DOKEZO Tokea tarehe 19 Novemba, mgonjwa wangu ndio kwanza kafanyiwa UTRASOUND Muhimbili. Changamoto ni nyingi sana

DOKEZO Tokea tarehe 19 Novemba, mgonjwa wangu ndio kwanza kafanyiwa UTRASOUND Muhimbili. Changamoto ni nyingi sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Pole sana !na inawezekana umesema ukweli kwa manufaa ya wengi.
mimi naamini katika universal health Insurence ambayo itamfanya mteja akifika asidaiwe fedha.
Usikate tamaa kwani unayo hoja ya namna gani haswa Afya ya msingi endelevu itolewe.naamini wataalamu wa afya watafanyia kazi kero yako hii.
Bila shaka sekta ya afya inalo la kujifunza wakati ikijiendeleza kiteknolojia na kuboresha huduma isusahau watanzania bado wana vipato vya chini na hivyo tusije geuka kama wamarekani au waingereza ...huduma bado zinapaswa kuwa za gharama za kadiri.

Zaidi kama wananchi tusisahau dhana ya uchangiaji wa huduma ili ziwe bora na endelevu na sio kwa msaada wa mataifa ya nje
Tuchangie huduma zipi? kununua mashine? Ujinga jinga ujinga, Yaani report ya CAG mwaka huu zimepigwa karibia trilion 1 na waliopiga Mama kawasamehe then unataka sisi raia tuchangie tena huduma?

Huu ujinga unapaswa kukoma kwa Watanzania.

Tukiendelea na uzezeta wa ina hii hakuna rangi tutataacha kuona
 
Mkuu poleni kwa kuuguza. Lakini ukweli ni kwamba viongozi hawaombwi bali wanalazimishwa na wakishindwa wanatimuliwa. Fikiria una mfanyakazi wako uliyemwajiri na unamlipa mshahara halafu eti unampigia magoti afanye kazi. Hili liwe fundisho kwako na siku nyingine jitokeze kuitokomeza CCM iwe ni kwa maandamano au kulinda kura.
hawa ndio wale utasikia sitaki Siasa, anasahau kila kitu ni siasa katika nchi hii,
 
Tuchangie huduma zipi? kununua mashine? Ujinga jinga ujinga, Yaani report ya CAG mwaka huu zimepigwa karibia trilion 1 na waliopiga Mama kawasamehe then unataka sisi raia tuchangie tena huduma?

Huu ujinga unapaswa kukoma kwa Watanzania.

Tukiendelea na uzezeta wa ina hii hakuna rangi tutataacha kuona
usipochangia nani unategemea achangie??
 
Nianze tu kwa kumuomba yyte mwenye uwezo wa kumfikishia Rais Samia hili na amfikishie.

Hali ya Muhimbili inasikitisha. Na mkono wake wahitajika.

Rais Samia chochote atachofanyia Muhimbili atapata baraka tele kutoka kwa MwenyeziMungu.

Nayasema haya kutokana na hali halisi. Mgonjwa kapewa rufaa kutoka mkoani kuja Muhimbili kwa Kesi ya Saratani.

Mgonjwa wa saratani. Fikiria kipimo cha kwanza akaandikiwa apime UTRASOUND. Akaandikiwa tar 19 na akifanye tar 27 nov 2024. (beurocracy). Kipimo cha dkk 15 kaambiwa asubiri hadi tar 27.

Wamethibitisha kuwa mgonjwa ana uvimbe tar 30.

Dr wake kamwandikia afanye uchunguzi zaidi. Hata hivyo kwanza mgonjwa anahitajika kuongezewa damu.

Pamoja na kutimiza masharti yote ya kupatikana kwa damu lkn ni Muhimbili hawana Damu ya kumpa mgonjwa huyu siku ya 10 leo.

Ombi langu kwa rais Samia. Zile pesa za watz anazogawa kwenye matumizi ya anasa, angetumia kuwahamasisha watanzania walau wachangie damu.

Walau hizo pesa zitumike kuwalisha pilau watz wengi watajitikeza kuchangia walau damu.

Kwa ufupi hali ya huduma Muhimbili imezorota au zimekufa kabisa.

Ukilitimba nao uko mwingi kuliko huduma.

Fikiria kipimo ambacho huchukua dakika 15, kwa Muhimbili kinachukua wiki mbili.

Rais umejipa dhima kwa Watanzania basi nakuomba sana onyesha utu kwa wagonjwa walio na rufaa za maisha yao pale muhimbili.

Mgonjwa ana ndugu ambao ni donars. Lakini mgonjwa wao hajapata damu. Nimejaribu kutaka kuwahonga ili tupate damu bado wanasema hawana damu.

Serikali yetu basi shindweni tore lkn musishindwe katika upande wa afya tena katika ngazi ya hospitali kuu ya rufaa Muhimbili.

Hii ni sehemu ndogo sana ya taarifa ya kiuchunguzi pale Muhimbili. Kuna madude mengi na milolongo mingo ya logistics kuliko huduma za matibabu sijayasema.

Niishie hapa kwa sasa
Dah,pole kwa kuuguza mkuu, usemacho nikweli kwa hospital zetu hizi, natamani kesho nije kuchangia damu
 
Back
Top Bottom