Top 10 ya nchi zenye utajiri wa madini Afrika, Tanzania haipo

Top 10 ya nchi zenye utajiri wa madini Afrika, Tanzania haipo

Anaemua Cha kufanya ni mwekezaji wewe uamue una mtaji? Una Teknolojia? Una soko? Subiria Cha kupewa.
Usitake tuanze mjadala mwingine juu ya hili, huku ukijua pamoja na kwamba hatuna mtaji lakini bado tunayo sauti kama nchi.
Mwalimu Nyerere aliamua kuyaacha madini haya ardhini, akiwa na matumaini ya kwamba hawa watu waliopo sasa wangekuwa na akili za kutosha kuyafanya madini haya yawe yenye faida kwenye taifa.
Kwa bahati mbaya sana, matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona sasa.

Lakini hebu sasa nikuulize, maanake naona unajifanya kusahau: Hivi kwa hiyo hata hizo nchi nyingine zilizo orodheshwa hapo, kumbe hawafaidiki na hayo madini yao?
 
Eti aliyaacha,baada ya kuyaacha tumefaidikaje? Kwani wewe unaogopa mjadala?
 
Kama wangeangalia mafuta pekee , kwenye list ungeikuta Equatorial Guinea.
E.Guinea wanayo mafuta kiasi gani?
Usije ukachanganya na mambo mengine ambayo hayakuhusika katika kuitengeneza hiyo orodha.

Egypt hawana madini mengine mbali ya gesi, pengine na vifuta kidogo. Algeria hivyo hivyo.
Hata Nigeria ni mafuta na gesi, hakuna madini mengine
Libya ni mafuta.
 
Mbumbumbu hao,Russia ndio namba 1 Duniani,Kuna Ukraine,Mongolia huko Kuna Madini ya Kila aina.
Watu exposure hawana, hii nchi uswahili unaiharibu unakuta muuza mifagio anakomaa eti JWTZ inaongoza ya kwanza jeshi la ardhini Afrika, unajiuliza hivi huyu anayajua majeshi ya Egypt, South Africa na Morocco.

Utawasikia wanaitaja Tanzanite kwamba inapatikana kwetu pekee hivyo ilitosha kututajirisha, Tanzanite ina maajabu gani kwenye soko la dunia. Na kiwango tunachochimba sio kwa wingi kivile. Facts hawataki
 
Eti aliyaacha,baada ya kuyaacha tumefaidikaje? Kwani wewe unaogopa mjadala?
Mimi siogopi mjadala, naogopa muda.

Mfano mzuri ni majadiliano kuelekea kuwa kama unavyoyapeleka sasa hivi na mfano wa mstari mmoja hapo juu.

Sina muda wa kufanya mjadala wa aina hiyo.
 
Watu exposure hawana, hii nchi uswahili unaiharibu unakuta muuza mifagio anakomaa eti JWTZ inaongoza ya kwanza jeshi la ardhini Afrika, unajiuliza hivi huyu anayajua majeshi ya Egypt, South Africa na Morocco.

Utawasikia wanaitaja Tanzanite kwamba inapatikana kwetu pekee hivyo ilitosha kututajirisha, Tanzanite ina maajabu gani kwenye soko la dunia. Na kiwango tunachochimba sio kwa wingi kivile. Facts hawataki
Dah!

Umenifanya nicheke mkuu!

Watu wa aina hiyo tunao wengi sana humu JF, siyo wauza mifagio tu huko mitaani.
 
Madini yapi mliyonayo Kwa wingi yaliyohifadhiwa kushinda hizo Nchi kwenye list ? Taja hayo madini na leta data maana nyie ndio mumemeza mambo ambayo hama uhakika nayo.
Acha ushabiki. Nawe toa data za hizo nchi, Make zimetajwa tu mbona waliotaja hukuwauliza watoe data au kuwauliza ni madini wataje hayo madini? Unashabikia tu. Hujui lugha wamesema nchi zinazozalisha madini kwa wingi! Kwa kukusaidia nenda Wizara ya madini watakupa data.
 
