Toto afya kadi yarejea usajili mtoto mmoja Tsh 150,000 na wale wa makundi Tsh. 50,400

Wakati wameindoa tulipolalamika tulitoa maoni kuwa hata wakiweka 100K- 150K tutatoa.

Hata hivyo 150K kwa watoto ambao hawako shule ni sawa kabisa. Kundi la watoto wa miaka mitano(5) kushuka chini wanaumwa mara kwa mara. Kwa mwaka kama ni cash unajikuta umetumia zaidi 500K kwa ajili ya matibabu pekee.
 
Pamoja na kulalamikia bei ya bima lakini wengi wetu tunajisajili au kusajili watoto wakiwa wameanza kuumwa,hilo ndiyo tatizo.

Hii ni kweli kabisa japo nilifikiri ipo haja ya kutafuta muarobaini wake BILA kuadhibu watu wote.....
Mfano: Mtu akilipia bima, ianze kuhesabiwa/kufanya kazi baada ya mwezi (siku 30). Hii ina maana mtoto akiumwa ukilipia Bima hutaweza kuitumia hadi baada ya mwezi (siku 30) ambapo wenye watoto wanajua kuwa; magonjwa ya kawaida ya watoto hupona kabisa ndani ya mwezi. Naamini kwa kufanya hivyo utakuwa umesha maliza tatizo la kusibiri mtoto augue ndio mzazi akate Bima
 
Hakuna afadhalii kabisaaa
 
Watanzania twapenda kumbatia ujinga.
Mtu hajalazimishwa lipia afu analalamika,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…