Top 10 ya nchi zenye utajiri wa madini Afrika, Tanzania haipo

Hii ndio source mbalimbali au source Moja? Bwege wewe..

Source yangu ni credible kuliko huu upuuzi wako hapa
 
Usisikilize story za mitaani. Tuulize wataalam wa fani hii tukueleze.

Fahamu:

Dhahabu yote ya Tanzania iliyochimbwa na ambayo haijachimbwa inakadiriwa kuwa ounces milioni 40. Dhahabu iliyochimbwa Witwatersrand Basin (South Africa) pekee ni ounces milioni 305. Dhahabu iliyochimbwa kwenye mgodi mmoja wa dhahabu wa Homestake USA ni ounces milioni 41. Mgodi mmoja wa Super Pit, Kalgoorlie Goldfield (Australia) mpaka sasa umezalisha dhahabu ounces milioni 60, na bado unaendelea.

Tunayo madini lakini siyo mengi kama watu wanavyodanganyana huko mitaani.

Kati ya sababu zinazotolewa kwa nini Tanzania hatuna migodi mingi mikubwa ya dhahabu kwenye greenstone belt yetu, ni kwamba ndani ya greenstone, tuna ratio ndogo sana ya mafics and ultramafics to granitoids, tofauti na greenstone belts nyingine kama zile za America au Australia.
 
Hebu muelewe ni kwamba hizo nchi wazungu au walitoa hizo takwimu wamepata nafasi za kuchunguza ila kwetu ardhi kubwa haijafanyiwa uchunguzi.

Pia wanavigezo lbd kuangalia mauzo ya nchi lkn huku zinapeperushwa nchi nyenginezo na sifa wanapata wao.
Kwani kwetu wazungu hawajakaa au hawapo? Si ndio wanagundua hata gas nk?
 
Kumbe mambo ya kusemekana. Tanzania ina madini ya kawaida sana, hata haina mafuta ya kutisha na kwenye gesi vilevile haipo top 5 ya nchi zenye reserve kubwa ya gesi.
Mambo ya unaambiwa, inasemekana hayajawahi kuwa facts
Wanaleta habari za eti inaaminika 🀣🀣.
Tunataka proven recoverable commercial reserves sio upuuzi upuuzi.
 
Tanzania itakuwa ya 11, napo bado tu siyo tajiri?
 
Mimi nilivyo elewa utajiri wa madini maana yake ni
Nchi zilizo tajilika kupitia madini yaliyomo nchimi mwao
Lakini Kwa Tanzania yetu madini tunayo Kwa wingi lakini Tanzania haijatajirika kupitia madini hayo
Maana yake mnayaiba
 
Wanaleta habari za eti inaaminika 🀣🀣.
Tunataka proven recoverable commercial reserves sio upuuzi upuuzi.
Yeah inatakiwa kuwa hivyo. Sio kuokota vitu hovyo hovyo mtandaoni
 
Na ndio hoja yangu,Tanzania Ina Madini ya ibangaizaji Wala haiwezi kuwepo kwenye list ya Nchi Zenye Madini kamwe..

Tanzania ingekuwa na akili ingekomaa kwenye sekta ya mifugo,Utalii, Transport Logisticas na kilimo ndiko walau tuna comparative and competitive advantage sio kubangaiza huko kwenye Madini ya hapa na pale 😜😜
 
Mimi nilivyo elewa utajiri wa madini maana yake ni
Nchi zilizo tajilika kupitia madini yaliyomo nchimi mwao
Lakini Kwa Tanzania yetu madini tunayo Kwa wingi lakini Tanzania haijatajirika kupitia madini hayo
Maana yake mnayaiba
Sio hivyo Bali wenye reserve kubwa na wanaozalisha Kwa wingi.
 
Source ya list tajwa kwanza. Siikatai list, ila nakataa Tanzania kuwa si miongoni mwa hiyo list. Wabongo fake sana. Tuseme kwa mfano, Tanzanite ipo kwenye nchi gani nyingine?
Tanzanite ni vanadiferous sapphire. Sapphire zisizo na vanadium zipo kwenye mataifa mengi. Hii yenye vanadium ipo Tanzania tu, lakini ni kiasi kidogo sana katika thamani. Na ufahamu kuwa tanzanite ni jiwe la mapambo, ndiyo maana huwezi kusikia kampuni kubwa zinaenda kuchimba tanzanite, ruby, sapphire, tourmaline au amethyst. Hiyo tanzanite huwezi kulinganisha na madini kama cobalt katika thamani, yanayochimbwa DRC. Gemstone inayochimbwa na makampuni makubwa ni diamond tu, hasa kwa sababu hata ile isiyo gem quality bado inatumika, tofauti na gemstones nyingine.
 
Kwa hiyo Msumbiji wanaweza izidi Nigeria au Algeria Gas? Au Angola? Kwanza haipo hata 10 Bora Zenye reserves kubwa licha ya kuwa walau Wana reserves mara 3 ya Tanzania.

Hapa Tanzania haitafika kokote ,55trilion cubic ni peanut hamna kitu hapo ndio maana tunabembeleza investors..

Kwa hiyo acheni porojo za ooh sijui tuna Madini mengi na blaa blaa kibao..

Hizo Nchi kwenye List sio tuu Zina aina Moja Bali aina kadhaa za Madini valuable.
 
Angalao gas, tunayo reserve ya kutosha. Lakini kutokana na sera mbaya za kiuchumi wakati wa awamu ya 5, bahati hiyo tuliipiga mateke. Watafiti na wawekezaji wakubwa wakakimbilia Msumbiji. Huko wakawekeza vilivyo kwenye utafiti na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gas.

Sasa hivi tunahangaika kuwabembeleza warudi.
 
Ndio Zenye Madini hizo nyie wengine ni wababgaizaji..

Pale Zimbabwe Mchina Katia Mgodi wa Til.4 wa Lithium,Tanzania una Mgodi upi wa thamani hiyo Kwa mfano?
Kwani tz lithium hakuna?
Mbona tunayo

Ova
 
Katika hiyo list ni nchi gani Wana tanzanite?
Tanzanite ni germstone isiyo na maana zaidi ya mapambo..Kuna Madini valuable kuliko hiyo Tanzanite

Mwisho na Nchi zingine Zina Madini ambayo hayapatikani kokote Duniani isipokuwa kwenye Nchi zao pekee so usiwe mshamba..

Bora hata chuma Ina maana kuliko hiyo Tanzanite Yako na ndio maana kwenye Madini yanayoingiza pesa za kigeni nyingi ,Tanzanite haipo Bali dhahabu, almasi na makaa ya mawe.
 
Well spoken,kunguru hawatakuelewa.
 
Kwani tz lithium hakuna?
Mbona tunayo

Ova
Uwe unaelewa ,ipo ila Kwa kiwango gani? Ndio point ya msingi.

Kama mnayo leta investor wa Til.4 kama Zimbabwe hapa πŸ‘‡
 
Saizi ndio kina Makamba wanawabembekeza equinox 😁😁

Advantage nyingine ya gas ya Mtwara iko.jirani na Msumbiji so kikinuka kile uzalishaji unaweza endelea hapa Tanzania.
 
Bongo yenyewe sahv lithium washaanza mdgmdg kufanyia kazi wadau

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…