Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Mkuu umenena kitu chema-elimu ndio kila kitu uwekezaji mkubwa unafanywa na makampuni ya nje sababu hatuna technology hata leo hii tukisema tuvinje mikataba tunaweza but tuna technology ya kuendeleza hayo makampuni jibu ni hapana.Na tukumbuke hizo mbinu ni za karne iliyopita.. Now day's technology imekuwa... Na bahati mbaya sisi ni tegemezi wa kila kitu haswa technology..
We jiulize kama waliweza mdukua chancellor wa ujerumani vip kuhusu sisi ambao hata furniture za maofisini kwa ulimbukeni wetu tuna import..
Yaani kwa kifupi ni labda tuanze kujitegemea technologically..
Pili,utawezaje kuwa mgunduzi na mbunifu wa mambo kama unatumia lugha ya mtu mwingine kujifunza??? Hapa napo jibu ni hapana huwezi , nchi zinazoongoza kwa technologia zinatumia lugha zao.haya mambo yalisetiwa toka enzi hizo ku undo kunahitaji kuwa na mtawala mwenye upeo mkubwa sana,the only solution tunachoweza kufanya ni kuwa kama china ku import technology kwa kusomesha watu kisha kurudi na kuwatengezea mazingira na hii ni long run solution.
Tunagandamizwa kwa kupitia Mult national corporations na kuondoka kwenye mikataba huu sio CCM wala CDM wanaweza bali apatikane mtawala mwenye maono tofauti kabisa