Top ten ya Mikoa inayoongoza kuchangia pato la Taifa

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
9,034
Reaction score
6,913
Niwasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Moja kwa moja kwenye mada,Kila mkoa na wananchi wake wanachangia sana kukuza uchumi wa Nchi na pato lao,lakini Ifuatayo ni Mikoa 10 ya wachapa kazi inayoongoza kuchangia pato la Taifa "GDP" zaidi kuliko Mikoa mingine.Ni muhimu kuibainisha na kuitambua ili kuipa credit stahiki.(Regions with the Largest Shares of GDP 2019), Figures in Million TZS.

1. Dar es Salaam = 23,896,520 (17.1%)

2. Mwanza = 10,285,442 (7.4%)

3. Mbeya = 7,849,917 (5.6%)

4. Shinyanga incl.Simiyu = 7,175,982 (5.1%)

5. Morogoro = 6,716,296 (4.8%)

6. Arusha = 6,562,356 (4.7%)

7. Tanga = 6,548,355 (4.7%)

8. Kilimanjaro = 6,298,586 (4.5%)

9. Geita = 6,211,376 (4.4%)

10. Ruvuma = 5,317,073 (3.8%)

MY TAKE: Nimefurahishwa na kuendelea kupungua kwa gap la kiuchumi kati ya Dar na Mikoa Mingine. Ukiangalia hapo utakuta mikoa 3 inayoifuatia Dar es Saalam kwa pamoja imechangia zaidi kuliko Dar ingawa gap bado ni kubwa but natumai litazidi kupungua kadiri uwekezaji unavyokua mikoani na kufuta kabisa utegemezi wa uchumi kwa Mkoa wa Dar na ile dhana ya Dar ndio Tanzania.

Pili nitoe pongezi kwa Mikoa ya Mwanza, Mbeya na Geita kwa kuendelea kufanya vizuri, japo inashangaza kuona mkoa kama Morogoro, Lindi, Ruvuma, Kagera, Njombe, Mtwara na Kigoma kushindwa kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa maana mikoa hiyo ina kila kitu kinachoweza kuufanya kuongoza Kitafa. kama ardhi nzuri, mvua za kutosha, mifugo, madini, misitu bahari, maziwa nk

Kana kwamba haitoshi ifike mahala viongozi wa mikoa mingine wapewe malengo ya miaka 5, kwa sababau haiingii akilini kwamba zaidi ya mikoa 16 iliyobaki iko chini ya asilimia 3.5% ,sasa hapa si wanalishwa bure hawa. Kwa maelezo zaidi soma PDF hapa chini pg 48-54.

SOURCE-NATIONAL ACCOUNTS OF TANZANIA MAINLAND 2013-2019, SECOND EDITION IN THE REVISED GDP SERIES BASE YEAR 2015

CREDITS - National Bureau of Statistics, Ministry of Finance and Planning, November 2020.
 

Attachments

Hii inaonyesha kumekua na maendeleo makubwa ya uchumi katika uwekezaji huko mikoani
Na haya ni matokeo ya Juhudi za kuboresha miundombinu muhimu kama barabara, reli, umeme, maji nk

Kazi iendelee
 
Mkoa wa Mara umezidiwaje na Ruvuma? Mgodi wa North Mara ule si wa tatu kwa uzalishaji Afrika?

Ina maana hauchangii katika pato la taifa hata tuwe top 3?
Ndio utajua hujui yaani kwa haraka haraka inaonesha mikoa inayotegemea biashara na kilimoiko vizuri kuliko yenye viwanda na migodi
 
Nimefurahi kuiona Geita ikiinua chato
 
Hii inaonyesha kumekua na maendeleo makubwa ya uchumi katika uwekezaji huko mikoani
Na haya ni matokeo ya Juhudi za kuboresha miundombinu muhimu kama barabara, reli, umeme, maji nk

Kazi iendelee
Soon mtaanza kutoka Dar na kuhamia mikoani,time will tell
 
CCM wanatakiwa kuja na mkakati kuhusu mikoa ya mipakani. Inatakiwa mikoa hiyo iwe masoko makuu ya nchi zinazotuzunguka.
Ni kweli mkuu yaani mkoa kama Kigoma,Mara,Kagera nk iko njema sana lakini cha ajabu hakuna inachozalisha cha maana ,kiufupi inategemea mikoa mingine hii sio sawa
 
Ndio utajua hujui yaani kwa haraka haraka inaonesha mikoa inayotegemea biashara na kilimoiko vizuri kuliko yenye viwanda na migodi
Ni ajabu sana!
Nimeacha kijijini kwetu watu wanachimba dhahabu (wachimbaji wadogo) na wamejikwamua kweli kiuchumi na serikali inabeba mapato.

Mkoa wa Mara una dhahabu nyingi sana
Ajabu sana hatupo kwenye list.

Mandhari ya kijijini kwetu



 
Ndio utajua hujui yaani kwa haraka haraka inaonesha mikoa inayotegemea biashara na kilimoiko vizuri kuliko yenye viwanda na migodi
Kuna mikoa inayoliingizia taifa fedha na mikoa yenye pato/gdp kubwa.
Kuna utofauti.

Kwa mfano, mikoa yote kwenye hiyo list ukijumlisha mchango wao kwenye kodi inayoingia serikalini (ukiondoa Dar). Halifiki mchango wa mkoa wa Arusha peke yake.
 
Mkuu Mkuu tuwekee na data za per capita. Hilo ndilo linaonyesha kipato cha mtu mmojammoja na hali halisi ya maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…