Congo Ina Madini ila sio kuzizidi hizo Nchi tajwa..

Algeria ndio Ina gas asilia nyingi kushinda Nchi zote hapa Afrika na inafanya utaratibu wa kulisha Ulaya, yaani Iko top 10 ya Dunia.

Sasa Congo itaisidi nini Nigeria? Copper na Cobalt au?
Kwa taarifa congo inamadini balaa Tanzania hata robo hatuwafikii
 
Kingereza kigumu sana.

Hiyo ni orodha ya nchi zinazotoa madini.

Siyo zenye hifadhi kubwa ya utajiri wa madini.
 
Mkuu'ChoiceVariable', Eti unasema...?
Gesi ya Msumbiji? Algeria au Egypt wana kiasi hicho cha gesi? Hebu tafuta takwimu ulinganishe.
Egypt wana madini gani mengine, unajua? Libya wana nini zaidi ya mafuta?

Madini ya Ghana, unajuwa ni nini? Mafuta kidogo sana, dhahabu, basi,...nini kingine unajua?

Hiyo 55 tuliyonayo, tungekuwa ni watu tunaojitambua (hapana niseme, tungekuwa na viongozi wanaojuwa na wakawa na uchungu juu ya nchi yetu hii, zingeifikisha mbali sana Tanzania kwa wingi wetu huu tulio nao.

Hata haya ma-'graphite' yanayozolewa watu wakati huu kama takataka bila ya sisi kujua kitu kuhusu umhimu wake, na ile Helium, au ulishasahu kwamba tunayo helium ya kutosha kabisa, ambayo sasa duniani ni ya mhimu kipekee; yote haya, kama viongozi wetu wangekuwa ni watu wenye akili, tusingekosa kuwemo kwenye orodha ile.

Ile gesi ile, kwa kuanzia tungetengeneza mbolea. Soko la mbolea Afirca pekee ingetosha kabisa kutupa manufaa.
Eti Libya wana nini zaidi ya mafuta. Iko hivi, wakati wa Ghaddafi Libya ilikuwa inazalisha zaidi ya mapipa milioni 1 kwa siku, wakati huo ina watu milioni 6 tu. Kwahiyo pipa moja kwa siku linagawanywa kwa watu sita. Ikitokea mgawanya wa keki ya taifa ni sawa kwa bei ya wastani kabisa ya $80 per barrel unakuta watu sita wanagawana kama 200,000 ya kibongo kwa siku. Ndio maana kila kitu kikawa bure, population ndogo na mafuta mengi.

Hapo nimetaja mafuta tu ya Libya, sitajata source nyingine ya fedha ambazo sio kubwa hata hivyo. Unataka uilinganishe na hii nchi tunayoambiwa tufyatuane tuko zaidi ya 61M. Unaona mapipa milioni 1 kila siku ni kidogo mpaka useme "wana nini zaidi ya mafuta".

Vitu vingi tunaenda kwa mihemko. Lawama kwa wanasiasa na sisi wote ziendane na ukweli na uhalisia. Madini tunayo, ila ni level za kawaida kwa Afrika. Hakuna mtu yuko Mali, Libya, Guinea utamtaka ataje nchi zinazoongoza kwa madini aitaje Tanzania. Ni kujikweza kwetu bure
 
Mkuu T14 Armata, umeghafilika, ukanirukia bure bila kujuwa nilichoandika hapo nikimjibu huyo niliyemjibu.

Sikuhoji wingi wa mafuta ya Libya, nilichohoji ni aina mbalimbali za madini yanayozalishwa na Libya mbali ya mafuta..

Baada ya kuyasema hayo, basi chukuwa mfano huo wa Libya wa kugawana mapipa kwa wananchi wake; sasa upeleke Equatorial Guinea, hata kama hawana wingi wa mafuta kama yale ya Libya, lakini wanao wananchi wachache zaidi.

