Top Secret: Nyaraka Namba 12333 kutoka Whitehouse

Top Secret: Nyaraka Namba 12333 kutoka Whitehouse

Status
Not open for further replies.
The bold nimeona ktk mada yako kua vijana waliochaguliwa ktk hiyo oparesheni walikua 100 hivi wakawa chini ya SAG sasa wazungu Na waarabu hawafanani..... Je ilibidi wachaguliwe askari wenye nasaba za kiarabu ili kujiunga Na SAG then ndio wakaingia Iran kufanya hizo harakati Kwa ajili ya kuhamasisha RAIA Wa kiiran? Au hao SAG wazungu walienda Iran wakachagua wairan Na kuwatrain?
 
Mkuu umeongea point za msingi sana..
Ila hiyo Picha uliyoambatanisha mwishoni imenivunja mbavu [emoji23] [emoji23] [emoji23]

"Shah"
Unajua kuna siku nilikaa najiuliza kama Taifa Marekani kupiga vita ukoloni na kuunga mkono juhudi za Waafrika kujikomboa kutoka kwa Wakoloni kwenye ile miaka ya sitini.Kumbe walikuwa wametuandalia ukoloni mwingine ambao ni mbaya sana.
 
Nimeikubali aiseee!!!!
Niliisoma sana ile ya kuuawa kwa Guevara Bolivia na hata Rodriguz ninazo picha zake ndie aliongoza wale Red Barret ambao ndio walimkata Guevara msituni na ndie mtu wa mwisho kuongea na Guevara kumwambia kuwa imeamuliwa uuawe na kumwambia ampe ukumbe wwte wa kumpelekea Fidel ambapo Gievara alimwambie amwambie Fidel atunze wanangu!!!!
Ni interesting kujua hawa watu jinsi wanavyoendesha mambo yao ya kihuni na kihayawani!!!!!
 
Muhimu Sana: Tafadhali usiquote Uzi wote kuepusha usumbufu kwa wanaotumia simu

Unaweza tu kunimention kwa kuandika @ The bold katika comment yako nitaiona..
Tuzingatie hilo tafadhali..
Na mimi uwe unanitag mkuu. Threads kama hizi ndizo zilinifanya niwe member wa kudumu JF sepecially jukwaa hili.
 
Wazungu si watu wajinga mpaka ifikie kipindi wanareveal missions walizozifanya kipindi cha nyuma zilizofanikiwa na ambazo hazikufanikiwa. Ila wanazitoa zile ambazo wanajua hazitasababisha madhala nyumbani kwao na kimataifa
 
Wakuu, marekani ina sheria ihusuyo Uhuru wa Wananchi kupata taarifa kuhusu masuala ya serikali yao (Freedom of Information Act).

Sheria hii inaamuru "Excutive Branch" ya Marekani "kushare" na wananchi yake masuala ya siri yanayofanywa na idara za "executive branch" (serikali na rais)

Hapa tunaongelea Idara kama CIA, FBI, DOD, the Army, etc.

Lakini pia sheria hii inatoa ruhusa kwa masuala yanayoweza 'kucompromise' Usalama wa Taifa au trade secrets au foreign policy yaendelee kubaki kuwa siri. Lakini kwa masuala ambayo haya compromise vitu hivi vitatu inaamuliwa na sheria kuwa lazima serikali waweke wazi kwa wananchi.
Mi nadhani wanaweka wazi siri kwaajili ya mission fulani, sio burebure tu,
kwani wakiamua kukaa kimya kitatokea nini?? Nani atakayejua?
Kwahiyo hapo nahisi suala ni moja tu wapo katika mission au target fulani.
 
The bold nimeona ktk mada yako kua vijana waliochaguliwa ktk hiyo oparesheni walikua 100 hivi wakawa chini ya SAG sasa wazungu Na waarabu hawafanani..... Je ilibidi wachaguliwe askari wenye nasaba za kiarabu ili kujiunga Na SAG then ndio wakaingia Iran kufanya hizo harakati Kwa ajili ya kuhamasisha RAIA Wa kiiran? Au hao SAG wazungu walienda Iran wakachagua wairan Na kuwatrain?
Mkuu ni SAG walienda Iran wakachagua baadhi ya vijana wa Kiiran na kuwatrain..

