Top 10 ya nchi zenye utajiri wa madini Afrika, Tanzania haipo

Kuzalisha na kuwa na hifadhi ya madini nadhani ni vitu viwili tofauti...unaweza ukawa na madini mengi lakini huzalishi vizuri
 
Na wewe kwa akili zako unasemaje? Hayo wanayosema ni kweli????
Can you share hilo jarida?
 
Takwimu kama hizo zinawekwa wazi kisiasa tu, kwa malengo ya yule anayezitangaza. Ni sawa na miaka ile ya tisini katikati takwimu zikasema Nigeria ina watu milioni 150 wakati ukweli ni kuwa hawakufika hata milioni 120 ni lengo fulani la kisiasa ambalo huja kujulikana miaka kadhaa ikiwa imeshapita.
 
Waliowahi kunipa hizi takwimu ni wataalamu waliobobea; siyo wanasiasa na hayupo mtaalamu mwingine yeyote aliye ndani au nje ya nchi yetu anayeweza kuwazidi uelewa wataalamu hawa
 
Waliowahi kunipa hizi takwimu ni wataalamu waliobobea; siyo wanasiasa na hayupo mtaalamu mwingine yeyote aliye ndani au nje ya nchi yetu anayeweza kuwazidi uelewa wataalamu hawa
Tuna utajiri mwingi sana wa madini hapa Tanzania kuliko hizo takwimu. Geologist wa kweli atakwambia juu ya ukweli huo.
 
Uranium mbona ni madini yenye thamani ndogo sana pamoja na kwamba ni mali ghafi ya kutengenezea silaha za nuklia pamoja na uzalishaji wa nishati ya umeme.
 
Tuna utajiri mwingi sana wa madini hapa Tanzania kuliko hizo takwimu. Geologist wa kweli atakwambia juu ya ukweli huo.
Mkuu kwanza aseme kama ni geologist tuanze kushusha hoja za kijiolojoa Kwa nini Tanzania Ina utajiri wa madini, lakini kama sio geologist ngoja tumuache aendelee kuamini alichokisoma kwenye chapisho lake.
 
Shusha nondo mkuu na sisi tufaidike ambao siyo geos, anza na migod mikubwa, kiasi cha madini(reserve) na LOM, kwa kuanzia.
 
list inaongelea natural resources, mleta mada anaongelea madini pekee, wakati kiuhalisia madini ni sehemu tu ya natura resources, sijui naeleweka?
 
Kwa hiyo kama haipo hapo kwenye Listi yako....!

Hitimisho lako ambalo hujaandika ni kwamba tunastahiri kuwa Masikini..!!!
 
Kwa hiyo kama haipo hapo kwenye Listi yako....!

Hitimisho lako ambalo hujaandika ni kwamba tunastahiri kuwa Masikini..!!!
Sisi tutakuwa fukara kabisa.Kama hao wa kwenye top ten ndio wamechoka hivyo vipi sisi ambao hatumo kwenye list
 
Tanzania ni nchi ya kawaida sana hapa Afrika na dunia kwa ujumla ni vile tu Watanzania hatuna desturi ya kufuatilia mambo kwa undani na huu Uzi sababu umekwenda na takwimu unawatoa watu jasho,maana wanapenda zile stories za vijiweni vya kahawa za "unaambiwa,inasemekana"nk"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…