Toka tumepata uhuru hadi leo, hatujawahi pata Rais wa maana!

Toka tumepata uhuru hadi leo, hatujawahi pata Rais wa maana!

Hayo mambo mabaya yaliytokea kwa sababu ya Urais wa kifalme na mifumo mengine mibovu inayoruhusu maovu kufanyika bila uwajibikaji.

Ni hivi, bunge letu linaweza kuvunjwa na Rais muda wowote, spika wa bunge anatoka kwenye chama ambacho Rais ni mwenyekiti wake. Spika akiamua kufanya kazi yake sawa sawa ya kukataa jambo la serikali Mwenyekiti wake anaweza kumfukuza uanachama akakoma kuwa spika na pia anaweza kufukuza wabunge wanaompinga wakaondolewa kuwa wabunge(Magu alitaka kufanya hivyo kwa wabunge wa kusini kwenye sakata la korosho)

Majaji wa mahakama wanateuliwa na Rais na hawathibitishwi na bunge kabisa.Kwa nini Rais asiwekwe loyalists wake.Nchi nyingine Rais anateua kisha wanapelekwa bungeni kufanyiwa usaili. Kenya majaji wanafanyiwa usaili na wanateuliwa na Tume ya mahakama Rais anapelekewa listi ambayo anatakiwa achague kati yao.

Sehemu nyingine wakuu wa vyombo vya usalama wanateuliwa na Rais kisha wanafanyiwa usaili na kuthibitishwa na bunge.

Kwingine katiba haziruhusu Mwanasheria mkuu au DPP haruhusiwi kuanzisha mashtaka au kukamata mtu kwa amri ya kisiasa.Hapa.
kwetu Rasi, Mawaziri, wakurugenzi, Ma RC na DC wanaweza kutoa amri ya mtu kukamatwa na kuwekwa ndani na kufungiliwa hata mashtaka yasio na dhamana. Achilia mbali haya masaa 48 ya wakuu wa mikoa na wilaya.

Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanafanya hata kutetea katiba hii ya sasa kuwa haiwezekani.
Hoja yangu ni kwamba mambo mengi mabaya yaliyotokea yalikuwa kinyume na katiba ya sasa hivyo hata ikija hiyo mpya kama watu hawataiheshimu ni kazi bure tu. Kwa Tanzania wakuu wa vyombo vya wanateuliwa na Rais na hii haiwezi kubadilika hata ikija katiba mpya, marekani na ulaya pia wakuu wa hivyo vyombo vya usalama wanateuliwa na wakuu wa nchi ila utofauti wetu na wao ni kwamba wao wanafata sheria na sio mtu hata kama amewateua.
 
Tungekuwa na msingi na kujua tunaelekea wapi, ingefanyika analysis ya kujua chanzo kikubwa cha mapato cha wananchi, baada ya kujua ni 80% kilimo......budget na uwekezaji huko ungekuwa mkubwa kuanzia pembejeo bora, vifaa bora vya kilimo, Vifaa bora na uwekezaji kwenye mbegu bora za mifugo......sasa Nyerere alijenga viwanda, Mkapa akauza.......
Mkapa na mwinyi walikuwa hawan budi kufanya hivyo,maji yalikuwa yamisha wafika shingoni.Matatizo hata yote ya Sera za kiuchumi aliye vurunda ni Nyerere kiburi chake ndicho kilichotuangamiza jamaa alikuwa hana tofauti na Magufuli kwa kiburi na jeuri.

Nyerere aliona kabisa mifumo ya kiuchumi ya Dunia inabadilika lakini kajifanya yeye kajifanya Mungu MTU hashauriki+bora angemsikiliza rafiki yake Kambona hata kidogo tungekuwa mbali.

Nyerere katika kipindi chake aliongoza watu wengi wakiwa wajinga,alikuwa na nafasi ya kuweka mifumo mingi ya kiutawala ,kijamii na kisiasa vizuri lakini hakufanya hivyo.
 
Kikwete ndie Raisi bora sana kwa Maendeleo katika kipindi chake Uchumi hadi wa Mtaani ulipiga hatua kubwa
Kikwete wako hakuwa mzalendo. Alikuwa tayari nchi iuzwe kwa Wachina. Ujambazi mitaani kwake sawa. Maajali ma njia panda, sawa. Mtoto wake kuwa celebrity tajiri, sawa. Ma umeme na ma maji kukatika, sawa ili mradi yeye anapata.

