Total yatoa fursa vituo vya COCO na CODO kuzigeuza DODO! Kuwa umiliki kituo cha mafuta cha total

Ila mkuu naona ni fursa sema wengi wetu tutakuwa hatuna elimu ya kutosha kwenye uendeshaji wa hizi biashara
 
Pascal acha upotoshaji. Naona kama kawaida yako umeamua kuja kufanya damage control baada ya kuona uzi wa mtu aliyeukiza kunani Total baada ya Tangazo Lao kuuza depot zao na Mali zao.

Labda nikuulize tu Pascal kama biashara na uwekezaji wa Total hapa Tanzania unaenda vizuri na kuwalipa kwa nini wanauza Mali zao depot zao????

Pili umeelezea mradi wa Bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania kama moja ya miradi yao wanaotaka kujikita nayo. Sasa nikuulize Je imekuwaje huo mradi Kukwama hadi saivi??? Maana hadi saivi hatuoni huo mradi ukiendelea????

Hoja yako ingekuwa na nguvu Kama tungeona mradi wa bomba la mafuta la Tanga ukiwa unafanya kazi sasa kama kote hatuoni lolote je unawezaje kuja na hoja mfu namna hii????

Alafu kwenye hili kumbuka pia kuna vituo vingi vya mafuta hapa Tanzania sasaivi vinaendeshwa kwa ukata na wafanyakazi wao hawalipwi mshahara kwa wakati. Je kwenye Hilo unaelezeaje juu ya sekta ya biashara ya mafuta Tanzania??? Je ipo stable????
 
Mkuu Retired, mimi nipo sana tuu, ila kwa sasa kufuatia mimi kuwa ni kada, hoja zangu nimezielekeza zaidi kwa maslahi ya taifa.
P
Hakuna cha maslahi ya taifa, sema unatafuta kula yako, tena kula ya ulaini! Maana sasa kula yako inatokana na hard earned money, siyo kama kwenye siasa ambapo ni kama kokota! Unadhani do you make any impact for the benefit of masses kwa kuandika humu?
 


Thanks Pascal,, Nmekuelewa vyema!!
 

Serikali ikishakuwa mshindani lazima pawe na kushindwa tu! Ngumu kuweza kushindana na serikali!

Case study " FastJet Vs Air Tanzania"
 
safi sana mliokuwa mnajifanya marketing hr procurement mafundi pump katafuteni kazi zingine, mie nikinunua kituo nauza mimi na mke wangu hakuna cha marketing officer
 
Maamuzi Total nyuma ya pazia ni mazingira magumu ya biashara tz, usumbufu mifumo ya kodi, serikali imeanza kujenga na kuendesha vituo vyake rejea vituo Dodoma,Dar.... Tozo nyingi toka maamlaka tofauti, Ewura, Nemc, jiji,manispaa na halmashauri. Lissu kwa siku chache kaweza kusemea taifa kuliko wabunge mamia wa ccm wapiga makofi.
 
Swali langu ni je? Itabaki nembo ya TOTAL vile vile? Na je oil zao zitaendelea kupatikana kwa bei ile ile au ndo zitapotea kama zilivyopoteaga oil za BP
No, brand ya Total itaendelea, BP, waliuza jumla, kama Total iliponunua GAPCO, hii wanachofanya ni vituo wa COCO na CODO, kuwa DODO.
P
 
Si kweli pasco labda uendelee na shule.
Lile tangazo ni la kuuza na si ubia, pia linasema anauza had depot hapo unasemaje ni CoCo au DoDo wakati wanauza?

Nilitegemea useme inauzwa kama shell ili watz tuchangamkie fursa kumbe wewe unaleta propaganda apply to good name, oooh poor u!!!!
 
Mbona advertisement yao inasema tofauti kabisa. Total wanauza mali zao zote kuanzia depots mpaka service stations. Je wanafanya hvyo kwa Nchi zote walizo na uwekezaji au ni Tanzania tu?

I know about Franchising, ila hili la Total sio franchising. Let's wait and see. Ila navyoona Total anafunga downstream business yake kwa Tanzania
 
Sioni fursa yoyote hapo zaidi ya anguko lakibiashara kwa hao watakaokuja kumiliki hivyo vituo.Kumbuka mabeberu sio wajinga kivile.Hizo nyingine ulizotuletea ni terminology tu ila ujatuambia sababu hasa zawao kufikia maamuzi hayo ili kuondoa sintofahamu iliyojitokeza.Ila ngoja tusubiri muda utatupa majibu sahihi.
 
No, brand ya Total itaendelea, BP, waliuza jumla, kama Total iliponunua GAPCO, hii wanachofanya ni vituo wa COCO na CODO, kuwa DODO.
P
Total is selling her properties, from plots, depots to Service stations. CODO ni leasing your properties to another person/company kwa muda, so hili kwa Total halipo, and you know that Paschal.

By selling her properties that means she owns non, so COCO haitahusika hapa.

DODO kidogo inaweza kuhusika ila nayo ni mpaka tupate agreements behind the selling process. Yawezekana ikawa total ownership kiasi kwamba mpaka brand name Dealer aliyenunua akaamua kubadilisha akaweka lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…