Binafsi nashauri aangalie swala la watendaji hasa wakuu wa idara namna wanavyopatikana.
Kumekuwa na undugu sana katika jambo hili. Watoto wa maskini wanakaimishwa miaka nenda rudi bila marupu rupu wala kifuta jasho afu unakuta mtu ana ndugu yake pale utumushi au tamisemi basi analetwa na kuthibitishwa fasta..
Kimsingi hii imekuwa haina tija sana kwa taasisi za umma.
Nakumbuka Mh Rais alisititiza kuwa mtu ateuliwe kwa utendaji wake wa kazi pamoja na nidham yake katika kazi.
Pili Mh aangalie utofauti wa mishahara kati ya watumushi wa mashirika ya umma, watumishi wa serikali za mitaa na serikali kuu.
Mwisho. Mh aangalie aina mpya ya ulaji wa watumishi wa umma. Unakuta mradi wa milioni 78. Unafuatiliwa eti na wakaguzi kutoka mfano..CAG, TAMISEM, PPRA, WIZARA YA FEDHA, RAS, PCCB. na ikumbukwe hao wote wana approach tofauti tofauti.gharama za mafuta, matengenezo ya magar. Wengine night siku 10, wengine 7, wengine watahitaji fedha kidogo ili wasiandike hoja, yan vurugu ni nyingi hasa huko halmashauri. Mwisho wa siku gharama ya ufuatiliaji ni M 156 na gharama za mradi ni M 78. Jumla ya gharama za usimamizi na mradi ni M200+.
Nadhan ifikie wakat dhan ya value for money iwe isiwe ya maneno..iwe katika vitendo.