Kipimo cha Kiongozi au Rais ni kuwatoa wale anaowaongoza kwenye matatizo, tena kuwatoa haraka.
Sasa basi, toka tumepata uhuru miaka 60 iliyopita tumepata marais wa 5, huyu ni wa sita. Wote hawa tukiwapima kwenye kipimo cha kututoa kwenye matatizo yetu wanapwaya vibaya.
Bado raia sisi ni maskini wa kutupwa, juzi tumeingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambao bado ni umaskini.
Nchi bado utapiamlo ni tatizo kubwa. Tena nasikia kabla ya uhuru tulikuwa ndiyo wauzaji wakubwa wa chakula Afrika, kwenye hiki tunerudi nyuma. Elimu bado ni tatizo kubwa, wanaofika sekondari hawafiki hata 30%. Afya , maji na indicator zote za maendeleo nchi yetu bafo ipo nyuma sana.
Ni kweli kuna hatua tumepiga toka uhuru lakini sidhani kama ni sababu ya uongozi bora bali ni natural course ya mambo, si sababu ya uelewa wa viongozi. Baada ya muda kuna hatua mtu utapiga.
Tukiwapima Marais wetu kwenye kazi yao kubwa, kututoa kwenye umaskini, wamefeli vibaya sana. Ima maana toka uhuru hatujawahi pata Rais wa maana?
Maendeleo yanaanzia kwako binafsi, kama huwezo kubadilisha maisha yako hakuna rais atakayekuletea maendeleo.
Changamoto zetu zinafanana
Si mnawachaguaga nyinyi wenyewe! Au mnachaguliwa na watu kutoka nchi nyingine....
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mwendazake mbona amefisadi mengi kuwazidi.Fence ya ukuta wake kijijini unajenga nyumba ngapi au shule ngapi za hao watoto masikini.Sio mimi tu, mamilioni ya Watanzania wanachukia kwa uchungu dalili za kurudi mauza uza ya enzi za JK.
Mazishi ya JPM Kikwete anasimama kusema watoto wake wanamsemesha kwa Kiingereza kwa sababu watoto wa siku hizi wanaenda shule za Kiingereza.
Watoto wangapi nchi hii wanaenda shule za Kiingereza ? Na ni watoto wa nani ?
Unakuwaje Rais mzima hujui kwamba 95% ya watoto wa nchi hii wanaenda shule za kikapuku, hazina vyoo wala vitabu, maskini wachafu hawana viatu, uniform hawana matako nje nje! Wewe JK, nani alikuwa audience yako kwenye msiba wa JPM uliposema watoto wa nchi hii wanaenda shule za Kingereza ? Watoto wa nani ????
Rais umestaafu unamiliki ma apertment building Mikocheni na Msasani Peninsula pamoja na mi mali mingine wewe na Wakuu Wastaafu wa Usalama wa Taifa. Kwa biashara gani zaidi ya undeclared gifts za kupewa na matajiri, rushwa za wazi, grand corruption, wizi wa kijambazi, grand larceny!
Afrika janga tulilonalo hatuna wazalendo.
Mimi nadiliki kusema kuwa kwa mara ya kwanza,selikali ya awamu ya tano ilikuwa na dhamira ya dhati kabisa kutatua matatizo sugu tuliyodumu nayo kwa miaka mingi.Tumechoka na mchakato wa mwendo konokono.Tunataka mchakato wa mwendo wa farasi
Mataga mama yako na baba yakoMawazo ya mataga.
Unazifahamu kwa nini tunachagua viongozi?
Kipimo cha Kiongozi au Rais ni kuwatoa wale anaowaongoza kwenye matatizo, tena kuwatoa haraka.
Sasa basi, toka tumepata uhuru miaka 60 iliyopita tumepata marais wa 5, huyu ni wa sita. Wote hawa tukiwapima kwenye kipimo cha kututoa kwenye matatizo yetu wanapwaya vibaya.
Bado raia sisi ni maskini wa kutupwa, juzi tumeingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambao bado ni umaskini.
Nchi bado utapiamlo ni tatizo kubwa. Tena nasikia kabla ya uhuru tulikuwa ndiyo wauzaji wakubwa wa chakula Afrika, kwenye hiki tunerudi nyuma. Elimu bado ni tatizo kubwa, wanaofika sekondari hawafiki hata 30%. Afya , maji na indicator zote za maendeleo nchi yetu bafo ipo nyuma sana.
Ni kweli kuna hatua tumepiga toka uhuru lakini sidhani kama ni sababu ya uongozi bora bali ni natural course ya mambo, si sababu ya uelewa wa viongozi. Baada ya muda kuna hatua mtu utapiga.
Tukiwapima Marais wetu kwenye kazi yao kubwa, kututoa kwenye umaskini, wamefeli vibaya sana. Ima maana toka uhuru hatujawahi pata Rais wa maana?
Kwahiyo mnaamuaje mkiwa kama raia wanyonge?Wanajiweka wenyewe.Labda tulaumiwe kwa kushindwa kuzuia wao kujiweka wenyewe.