Japkas
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 3,011
- 4,617
Wakati wameindoa tulipolalamika tulitoa maoni kuwa hata wakiweka 100K- 150K tutatoa.Bima ya Afya ya Taifa wamezindua vifushi vipya ambapo kubwa ilikuwa ni kilio cha watanzania kuhusu toto afya kadi ambayo ilifutwa awali na kwasasa usajili utakuwa kama ifuatavyo
kama unataka kumsajili mtoto wako ambae sio mwanafunzi utalazimika kulipa kiasi cha shilingi laki moja na nusu kwa mwaka
mfumo wa pili utakuwa ni kwa makundi ambapo watasajili kwa kiasi cha shilingi elf hamsini na nne, watasajiliwa kupitia shule za awali msingi na sekindari
swali hivi Nhif wanaona shida gani kubakia na bei ya elf hamsini na nne kwa watoto wote kuliko huu usumbufu ..
Hata hivyo 150K kwa watoto ambao hawako shule ni sawa kabisa. Kundi la watoto wa miaka mitano(5) kushuka chini wanaumwa mara kwa mara. Kwa mwaka kama ni cash unajikuta umetumia zaidi 500K kwa ajili ya matibabu pekee.