Mahuduma ya afya duni kwake sawa, ili mradi yeye anaenda kufanyiwa surgery ya tezi dume na medical check up John Hopkins Hospital, Maryland, Marekani.

Mameneja wa NMB wanasema ilikuwa ukiona land cruiser la Ikulu limekuja benki ujue limebeba masanduku ya madafu wabadilishiwe wapewe dola na ujue kesho yake JK anaamsha. Kwenda kuomba misaada ya vyandarua, na ume spend kugharamia safari na msafara hela nyingi kuliko thamani ya vyandarua unavyoenda kuomba!

No scrap of patriotism. Uzalendo sifuri. To hell with that man Kikwete.
 
Kipimo cha Kiongozi au Rais ni kuwatoa wale anaowaongoza kwenye matatizo, tena kuwatoa haraka.

Sasa basi, toka tumepata uhuru miaka 60 iliyopita tumepata marais wa 5, huyu ni wa sita. Wote hawa tukiwapima kwenye kipimo cha kututoa kwenye matatizo yetu wanapwaya vibaya.

Bado raia sisi ni maskini wa kutupwa, juzi tumeingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambao bado ni umaskini.

Nchi bado utapiamlo ni tatizo kubwa. Tena nasikia kabla ya uhuru tulikuwa ndiyo wauzaji wakubwa wa chakula Afrika, kwenye hiki tunerudi nyuma. Elimu bado ni tatizo kubwa, wanaofika sekondari hawafiki hata 30%. Afya , maji na indicator zote za maendeleo nchi yetu bafo ipo nyuma sana.

Ni kweli kuna hatua tumepiga toka uhuru lakini sidhani kama ni sababu ya uongozi bora bali ni natural course ya mambo, si sababu ya uelewa wa viongozi. Baada ya muda kuna hatua mtu utapiga.

Tukiwapima Marais wetu kwenye kazi yao kubwa, kututoa kwenye umaskini, wamefeli vibaya sana. Ima maana toka uhuru hatujawahi pata Rais wa maana?
Uko sahihi kabisa, hsa hsa awamu ya tatu, nne na tano ambayo ndio ya ovyo kuwahi kutokea
 
Kabla ya uhuru Uchumi Wa Tanganyika ulikua Unafanana na Korea Kusini.
Ila baada ya Miaka Kupita Tanzania Imeachwa Mbali kiuchumi.
Kifupi Niseme Tu Mtoa mada Unahoja Mzuri Juu ya Hili.
 
Sawa mkuu nilikuwepo tangu enzi za Nyerere nipe fact ya vitu alvyo fanya mwinyi
Kama kweli kabisa ulikuwepo enzi za Nyerere wala huitaji kupewa facts za Mwinyi,

Ushauri: Watafute wazee uwanunulie kahawa na tangawizi kisha waulize habari za kipindi cha Nyerere na Mwinyi,
Hujachelewa.
 
Kwanini tusijipime na Waafrika wenzetu kwanza halafu ndio tuangalie Mashariki
South Africa imepata uhuru juzi tu, tizama maendeleo yao, tena baada ya uhuru maendeleo yameslow down mpaka wanapitwa na Nigeria.... Tatizo uongozi, kweli hatujapata watu wenye akili na maarifa ya kwenda sambamba na speed ya dunia.
 
Kama kweli kabisa ulikuwepo enzi za Nyerere wala huitaji kupewa facts za Mwinyi,

Ushauri: Watafute wazee uwanunulie kahawa na tangawizi kisha waulize habari za kipindi cha Nyerere na Mwinyi,
Hujachelewa.
Achana na maneno ya vijiweni lete fact na twakum mkuu
 
Achana na maneno ya vijiweni lete fact na twakum mkuu
Kuna vitu havihitaji takwim, si wengine wazee wetu wanatuambia kipindi cha nyerere maisha yalikuwa magumu sana, kila kitu hadi ukapange mstari dukani na mnapewa kwa kiasi kinacholingana kutokana na familia yako.
 
