Top Secret: Nyaraka Namba 12333 kutoka Whitehouse

Top Secret: Nyaraka Namba 12333 kutoka Whitehouse

Status
Not open for further replies.
Kuandika kwenyewe tu hujui ndio sembuse kufafuta pesa? Fala kabisa msivamie majukwaa yanayowazidi kimo.

Hivi common sense tu huoni kama mi upumbavu wa kiwango cha PHD kuquote thread ndefu kama hii?
 
Naam,nimemaliza sasa kuisoma makala hii ya aina yake.

SWALI
Nimeona mwisho wa makala hii Waingereza walishinda 'vita' dhidi ya Mohammad Mosaddegh ambaye alikuwa kawabana mbavu katika dili la mafuta.
Na kiongozi aliyefuata alikuwa kibaraka wao aliyekuwa anafuata kila wamuambialo.
Je,Iran waliweza vipi kujikwamua kutoka katika utumwa huu dhidi ya Uingereza?
Ni nani aliyeongoza mapambano hayo ya kurejesha visima vyao vya mafuta?
Je alitumia mbinu gani?

Swali zuri sana mama, ingawa jibu lake nahisi linastahili niandike uzi mwingine but ngoja nigusie walau kidogo naona pia The Boss, Adharusi na gwijimimi wameshauri ningegusia hilo pia..

Kwanza ni muhimu kufahamu baada ya Mosaddegh kuondolewa madarakani na Shah kurudishiwa mamlaka yake na Marekani kuanza kuhusika na uchimbaji wa mafuta Iran ikaanza kupata maendeleo ya kasi mno.

Huduma za kijamii zikaboreka sana na vipato vya wananchi vikakua maradufu.

Lakini Shah Mohammad Reza Pahlavi alifanya makosa haya makubwa;

1. Alikataa kuifanya Iran kuwa nchi ya Kiislamu tofauti na matamanio ya wananchi wengi.
Badala yake Shah Pahlavi akawa anaifanya Iran kuwa ya nchi ya kimagharibi zaidi kiutamaduni.

2. Aliishi maisha ya kifahari kupitiliza kiasi wananchi wakaanza kukwazika.

3. Akaingia kwenye mgogoro na Marekani kwa 'kusapoti' mkataba wa nchi za OPEC kuhusu kuongeza bei ya mafuta.

Makosa haya yakazaa yafuatayo;

=> likaanza vugu vugu la kiislamu la kudai Iran kuwa Jamuhuri ya kiislamu na kupinga umagharibi ndani ya Iran.
Vugu vugu hili liliongozwa na waislamu wa madhehebu ya Shia chini ya kiongozi wao Ayatollah Khomeini.

=> Marekani wakatangaza kuwa hawatakuwa bega kwa bega wala kuwauzia silaha nchi zisizo heshimu haki za binadamu.

=> Baada ya wapinzani wa kisiasa wa Shah kugundua uhusiano wa Shah na marekani umedorora nao wakaanzisha vugu vugu la kupinga Iran kutawaliwa na koo moja (Dynasty).

Baada ya mambo hayo kutokea, Shah Pahlavi akishikwa na kitete na kufanya makosa zaidi;

Mfano;

- akaamuru Ayatollah Khomeini akamatwe. Hii ikamlazimu Ayatollah khomeini kukimbia Iran na kwenda kuishi uhamishoni nchini Uingereza.

- Shah akasimamia kuuwawa kwa sumu kwa Mostafa Khomeini, mtoto mkubwa wa kiume wa Ayatollah Khomeini.

- Shah akasimamia pia kuuwawa kwa sumu kwa moja wa wanafalsafa nguli wa nchi hiyo aliyeitwa Ali Shariat ambaye kwa kipindi hicho alikuwa anaandika makala za kufikirisha mno lakini zikimpinga Shah na mawaziri wake.

- Shah akaamuri kuwekwa vizuizini na gerezani kwa wanasiasa wengi wa upinzani.

- Pia Shah akaanzisha mkakati wa kipumbavu kabisa, ambapo kupitia magazeti ya nchi hiyo zikawa zinaandikwa makala za kumkashifu Ayatollah Khomeini kuwa ni kibaraka wa Uingereza anayetumiwa kuivuruga Iran. Hii iliwaudhi wananchi wake ambao walikuwa wanamuheshimu sana Ayatollah na pia liliwaudhi mabwana wakubwa nchi za magharibi kwa kupewa tuhuma mbaya namna hiyo.