Kwa hiyo, inawezekana pakawepo na vigezo vingine vya ziada vilivyotumika kwenye orodha hiyo iliyowekwa hapo. Mimi sijui; lakini kwa mantiki uliyotumia hapa, pamoja na kwamba haikuwa hoja niliyoitetea, nadhani utaona kwamba kuna upungufu fulani, hata katika hayo uliyoweka hapa.
 
Watanzania wamekuwa wakidanganywa sana na Wanasiasa wakiwemo Chadema, Mwendazake nk kwamba Nchi yetu ni tajiri sana hapa Afrika ingawa kiuhalisia sio Kweli.. Mbona kweli list hapa ya utajiri haipo?

Kwa mujibu wa jarida la economist intelligence Nchi 10 Zenye Utajiri wa Madini hapa Afrika ni zifuatazo

1.South Africa
2.Nigeria,
3.Algeria,
4.Angola,
5.Libya,
6.Egypt,
7.Ghana,
8.DR Congo,
9.Gabon,
10.Zimbabwe.

Sasa kama Tanzania hatumo kwenye hiyo list utajiri ambao huimbwa na Wanasiasa ni upi?
Maana hata kama ni Ardhi nzuri ya Kilimo hatuwezi ifikia South Sudan, Angola, Zambia, DR Congo nk.

Hivi utajiri wa Tanzania hasa ni upi? Au tafsiri ya Utajiri inayosungumzwa ni ipi hasa?

Je! Huenda ingekuwepo kama list inge taja nchi 11, au 12,au 13, 24,etc
Kwa maoni yako mpaka ziwe 10 ndiyo nchi itakuwa tajiri! Je, kama wangetaja nchi 4 tu, Libya, Zimbabwe etc, zisingekuwa tajiri? Au wakisema Tanzania ni masikini ya mwisho! Unapata nini au kupungukiwa nini?
 
Jamani Wana JF, naomba tuwe makini na lugha ya King Charles, inaposemwa " top 10 mineral producing countries in AFRICA, siyo nchi zilizo na utajiri MKUBWA Africa, la hasha, Ina maana ni wazalishaji wakubwa, basi!
Unaweza ukawa na wingi wa madini lukuki, lakini ukazalisha kidogo kabisa, ama usizalishe kabisa. Hapo huwezi kuhesabiwa kuwa uu miongoni mwa wale wasiokuwa na madini.
Hebu akina Mshana Jr mukuje huku, hawa madogo wa memkwa wanatuharibia sana siku hizi. Pia nimeambiwa kuwa kuna ma - professor wa majalalani na ma Dr. wa mchongo.
Hii imekaaje?
Karibuni kwa hoja
 
Karibuni kwa hojaL
 
Watanzania wamekuwa wakidanganywa sana na Wanasiasa wakiwemo Chadema, Mwendazake nk kwamba Nchi yetu ni tajiri sana hapa Afrika ingawa kiuhalisia sio Kweli.. Mbona kweli list hapa ya utajiri haipo?

Kwa mujibu wa jarida la economist intelligence Nchi 10 Zenye Utajiri wa Madini hapa Afrika ni zifuatazo

1.South Africa
2.Nigeria,
3.Algeria,
4.Angola,
5.Libya,
6.Egypt,
7.Ghana,
8.DR Congo,
9.Gabon,
10.Zimbabwe.

Sasa kama Tanzania hatumo kwenye hiyo list utajiri ambao huimbwa na Wanasiasa ni upi?
Maana hata kama ni Ardhi nzuri ya Kilimo hatuwezi ifikia South Sudan, Angola, Zambia, DR Congo nk.

Hivi utajiri wa Tanzania hasa ni upi? Au tafsiri ya Utajiri inayosungumzwa ni ipi hasa?