Tumeendelea kuweka mwiko wa kuchagua marais kutoka jamii matajiri zenye mwamko wa kiuchumi na zinazojua fedha na bidii ya utafutaji wake ndio tumefika hapa leo. Nyerere alikuwa na mawazo maskini kuliko mtu mwingine yeyote enzi zile, Mwinyi mtu wa kusubiri upepo wa bahari uvume, Kikwete mtu wa kukaa chini ya miembe, Mkapa mtu wa kubangaiza, Magufuli mtu wa kuchunga ng'ombe porini na sasa tumerudi kupunga upepo wa bahari na kusubiri nazi zianguke tuokote. Tujifunze kuchagua watu wenye muamko wa maendeleo, hadi siku hiyo kufika, tuendelee na umaskini wetu!
Kipimo cha Kiongozi au Rais ni kuwatoa wale anaowaongoza kwenye matatizo, tena kuwatoa haraka.

Sasa basi, toka tumepata uhuru miaka 60 iliyopita tumepata marais wa 5, huyu ni wa sita. Wote hawa tukiwapima kwenye kipimo cha kututoa kwenye matatizo yetu wanapwaya vibaya.

Bado raia sisi ni maskini wa kutupwa, juzi tumeingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambao bado ni umaskini.

Nchi bado utapiamlo ni tatizo kubwa. Tena nasikia kabla ya uhuru tulikuwa ndiyo wauzaji wakubwa wa chakula Afrika, kwenye hiki tunerudi nyuma. Elimu bado ni tatizo kubwa, wanaofika sekondari hawafiki hata 30%. Afya , maji na indicator zote za maendeleo nchi yetu bafo ipo nyuma sana.

Ni kweli kuna hatua tumepiga toka uhuru lakini sidhani kama ni sababu ya uongozi bora bali ni natural course ya mambo, si sababu ya uelewa wa viongozi. Baada ya muda kuna hatua mtu utapiga.

Tukiwapima Marais wetu kwenye kazi yao kubwa, kututoa kwenye umaskini, wamefeli vibaya sana. Ima maana toka uhuru hatujawahi pata Rais wa maana?

"The beautful ones are not yet born"

Maendeleo Ni mchakato. Kuna siku yatatimia kwa kiasi chake hayo unayotoka.

Kwa dhana yako hiyo ina maana kwa miaka 30 Chadema haijapata mwenyekiti wa maana kwa sababu hawana maendeleo yoyote hata jengo tu!

Tupime kiwango cha Maendeleo na ninaweza kusema tumetoka mbali na Maendeleo yanaonekana japo sio sekta zote

Hakuna hatua tumepiga Mkuu, ukilinganisha na miaka 60 ya uhuru haya yote yalitakiwa kukamilika ndani ya miaka angalau mitano, waafrika tuna matatizo ya akili.

Hatujafika popote, haya maendeleo ni natural course. Ni kawaida kwa binadamu kupiga hatua baada ya muda fulani.

Tuseme tu ukweli Mwinyi na JK hawakupaswa kuwa ma-Rais wa nchii hii

Maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi na ubunifu sio kuongea ongea

Patema

ni kwanini hawakupaswa kuwa marais?

Basi hii ni taswira halisi ya mtanzania, ukiona hivyo basi taifa halina watu wa maana, ndio maana we're poor.

Upinzani wameturudisha sana nyuma.

Tumechoka na mchakato wa mwendo konokono.Tunataka mchakato wa mwendo wa farasi

Hahahaha ni kweli kabisa alafu hatujapata maendeleo badala yake tumempata Rais mwanamke

Ukitika kupima maendeleo yetu tujipime na nchi kama Singapore,Vietnam, Malysia na Korea ya kusini ambazao mwaka 1960 wakati tunapata huru tulikuwa sawa nazo kimaendeleo ndipo utajua jinsi tunapiga tu mark time kwa miaka 60.
 
Kuna vitu havihitaji takwim, si wengine wazee wetu wanatuambia kipindi cha nyerere maisha yalikuwa magumu sana, kila kitu hadi ukapange mstari dukani na mnapewa kwa kiasi kinacholingana kutokana na familia yako.
Ahsante maana niliona naweza nikabishana kumbe nabishana na mtoto aliyezaliwa mwaka 2000.
 
Maendeleo yanaanzia kwako binafsi, kama huwezo kubadilisha maisha yako hakuna rais atakayekuletea maendeleo.
 
Spiritual afrika imerogwa bora tungewaacha wakoloni tungekuwa mbali sana
 
Back
Top Bottom