Binafsi napenda kutumia fursa hii adhimu kuendelea kumshukuru na kumpongeza mheshimiwa Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Serikali yake yote kwa kazi njema wanazozifanya kwa ajili ya watanzania.
Zaidi sana natoa pongezi zangu kwao kutokana na UZALENDO usio na mashaka walio nao na unaoonekana kwa wazi kabisa.
Hapa katikati kumekuwa na shutma nyingi sana dhidi ya hawa viongozi wetu. Lakini kwa mtazamo wangu nimeona shutuma hizo hazina ukweli ndani yake.
Mimi naomba tumwache Rais afanye kazi yake ya kuwaletea watanzania maendeleo.
Kwa hakika, kazi hii ya kutetea rasilimali za nchi inayofanywa sasa kama ingefanywa kikamilifu tangu awamu zote zilizopita nchi hii ingekuwa mbali sana kimaendeleo.
Sina maana kwamba awamu zilizopita hazikufanya kitu, la hasha, kila awamu imefanya mengi tu mazuri.
Nihitimishe kwa kuwaomba watanzania tumuunge mkono Mh. Rais wetu, kwani hizi rasilimali anazopigania si kwa ajili yake na familia yake bali ni kwa ajili ya watanzania wote. Amina.