We unaamini kila list ya vitu mtandaoni ni sahihi? Tafuta vyanzo sahihi vya taarifa mkuu achana na upuuzi
 
Ifike mahali tuache ubishi usiokuwa na tija na tujifunze vitu hivi vitatu yaani learn, unlearn & Re-learn.
Tatizo lako mtoa mada hautaki ku-unlearn hili uweze ku-relearn tena.

Ukiuchukila kama mfano hakika utaelewa na sio ubishi usiokuwa na tija.
Sote ni wakulima Mimi ambaye ni "No One" na wewe ambaye ni "ChoiceVariable" . Mimi nikalima heka 2000 za mahindi na kupata magunia 10,000 ya mahindi nikahifadhi kwenye ghala la mazao, nakupeleka sokoni gunia 500 hizo zilibakia 9500 zikaendelea kubaki kwenye ghala maybe nasubiri bei ya mazao ipande zaidi au ntauza msimu mwingine wa chakula.

Wewe Mr.Choice ukalima hekta 1000 na kupata gunia 5000 na zote ukazipeleka sokoni.
Kimahesabu wewe Mr.Choice utaonekana umezalisha(produce) sana kuliko mimi kwa sababu ya kupeleka gunia zote 5000 kwenye market. Huku mimi Mr. No One nikipeleka gunia zangu 500 sokoni kati ya 10,000 na kubakiwa na 9,500 kwenye Reserve yangu (Ghala).

Interms of production utakuwa umenizidi kwa kuzalisha gunia 5000 na kuuza zote 5000.
Interms of Reserve ntakuwa nimekuzidi kwa mimi kuwa na magunia 9500 ya mahindi kwenye ghala langu na kuuza magunia 500 tu.​
 
Hizi list za watafiti uchwara zipo nyingi sana mtandaoni. Ukweli hapo ni mmoja tu kwamba Nigeria ndo inaongoza. Haiwezekani DRC iwe namba 8 wakati 70% ya Coltan duniani inatoka huko. Hiyo list uchwara. Lakini ukweli mchungu ni kwamba watanzania wasijidanganye kwamba wana madini mengi sana kama wanasiasa na wanaharakati wanavyotuaminisha. Upekee wa Tanzania ni kuwa na Tanzanite ambayo inachimbwa hapa tu.
 
Sasa kama ulimwengu unajua tanzanite inatoka Kenya unategemea nini? Ni uzembe wetu kuruhusu Wakenya watuzidi akili.
 
Tanzania is the 4th largest gold producer in Africa after South Africa, Ghana and Mali and is the world's sole producer of the precious stone Tanzanite. Gold production currently stands at roughly 40 tonnes a year, copper at 2980 tonnes, silver at 10 tonnes and diamond at 112,670 carats.
🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃
 
Watanzania wamekuwa wakidanganywa sana na Wanasiasa wakiwemo Chadema, Mwendazake nk kwamba Nchi yetu ni tajiri sana hapa Afrika ingawa kiuhalisia sio Kweli.. Mbona kweli list hapa ya utajiri haipo?

Kwa mujibu wa jarida la economist intelligence Nchi 10 Zenye Utajiri wa Madini hapa Afrika ni zifuatazo

1.South Africa
2.Nigeria,
3.Algeria,
4.Angola,
5.Libya,
6.Egypt,
7.Ghana,
8.DR Congo,
9.Gabon,
10.Zimbabwe.

Sasa kama Tanzania hatumo kwenye hiyo list utajiri ambao huimbwa na Wanasiasa ni upi?
Maana hata kama ni Ardhi nzuri ya Kilimo hatuwezi ifikia South Sudan, Angola, Zambia, DR Congo nk.

Hivi utajiri wa Tanzania hasa ni upi? Au tafsiri ya Utajiri inayosungumzwa ni ipi hasa?

Attachment ako nazungumzima most producing na sio zenye deposit/uwepo mwingi wa maini.
 
Back
Top Bottom