Tottenham Hotspurs Thread

Steven Bergwijn kakosa nafasi mbili za wazi. Tulikuwa na big chances 4 kwa 0. Ilitakiwa tuwapige game ya leo.
Mkuu uliangalia game? Nipe starts za short on target kati ya liver na spurs tuone
 
Sijazungumzia hizo. Nimekuwa very specific: Big chances 0 - 4
Ni ajabu pamoja na kupaki basi liva iliweza kupiga shots on target zaidi ya 10.

Ingebaki suluhu mourinho angeongea shombo kwa hizo stats ni bora amenyamazishwa.

Now bado europa.
 
Ni ajabu pamoja na kupaki basi liva iliweza kupiga shots on target zaidi ya 10.

Ingebaki suluhu mourinho angeongea shombo kwa hizo stats ni bora amenyamazishwa.

Now bado europa.
Kwa quality ya attackers wa Looserpool hata ukiwadhibi bado watafanya shots on target, ingawa ndiyo hivyo zilikuwa weak shots. Sabu ya Moura ilitugharimu sana. Hatari nyingi kipindi cha pili kilianzia eneo lake. Kuna wachezaji hawajui umuhimu wa kupata matokeo mazuri. Hakuwa mzuri both with & without the ball.
 
Bro ishu siyo shots on target ishu ni kua na shots nyingi on target na huku mmepaki basi.

Timu waliyocheza nayo ucl, Midjtallyand (sijui kama sijakosea), haikua treated hivi na ina jina kama password ya hotspot.

Huyu mourinho ni kocha ila asipobadilika kazi mtakua nayo.
 
Sioni sababu ya Mourinho kubadilika. Kucheza kila mechi kulingana na mpinzani alivyo ndiko kumempa mafanikio miaka nenda rudi. Hata yeye alikiri kuwa kuna mambo kadhaa anajifunza ili awe up to date ila hawezi kubadilisha mambo ya msingi yanayomjmfanya awe Mourinho.

Wengi wanatamani aende pale Anfield na atafute ushindi kwa kucheza mchezo wa wazi. Ile ni Liverpool, timu bora ya dunia, ikiwa nyumbani! Spurs inayocheza na akina Eric Dier, Sissoko na Serge Aurier kwenye first eleven ifunguke dk 90 mbele ya Liverpool?

Jose ni kocha mzuri na huenda akawashangaza watu mwishoni mwa msimu.
 
Nilivyosema abadilike nilimaanisha kikosi of coz ukicheza na timu iliyokuzidi usipoonyesha kuiheshimu kwa kujilinda utakufa nyingi utie aibu.
 
Ni ajabu pamoja na kupaki basi liva iliweza kupiga shots on target zaidi ya 10.

Ingebaki suluhu mourinho angeongea shombo kwa hizo stats ni bora amenyamazishwa.

Now bado europa.
Europa hana mpinzani
 
Tottenham wanahitaji kuimarisha defense kwa usajili mzuri ili timu iwe na balance nzuri ya kushambulia.
 
Nilivyosema abadilike nilimaanisha kikosi of coz ukicheza na timu iliyokuzidi usipoonyesha kuiheshimu kwa kujilinda utakufa nyingi utie aibu.
Pamoja mkuu, now nimekusoma fresh.
 
Halafu jukwaa lao limeanza kihuni.

Eti "Avumaye baharini papa ...."
Hili chama linakwenda kupewa heshima yake stahiki muda si mrefu. Imefika hatua Spurs inajiona ina "wajibu" wa kushinda Anfield kwa timu bora ya dunia!?

Beast mode activated. We are out for glory.

Tottenham wanahitaji kuimarisha defense kwa usajili mzuri ili timu iwe na balance nzuri ya kushambulia.
Well said. Pale ni lazima kupata CB anayecheza kushoto atakayekuwa mbadala wa Super Jan Vertonghen. Dier ni ile anajituma tu, siyo wa kiwango kinachotakiwa. Yule dogo Rodon bado sana, nadhani Levy keshapata majibu.
 
Kweli?

Mmepigwa na Royal Antwerp.

Mmesuluhu tatu tatu na Ludogorets.

Ni kweli hakuna wapinzani?
Hizo mechi tulizofanya vibaya zote alianza na kikosi cha pili ambao kama alivyosema "hawana motivation". Kwenye knockouts itakuwa full squads na hapo ndipo watu watamkumbuka yule Jose wa vikombe. Yule Jose ambaye aliwapa United vikombe vyao vya mwisho kubeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…