Kuhusu mond kusapotiwa na davido hata yeye alisema na kukiri na kumshukuru davido, remix na number 1, na alisema alitumia mkwanja mwingi pale nusu kufilisika, lakini imemuingizia faida kubwa kwa mujibu wa chibu, na kweli imeleta faida.
Sasa ww ulidhania
Bro naona hatujadiliani zaidi ya kubishana kwa sababu tayari umeshaweka kichwani kuwa, yoyote anaeongelea kitu tofauti na matarajio yako kwa Diamond ni kama "hater" Wake. Na haupo peke yako humu
Imagine unabishana na facts ambazo hata Diamond na managers wake walishaliongelea.
Yani unabisha hadi role ya davido kupitia my number one remix na role ya mr flavour kupitia Nana katika kumpeleka Diamond international
Na wanapoongelea u_copy cat sio tu muziki ni hadi muonekano. Hiyo issue ya burna kuwa influenced na Fella kuti mbona ipo wazi maana mama yake alifanya nae kazi, hata wimbo wake wa last last kasample wimbo wa tony braxton lakini kampa royalties na acknowledgement, vipi kuhusu Diamond?..
Na nani alikuambia kuwa kila wimbo ni lazma uwe "hit" Kwa sababu umefanya na mtu mkubwa unless huujui muziki
Mengine umejibu bila kuelewa comment yangu na hii ndo text yangu ya mwisho katika hili, ushindi chukua mkuu
Jamaa ulivyo hater kwa Mond "Hiyo issue ya burna kuwa influenced na Fella kutti" check maneno unayotumia ila diamond et ni copy cat. Aya Fella kutti alilipwa royalties?????
Na managers wa Diamond au Diamond ku wa recognised Davido au Mr Flavour ni kuendelea kuweka mahusiano yao ya kikazi sawa, kwani Davido hana collabo nyingine na wabongo? Mbona wao hakuwasogeza kimataifa? Hilo nakupinga kwa ssb since then Diamond amekuwa aki appear katika matukio makubwa ya kimuziki duniani kama kupata tuzo au shows ata bila hao kina Davido au Mr Flavour.
Ingekuwa angegota kimafanikio baada ya influence ya Mr Flavour na Davido km ilivyokuwa kwa Ali kiba, Ali kiba baada ya kupata connection ya kimataifa enzi za kina R Kelly basi ningekwambia.
Ila kwa Diamond has been growing even without those A list artist in Nigeria.
Na kuhusu muonekano Diamond ndio kaanza kuvaa hivi wayback, koti kwenye commando wa Nigeria wanadai amemuiga burna wakati Diamond alishalitumia kwenye tetema, kuvaa oversize Diamond kavaa even before wasanii wabongo hawajuhi fashion, buti la jeje, suruali la jeje ila watu wakawa wanamcheka ila sasa hv wasanii wote wakibongo wanavaa hivyo.
Kuvaa vidani mbali mbali Diamond ndio muda sana anavaa ila kwa vile tutafute fimbo ya kumchapia tumwambie anamuiga Asake wakati Asake ata miaka 4 kwenye game hana na Diamond tayari amekuw akivaa hivyo, au Diamond ndio mara ya kwanza kusuka?
Au kila wanalosema hao wanigeria ni kweli???? Diamond amekuwa akifanya hivyo miaka mingi nyuma tena sidhani km anamuiga msanii fulani kutoka Nigeria maaana hizo fashion huwa trends za dunia