Kipimo cha Kiongozi au Rais ni kuwatoa wale anaowaongoza kwenye matatizo, tena kuwatoa haraka.
Sasa basi, toka tumepata uhuru miaka 60 iliyopita tumepata marais wa 5, huyu ni wa sita. Wote hawa tukiwapima kwenye kipimo cha kututoa kwenye matatizo yetu wanapwaya vibaya.
Bado raia sisi ni maskini wa kutupwa, juzi tumeingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambao bado ni umaskini.
Nchi bado utapiamlo ni tatizo kubwa. Tena nasikia kabla ya uhuru tulikuwa ndiyo wauzaji wakubwa wa chakula Africa, kwenye hiki tunerudi nyuma. Elimu bado ni tatizo kubwa, wanaofika sekondari hawafiki hata 30%. Afya , maji na indicator zote za maendeleo nchi yetu bafo ipo nyuma sana.
Ni kweli kuna hatua tumepiga toka uhuru lakini sidhani kama ni sababu ya uongozi bora bali ni natural course ya mambo, si sababu ya uelewa wa viongozi. Baada ya muda kuna hatua mtu utapiga.
Tukiwapima Marais wetu kwenye kazi yao kubwa, kututoa kwenye umaskini, wamefeli vibaya sana. Ima maana toka uhuru hatujawahi pata Rais wa maana?