Kwanza nataka mjue kuwa kuna tofauti kubwa kati ya hiphop na rap. Ukiwasikiliza hawa wasanii unaweza kudhani wanafanya mziki wa aina moja.
Wanaofanya real hiphop ni Roma Mkatoliki na Stamina. Hao kina fid Q na Jay wao wanafanya Rap. Unajua mara nyingi hip hop inagusa maisha halisi ya mtu. Mara nyingi huwezi kukuta hiphop ipo kwenye mashwala ya mapenzi.
Kwa bongo hiphop ipo Arusha na morogoro. Ingawa kwa dsm wapo wachache wanaojaribu kufanya hiphop ingawa wakati mwingine wanatoka kwenye mstari.
Kwangu wanaofanya hiphop ni
1. Stamina
2. Roma Mkatoliki
3. Afande Sele
4. Ney wa Mitgo ingawa huyu anatoka nje ya mstari.
5. Kala jere100.
6. Madee
Wanaofanya rap wapo kibao.
1. Jay
2. Fid Q
3. Nikki Mbishi
4. Jay moo
Na wengine wa aina hiyo.