Hakuna hatua tumepiga Mkuu, ukilinganisha na miaka 60 ya uhuru haya yote yalitakiwa kukamilika ndani ya miaka angalau mitano, waafrika tuna matatizo ya akili.Kipimo cha Kiongozi au Rais ni kuwatoa wale anaowaongoza kwenye matatizo, tena kuwatoa haraka.
Sasa basi, toka tumepata uhuru miaka 60 iliyopita tumepata marais wa 5, huyu ni wa sita. Wote hawa tukiwapima kwenye kipimo cha kututoa kwenye matatizo yetu wanapwaya vibaya.
Bado raia sisi ni maskini wa kutupwa, juzi tumeingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambao bado ni umaskini.
Nchi bado utapiamlo ni tatizo kubwa. Tena nasikia kabla ya uhuru tulikuwa ndiyo wauzaji wakubwa wa chakula Africa, kwenye hiki tunerudi nyuma. Elimu bado ni tatizo kubwa, wanaofika sekondari hawafiki hata 30%. Afya , maji na indicator zote za maendeleo nchi yetu bafo ipo nyuma sana.
Ni kweli kuna hatua tumepiga toka uhuru lakini sidhani kama ni sababu ya uongozi bora bali ni natural course ya mambo, si sababu ya uelewa wa viongozi. Baada ya muda kuna hatua mtu utapiga.
Tukiwapima Marais wetu kwenye kazi yao kubwa, kututoa kwenye umaskini, wamefeli vibaya sana. Ima maana toka uhuru hatujawahi pata Rais wa maana?
Maendeleo Ni mchakato. Kuna siku yatatimia kwa kiasi chake hayo unayotoka.
Hatuwezi kujifananisha na Wenzetu ili tuone kama Drc Mali na Burkina?.Hatujafika popote, haya maendeleo ni natural course. Ni kawaida kwa binadamu kupiga hatua baada ya muda fulani.
Tupime kiwango cha Maendeleo na ninaweza kusema tumetoka mbali na Maendeleo yanaonekana japo sio sekta zote
I will marry When I want .haha haa na"The beautful ones are not yet born"
Kwanini tusijipime na Waafrika wenzetu kwanza halafu ndio tuangalie MasharikiUkitika kupima maendeleo yetu tujipime na nchi kama Singapore,Vietnam, Malysia na Korea ya kusini ambazao mwaka 1960 wakati tunapata huru tulikuwa sawa nazo kimaendeleo ndipo utajua jinsi tunapiga tu mark time kwa miaka 60.
Maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi na ubunifu sio kuongea ongea
Hao ndio New Generation Mataga au kwa kifupi NEGEMAHapo ulipo huoni watu waliokuzunguka wanafanya kazi??
Watu walikuwa wanafanya kazi hata kabla baba yako hajatoa mbegu yako ya kuzaliwa.