Top ten ya Mikoa inayoongoza kuchangia pato la Taifa

Mheshimiwa, michango ktk GDP ya Taifa (Tanzania Muungano au Tanzania - Tanganyika?), na kama Muungano Zanzibar iko wapi? maana juzi tumegawana zile gharama zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sikukuu ya muungano.
 
Hii inaonyesha kumekua na maendeleo makubwa ya uchumi katika uwekezaji huko mikoani
Na haya ni matokeo ya Juhudi za kuboresha miundombinu muhimu kama barabara, reli, umeme, maji nk

Kazi iendelee

Dar ilifaidi tu centralization ya shughuli za serikali, kibiashara na bandari (sababu zingine zilidumaa au kudumazwa) ambayo ilipelekea kuwa na population kubwa sana, ila kiuhalisia haina natural advantage yoyote kwa shughuli za kiuchumi kulinganisha hata na Tanga.

Kiufupi Dar imekuzwa tu

na kwa decentralization inayoendelea ya kiserikali, Bandari nyingine zikipanuliwa zaidi, Huduma za kijamii na miundombinu inavyopanuliwa mikoani

Influence ya Dar itazidi kushuka zaidi ya Hapa japo itaendelea kuwa commercial city ta Tz kwa miaka mingi zaidi
 
Mheshimiwa, michango ktk GDP ya Taifa (Tanzania Muungano au Tanzania - Tanganyika?), na kama Muungano Zanzibar iko wapi? maana juzi tumegawana zile gharama zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sikukuu ya muungano.
Uwe unasoma sio kukirupuka ,Rudi kwenye pdf hapo kuna hayo majibu ya maswali yako
 
Na mimi nataka ishuke zaidi Ili tuheahimiane

Miaka 20 ijayo bila shaka inaweza.kujikuta at par na mikoa mingine, yaani nataka tufike mahala kama Jimbo la california kuongoza kiuchumi marekani lakini stii Jiji la Newyork ndio Jiji kuu la uchumi
 
Wewe una shida na Mkoa wa Dar.
Viwanda vyote vikubwa viko Dar na Watu wengi wako Dar, inapitwaje?
 
Una chuki na Dar
Chuki ya nini na kwa nini niwe na chuki? kwani kutoa maoni mbadala ndio chuki? Hilo ni wazi mtaanza kutoka Dar kuja mikoani.Kwa nini nasema hivi,jibu ni moja uwekezaji mkubwa unafanyika mikoani bandari mpya zinajengwa,viwanja vya ndege na miji mingine inakua vyote hivi vitasababisha utegemezi kwa Dar kupungua na kuifanya Dar ya kawaida.

Hivi ndivyo maendeleo yanavyotaka yaani diversification kiasi kwamba hata kasi ya watu kukimbilia Dar itapungua,na uwekezaji huu unafanyika kote kuanzia sekta za uchumi hadi za kijamii.Saizi nikitaka CT Scan naishia mbeya tuu,nikitaka heart surgery sio lazi ma kuja Dar naenda DOM,Cancer hivyo hivyo sasa huoni kwamba ushawishi wa Dar unapungua?
 
Nashangaa Iringa haipo.

Kwa nini Shinyanga na Simiyu zimewekwa pamoja?

Kilimanjaro wanajitahidi katika hiyo top ten ndiyo mkoa wenye idadi ndogo ya watu ila wapo hapo walipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…