Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,157
- 10,829
Kipimo cha Kiongozi au Rais ni kuwatoa wale anaowaongoza kwenye matatizo, tena kuwatoa haraka.
Sasa basi, toka tumepata uhuru miaka 60 iliyopita tumepata marais wa 5, huyu ni wa sita. Wote hawa tukiwapima kwenye kipimo cha kututoa kwenye matatizo yetu wanapwaya vibaya.
Bado raia sisi ni maskini wa kutupwa, juzi tumeingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambao bado ni umaskini.
Nchi bado utapiamlo ni tatizo kubwa. Tena nasikia kabla ya uhuru tulikuwa ndiyo wauzaji wakubwa wa chakula Afrika, kwenye hiki tunerudi nyuma. Elimu bado ni tatizo kubwa, wanaofika sekondari hawafiki hata 30%. Afya , maji na indicator zote za maendeleo nchi yetu bafo ipo nyuma sana.
Ni kweli kuna hatua tumepiga toka uhuru lakini sidhani kama ni sababu ya uongozi bora bali ni natural course ya mambo, si sababu ya uelewa wa viongozi. Baada ya muda kuna hatua mtu utapiga.
Tukiwapima Marais wetu kwenye kazi yao kubwa, kututoa kwenye umaskini, wamefeli vibaya sana. Ima maana toka uhuru hatujawahi pata Rais wa maana?
Yaani wewe hata baba yako sidhani kama ni baba sahihi kwako!!!!
kwanini haukuzaliwa na bakhresa au familianya dewji, basi Rostam aziz au Manji
Na unatamani mama yako angekuwa Winnie Mandela au Magreth Thatcher
Unajikana historia na kujidhalilisha, hao babu na bibi zako waliokuleta duniani walikuwa wapi kuchukua hizo nafasi sa urais miaka karibu 70 yote??? au wewe mkimbizi au umezamia nchi??
au umejizaaa na kushtukia uko TZ? kwa nn haukuzaliwa USA?
kesho pia utaona hata mke uliyeoa hana uzuri unaoutaka
una tatizo