Mambo haya yote yakaifanya Iran kuwa katika 'tension' kubwa. Na hatimae mwaka 1977 waislamu wote wa madhehebu Shia nchi nzima wakaanzisha maandamano ya kupinga Shah Pahlavi na uongozi wake.

Mwishoni mwa mwaka huo pia kukatokea mdodororo wa kiuchumi na mfumuko wa bei kutokana na nchi za magharibi kugoma kununua mafuta ya Iran kutokana na kutoridhishwa na muonendo wa uongozi wa Shah Pahlavi.

Hii ikasababisha wafanyakazi wote kugoma nchi nzima na kuingia mitaani kuungana na wananchi wengine kumpinga Shah na uongozi wake.

Maandamano haya yalikuwa ni yale "maandamano yasiyo na kikomo" na yalifanyika nchi nzima.

Shughuli za kiuchumi zote zikasimama. Wananchi wote wako mitaani wanaandamana.
Shah Pahlavi alishindwa kulihusisha jeshi kwasababu alijua fika ingembidi kuuwa wananchi wote na ni wazi kama angeliamuru jeshi kufanya hivyo wangemgeuzia kibao na kumkataa.

Kwahiyo suluhisho aliloliona, mwezi Febeuary 1979 akaondoka kwa siri nchini Iran na kwenda uhamishoni.

Baadae mwezi machi Jeshi likatangaza kutokumuunga mkono Shah.

Taarifa za jeshi kuunga mkono juhudi za wananchi na kwamba Shah Pahlavi amekimbia Iran zikamfikia Ayatollah Khomeini aliyeko uhamishoni Uingereza.

Kwahiyo, mwezi April 1979 Ayatollah Khomeini akarejea Iran na kuchukua Uongozi wa nchi na kuitangaza Iran kuwa ni Jamuhuri ya Kiislamu na yeye Ayatollah akiwa kama "Supreme leader".


Huu ndio ukawa mwanzo wa historia ya Iran hii ya sasa tuliyonayo.

Nikipata wasaa huko mbeleni nitaweka Uzi kueleza kwa kina kuhusu Iran hii ya sasa ilivyanza.
 
The bold shukrani kwa mara nyingine tena.
Nitarudi kusoma vizuri usiku nikiwa nimetulia, maana mada zako ukiwa unasoma huku unafanya kazi, unaweza kuharibu kabisa.
 
Ktk kitu nilichokiona ni kwamba huu unyonyaji Wa kutumia nguvu Wa haya mataifa makubwa hautoisha kamwe. Haya mambo yataendelea siku zote Na kila nchi masikini zinalia Kwa hii mikataba mibovu ya kinyonyaji Na kandamizi
 
Mkuu uko vizuri sanaaa
Kama kawaida yenu, ningeshangaa kamamngekosekana watu wa sampuli hii.
Siku nyingine ukiona mada ndefu namna hii, we andika maoni yako tu, tutaelewa.
Sio una qoute uzi mzima halafu unaishia kuandika kama ulichoandika hapo juu, unatuumiza wenye simu.
 
Unakumbuka Wikileaks ilichokisema kuhusu Tanzania na watu kununuliwa suti?

Kuna kila dalili kuwa hata Tanzania tumepakatwa na hii Mibaba ya CIA. Kama nyumbu vile. Wanatuswaga kama wanataka kutupeleka Kenya kwa miezi 3 kwenda kujifungulia Maasai Mara.

Anachokifa sasa hivi Rais Magufuli (hata kama baadhi hukubaliani navyo) ni kujaribu kutuondoa kwenye magoti ya hao Mibaba na walau tukae chini ya miguu yao. Unajua ukipakatwa maana yake huwezi hata kufurukuta au kujikuna. Enzi zetu tulisema umebanwa kwenye Angle Theta.

Mikataba ya madini yote ni siri.