Lakini kiongozi wa Operations wa SAG (CIA) aliyekuwepo Iran Bw. Donald Wilber alikuwa na kiasi fulani ana asili ya kiarabu (Wilber alikuwa kiongozi wa mission za kijeshi na Kermit Roosevelt alikuwa kiongozi upande wa Utawala (Senior Officer)). Pia Wilber alikuwa na ujuzi mkubwa wa lugha ya kiarabu na tamaduni zao. Hii ilitokana na ubobezi wake katika masuala ya akiolojia na historia ya kale ya Persia kama nilivyoeleza kwenye makala.

Hata muonekano wa Wilber na uvaaji wake ulikuwa wa kiarabu kabisa. Hii ilimsaidia 'kublend' kiurahisi katika jamii ya Wairan..

Nitapandisha picha yake hapa baada ya dakika kadhaa..
 
Naona hapa kwetu Chadema ndio wanatumika na siku wakiingia madarakani watafanya ya vibaraka wakienda tofauti watatolewa tu.Wito wangu kwa CCM kutoiachia nchi kwa upinzani.[emoji4] [emoji4]
 
Mi nadhani wanaweka wazi siri kwaajili ya mission fulani, sio burebure tu,
kwani wakiamua kukaa kimya kitatokea nini?? Nani atakayejua?
Kwahiyo hapo nahisi suala ni moja tu wapo katika mission au target fulani.
Kabisa Mkuu! Kwa namna fulani pia ni sehemu ya propaganda kuonyesha ulimwengu juu ya "supremacy" ya taifa la Marekani.

Ni sawa sawa na nchi nyingine inavyofanya maonyesho ya silaha nzito, makombora, na teknolojia ya kijeshi.. Ni mkakati wa kutisha maadui..

So kwa sehemu fulani nakubaliana nawe kuwa utoaji/uwekaji wazi wa siri hizi nzito huwa pia una lengo lilijificha..

Lakini pia kwa upande mwingine tufahamu kuwa si suala jepesi kwa CIA kuachia hadharani siri hizi, huwa kesi zinafunguliwa mahakama kuu kudemand hizi files na kesi huunguruma kwa miaka kadhaa mpaka CIA kufikia hatua ya kuachilia hizi files..
 
Naona hapa kwetu Chadema ndio wanatumika na siku wakiingia madarakani watafanya ya vibaraka wakienda tofauti watatolewa tu.Wito wangu kwa CCM kutoiachia nchi kwa upinzani.[emoji4] [emoji4]
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Mkuu naona unataka kuwachokoza watu..

Sio kwamba CCM ndio imewekwa mfukoni?? Maana mikataba ya madini na gesi inatia mashaka aisee [emoji4] [emoji4]
 
Eeeeeh bwana eeeh?Sasa kama mission zenyewe zilikuwa hivi si hatari tupu?

Sipatii picha The bold wangu akizielezea in deep
Uwiiiiiiii hiyo siku nahisi sitokula chakula kwa furaha nitakayoipata.
Napenda sana makala za aina hii,sana.

Na tusubiri mkuu...
Naamini atalifanyia kazi ombi la bae.
Usijali mama, I will look into that..

Ila inabidi "unishawishi zaidi" [emoji6] [emoji39]
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Mkuu naona unataka kuwachokoza watu..

Sio kwamba CCM ndio imewekwa mfukoni?? Maana mikataba ya madini na gesi inatia mashaka aisee [emoji4] [emoji4]
Wakati mwingine ukimya ni jibu zuri sn kwa yule ajionae mwelevu Na kuongea hovyo tu.....

Nimeona hiyo comment Yake huyo jamaa ikanichfua kabisa moyo lkn nikaona nikimjibu nitampa faida..... Bora kukaa kimya maana ukimya ni bora sn....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom