ALEX_ANDER
JF-Expert Member
- Jul 8, 2014
- 570
- 816
Ila mkuu naona ni fursa sema wengi wetu tutakuwa hatuna elimu ya kutosha kwenye uendeshaji wa hizi biashara
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna cha maslahi ya taifa, sema unatafuta kula yako, tena kula ya ulaini! Maana sasa kula yako inatokana na hard earned money, siyo kama kwenye siasa ambapo ni kama kokota! Unadhani do you make any impact for the benefit of masses kwa kuandika humu?Mkuu Retired, mimi nipo sana tuu, ila kwa sasa kufuatia mimi kuwa ni kada, hoja zangu nimezielekeza zaidi kwa maslahi ya taifa.
P
Wanabodi,
Japo hili ni Jukwaa la Siasa, na hii ni story ya fursa za Kiuchumi, issues zozote za utilities, umeme, maji na mafuta, ni siasa, hivyo ikitokea sintofahamu yoyote kwenye issues za mafuta ya fuel, nchi inatikisika!.
Kumetokea Tangazo fulani la Total kwenye gazeti, kuna jamaa ka panic, anataka kuwapanikisha Watanzania!.
What happened? Total yafungasha virago vyake Tanzania(?)
Kabla sijakisema nilicho dhamiria, naomba kwanza nitoe elimu kidogo kuhusu biashara ya mafuta na gesi Tanzanian.
Biashara ya mafuta na gesi Tanzanian imegawanyika katika makundi mawili,
1. Upstream- Watafutaji mafuta na gesi, wachimbaji mafuta na gesi, hawa wanadhinitiwa na PURA.
2. Downstream- hawa ni wasambazaji wa mafuta na gesi, yaani makampuni ya mafuta. Hawa wanadhibitiwa na EWURA.
Kwenye usambazaji wa mafuta, nako kuna makundi mawili,
Waagizaji wa mafuta ya jumla, bulk procurement na wasambazaji wa mafuta ambao wanachukua kutoka kwa bulk na kuuza kwenye vituo vya mafuta.
Ni makampuni machache ambayo wanafanya biashara ya mafuta kuanzia upstream, downstream na retail supply, kwa Tanzania kampuni ya kwanza ilikuwa Shell, ya Waingereza, pili Agip ya Wataliano na tatu ilikuwa Total ya Wafaransa.
Shell iliuzwa sasa ndio Puma, Agip ikauzwa na kuwa Gapco, hivyo kwa sasa, baada ya Total kuinunua Gapco, Tanzania, kampuni kubwa ya mafuta, kwa upande wa mtandao wa vituo vya mafuta, ni Total.
Kwa msio jua, Total ndio kampuni inayoongoza kwa uwekezaji Tanzania, yaani investment, mradi wa bomba la gesi la Hoima Uganda hadi Chongoleani ndio the biggest investment in the history of TIC, hata Dangote atasubiri!.
Tukija kwenye biashara ya reja reja ya mafuta, Total ndio inayoongoza kwa wingi wa vituo vingi.
Sasa naomba kuendesha shule fupi ya maneno matatu haya, COCO, CODO na DODO kuhusu vituo vya mafuta vya Total.
Kuna aina tatu ya vituo vya mafuta vya Total.
COCO ni Company Owned, Company Operated, hivi ni vituo vinavyomilikiwa na kampuni ya Total, 100% kwa 100% na kampuni ya Total inaviendesha, vikiwemo vituo vyake vyenyewe na vituo vyote vilivyokuwa Gapco.
CODO ni Company Owned, Dealer Operated, ni vituo ambayo Total inavimiliki lakini vinaendeshwa na watu wengine, dealers.
DODO ni Dealer Owned, Dealer Operated, hii ni mtu au kampuni binafsi inamiliki kituo na kukiendesha, ila Total wanakupa mkataba wa franchise, kwa kukijenga kwa viwango vya Total na kuuza bidhaa za Total.
Sasa Total Tanzania imemwaga fursa kibao kwa Watanzania kumiliki vituo kwa huo mtindo wa DODO ambapo Total inauza vituo vyake vyote vya COCO na CODO kuwa DODO!.
Changamkia Fursa.
Naomba kuchukua fursa hii kuwaonyesha uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Dodo uliofanyika jana pale Goba Mshigeni.
Kwa faida ya wasiojua mambo ya Total karibuni mitaa hii
Kampuni ya Total Yainunua Gapco na Kuwa The Biggest Oil Company in Tanzania, Kenya & Uganda.
Maendeleo ya Kweli Yataletwa na Watanzania: Kampuni ya Mafuta ya Total Yazindua Kituo cha Kwanza cha Watanzania, Total Tegeta Service Station
Jee Kuna Ukweli Kuwa in Tanzania, Mafuta ya Vituo vya Total, " They are The Best?. If Yes, How Wakati Tunanunua Bulk?.
Leo ni Valentine: Jaza mafuta kituo cha Total, upate Zawadi ya punguzo la bei ya mafuta.
From Hyatt Regency, The Kilimanjaro: the 2nd Tanzania Oil & Gas Congress. Wazungu Wengi Kuliko Wenyeji!
Total Tanzania yazindua shindano la 'startupper of the year by total'
Total Tanzania Yafanya Makubwa, Kuigeuza Tanzania Kama Ulaya!, Yaanzia Temeke.
Vita dhidi maambukizi ya corona Tanzania, kampuni ya Total Tanzania mfano wa kuigwa!. Ukifika lazima unawe, upimwe na mashine ndipo uruhusiwe kuingia!
Paskali
Dodo la Total ni bonge la fursa!.
P
Idea ya kuuza hizo kampuni ndogo ndogo ni nzuri kwa sababu itasaidia kuongeza mzunguko wa pesa kwa jamii, sijui kama bei ya hizo kampuni itakuwa nzuri kwa watanzania ili wengi waweze kujitokeza kuzinunua.
Lakini pia serikali kujiingiza kwenye biashara ya mafuta nayo inaweza kupunguza idadi ya wataojitokeza kununua hizo kampuni kwa kuhofia ushindani na serikali kwenye biashara ya mafuta.
Swali langu ni je? Itabaki nembo ya TOTAL vile vile? Na je oil zao zitaendelea kupatikana kwa bei ile ile au ndo zitapotea kama zilivyopoteaga oil za BPNo sijawahi kuwa MC event yoyote ya Total
P
No, brand ya Total itaendelea, BP, waliuza jumla, kama Total iliponunua GAPCO, hii wanachofanya ni vituo wa COCO na CODO, kuwa DODO.Swali langu ni je? Itabaki nembo ya TOTAL vile vile? Na je oil zao zitaendelea kupatikana kwa bei ile ile au ndo zitapotea kama zilivyopoteaga oil za BP
True!.
Total is selling her properties, from plots, depots to Service stations. CODO ni leasing your properties to another person/company kwa muda, so hili kwa Total halipo, and you know that Paschal.No, brand ya Total itaendelea, BP, waliuza jumla, kama Total iliponunua GAPCO, hii wanachofanya ni vituo wa COCO na CODO, kuwa DODO.
P