiwa ni kuifanya nchi kuwa katika taharuki muda wote.
(3)Kutengeneza matukio ya ovyo ili tu serikali iweze kulaumiwa na jamii mbalimbali zikiwemo za kimataifa.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi naomba uendelee na msimamo huu huu. Hivi ndivyo ipendezavyo. KAMWE usiwape nafasi wapumbavu niliowataja hapo juu, wasije wakatuingiza shimoni.
MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU wabariki vingozi wa nchi hii, uwalinde dhidi ya ovu lolote lile, uwajalie mshikamano na umoja wa kweli baina yao na hatimaye utujalie mafanikio makubwa ya kiuchumi hapa nchini. Amina.
 
wewe unamkubali siyo sisi. maana sisi wengine wenye akili tumeona udhaifu mkubwa wa Magufuli.
 
Siku Ambapo milio ya SMG itarindima kwenu ndio utatoa pongezi ya dhati,lakini kwa sasa bado unaisikia kwa kwa jirani utaachaje kutoa pongezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAKATI UMEFIKA WATU TUWE WAKWELI.
( 1) UFISADI
Ni vitendo vingapi vya kifisadi vimekuwa vikifanyika katika nchi hii?
Kwa nini hatukuona watu wa HAKI ZA BINADAMU, WATU KUTOKA TAASISI MBALIMBALI nk, wakipaza sauti zao kupinga ufisadi kwa sauti ya kusikika?
Kwa nini hatukufanya MAANDAMANO kupinga ufisadi?
Iweje Leo?
(2)UHUJUMU WA MADINI
Kuna vitendo vingapi vya uhujumu wa madini yetu vimefanyika?
WATU WA HAKI ZA BINADAMU, TAASISI MBALIMBALI nk, walikuwa wapi kupaza sauti zao kwa nguvu zao zote na kwa kusikika vizuri?
Iweje Leo?
(3)MAUAJI YA KIBITI NA MAENEO MENGINE.
Kuna watu wangapi wameuawa KIBITI NA MAENEO MENGINE?
Kwa nini hatukuona watu wa HAKI ZA BINADAMU, TAASISI NA VIKUNDI MBALIMBALI wakipaza sauti zao kwa nguvu zao zote na kwa kusikika vizuri na hata kufanya MAANDAMANO kupinga maovu yale?
Iweje Leo?
Mimi siungi mkono maovu yoyote yale hapa nchini lakini napenda sana haki na ukweli.
Naomba ndugu zangu watanzania tuwe makini sana katika kuchukua hatua dhidi ya mikasa inayotupata, tujitahidi sana kutenda haki katika kutoa judgement(hukumu) zetu.
Mungu wetu huwa hapendi unafiki.
MUNGU ATUEPUSHE NA MIKASA MBALIMBALI HAPA NCHINI.
 
Uzi maalumu wa kufichua rushwa wizi na mapato ya serikali na umma

Kumekua na upotevu mkubwa sana wa pesa za umma hasa kwenye mifumo mingi ya ki electronic mapato mengi yanaishia mikononi mwa watu binafsi
 
MHESHIMIWA Rais JPM, songa mbele, usisikilize za watu hawa. Watu wa mtindo huu walishatabiriwa na Baba wa Taifa tangu enzi za uhai wake. Kwa hiyo hawa wasikutishe. Watapiga kelele za kila aina, watatengeneza matukio ya kila aina, watafanya njama na mikasa ya kila aina lakini mwisho kabisa WATASALIMU AMRI, na nchi itasonga mbele.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali yake. Amina.
 
kero Yangu ni watu kuokotwa coco beach wakiwa wamekufa huku dalili zote zikionyesha waliteswa kisha kuwekwa kwenye mifuko na kutoswa baharini. hii ni kero kubwa kushinda zote. watu wore tukiisha maendeleo hayana maana tena.
 
Wakazi wa Chanika Mjeule tunapata tabu kipindi cha mvua,kwani tunashindwa kupita kwenda makazini kwasababu mto hujaa maji! Tunaomba kero hii itatuliwe kabla mvua hazijaanza
 
Back
Top Bottom