_63300937_11_tanzania_reuters.jpg
Mkuu umeongea point za msingi sana..
Ila hiyo Picha uliyoambatanisha mwishoni imenivunja mbavu [emoji23] [emoji23] [emoji23]

"Shah"
 
Mkuu haya majibu unayotoa ungekuwa unayapandisha pale juu, wengine sisi tunasoma page to page, neno kwa neno, mstari kwa mstari tena narudi mara mbili mbili The bold
 
Mkuu umeongea point za msingi sana..
Ila hiyo Picha uliyoambatanisha mwishoni imenivunja mbavu [emoji23] [emoji23] [emoji23]

"Shah"
Hujacheka kunizidi mimi love...
'Shah' wetu katulia hana habari.
Chezea raha za kigari cha farasi wewe?
Namna hii tutaendelea kunyonywa zaidi ya miaka 100 ijayo.
 
The bold Hivi Nchi kama Marekani ikiamua kuvujisha siri za matukio ya fitna na ubadhilifu kama hayo, haioni kwamba itajipunguzia Amani na ushirikiano kutoka nchi iliyotendewa kitendo hiko? Au haiogopi wala kugofia kuwekewa chuki ??
Imagine mtu anakwambia ''ndugu yako aliyekufa miaka 5 iliyopita Mimi ndo niliyemuua''
UTAMCHUKULIAJE HUYO MTU?,
mi nadhani Marekani haikupaswa kuweka mfumo wa kuvujisha siri zao za kiintelijensia hasahasa maovu waliyowatendea magaifa mengine.

mkuu sidhan kama wanavujisha wao bali kuna watu wanachoka na hzo mission then wanaandika vitabu au wanakua wistle blower tu
Wakuu, marekani ina sheria ihusuyo Uhuru wa Wananchi kupata taarifa kuhusu masuala ya serikali yao (Freedom of Information Act).

Sheria hii inaamuru "Excutive Branch" ya Marekani "kushare" na wananchi yake masuala ya siri yanayofanywa na idara za "executive branch" (serikali na rais)

Hapa tunaongelea Idara kama CIA, FBI, DOD, the Army, etc.

Lakini pia sheria hii inatoa ruhusa kwa masuala yanayoweza 'kucompromise' Usalama wa Taifa au trade secrets au foreign policy yaendelee kubaki kuwa siri. Lakini kwa masuala ambayo haya compromise vitu hivi vitatu inaamuliwa na sheria kuwa lazima serikali waweke wazi kwa wananchi.
 
Somo ninalopata kwa post yako bold ni kwamba walichowafanyia waarabu na hawa waingereza ni hicho hicho wanatufanyia sisi waafrika na tz kwa ujumla,
tofauti moja ni kwamba viongozi wetu hazihitajiki nguvu kubwa kuwalaghai wanaelekea kibla kwa sound ndogo na vijisent
 
Nilichogundua viongozi wa Africa hawawezi kujifanya wababe mbele ya Marekani, Uingereza na Russia, jamaa wana kila mbinu ya kuwaondoa madarakani. Kwa hizo akili daaah
 
Sasa nimeanza kuelewa! tuwe makini na CIA na vikundi vingine vinavyofanana hivyo! hawa wanaweza kuangusha serikali yetu!
 
Kuandika kwenyewe tu hujui ndio sembuse kufafuta pesa? Fala kabisa msivamie majukwaa yanayowazidi kimo.

Hivi common sense tu huoni kama mi upumbavu wa kiwango cha PHD kuquote thread ndefu kama hii?
...HII ITAKUWA NI AINA YA JUU KABISA YA UPUMBAVU....
 
Sasa nimeanza kuelewa! tuwe makini na CIA na vikundi vingine vinavyofanana hivyo! hawa wanaweza kuangusha serikali yetu!
Unaweza kuishi duniani hadi unakufa na miaka yako 100 usijekujua hata sura moja ya CIA, wakitaka kukudhuru wanaweza hata kumtumia mkeo au mwanao na akawa ndo CIA.
 
Kwenye app hakuna option ya kufollow! Fungua JF kwa kutumia browser then ingia kwenye profile yangu utaona option ya kufollow.. Bonyeza hapo then rudi endelea kutumia app

Ahsante sana chifu, pia pamoja na kifuatilia naomba nipe mwangaza jinsi ya kupata hizi lishe unazozimwaga hapa nizisome zaidi..

Haya mambo nayafurahia sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom