Liverpool alikua na chansi ya kugombea ligi na ucl ufinyu wa kikosi ukamfanya akazanie ucl.
Msimu uliofuata akajikuta na tatizo hilo hilo akajikuta anakazania ligi.
Msimu huu bado ana tatizo hilo hilo.
Kocha wao hua anaongea kwa dharau kwamba hahangaiki na vikombe vidogo lakini siyo kweli sababu kuu ni kutokua na kikosi kipana.
City misimu kadhaa nyuma alikua anaweza kugombea vikombe vyote misimu ya hv karibuni haiwezekani tena as hana kikosi kipana.
Tunakuja kwenu.
Wewe unasema kikosi kilichopigwa na kusuluhu ni cha pili (ni uongo ila ngoja nidebunk logic yako) hivyo ili ushinde inabidi uchezeshe kikosi cha kwanza.
Hiki kikosi cha kwanza inabidi kicheze kwenye ligi pia. Kwa hiyo focus iko wapi? Ligi europa? Hakiwezi kushika vyote kuna kimoja kitateleza hivyo jiandaeni kutia aibu europa kwakua kwa sifa za mourinho atataka kugangamala kwenye ligi.
Uchambuzi hai kabisa. Umenena vyema kabisa kuhusu Looserpool na City. Napenda sana kuona mpira unajadiliwa na mtu anayeujua na kuufuatilia kisawasawa.
Ila kuhusu Spurs ngoja nikupe kidogo story ya Jose kutaka vyote msimu huu.
Ifahamike kuwa makocha wengi waliofanikiwa na kutwaa vikombe vingi kama vile SAF, Pep na Jose, huwa hawachagui vikombe na ndiyo sababu makocha hawa wametwaa vikombe vingi. Na hii ndiyo sababu Klopp anaweza kuishia kuwa na jina kubwa kuliko idadi ya vikombe kama mzee Wenger.
Aghalabu hutokea misimu ambayo hawawezi kugombea kila kitu. Mf; Pep na Jose 2016/17.
Jose na makombe madogo msimu huu:
Kabla ya dirisha la usajili lililopita ilikuwa wazi kuwa Spurs wangekuja msimu huu kugombea makombe 3 ya Europa, FA na Carabao. Kuhusu Europa Jose alinukuliwa akisema kuelekea mchezo wao dhidi ya Leicester ambao ungewapa ticket ya kucheza Europa kuwa aliwaambia wachezaji kwamba wamebakiza mchezo mmoja tu "watwae" Europa. Yaani kwamba kwa kushiriki tu wamekwisha beba kombe. Hapo haihitaji kujiuliza Jose ana dhamira gani na kombe hilo.
Jose na EPL msimu huu.
Imani ya kuwa timu yake inaweza beba ubingwa wa ligi ilianza baada ya dirisha kukamilika na Levy kumpatia wachezaji wengi zaidi ya matarajio yake (kwa mujibu wake mwenyewe).
Alipewa wachezaji 7 ambao wanagusa karibu kila eneo aliloripoti udhaifu kwa klabu. Ni mchezaji mmoja tu ambae hakupewa alichotaka miongoni mwa hao; Joe Rodon kutoka Swansea badala ya Milan Skriniar. Inadaiwa kuwa baada ya mechi mbili tatu za ligi aliwaambia wachezaji wake kuwa "anadhani wanaweza pia kutwaa ubingwa wa ligi.
Kikosi gani kimecheza Europa.
Kwenye raundi 3 za awali kama ilivyotarajiwa, alitumia kikosi cha kwanza. Baada ya mechi za makundi kuanza aliamua kuwatumia squad players. Tatizo likawa Spurs haishindi mpaka alazimike kuwaingiza senior players. Na hili alililalamikia mara nyingi kwamba linamfanya ashindwe kufanya rotation.
Tarajia kwenye knockout games (siyo za Europa tu) kuwa atakuwa akishusha full squad huku akijaribu kuua mchezo mapema ili awapumzishe nyota wake kwa ajili ya michezo ya ligi.
NB: Ikumbukwe kuwa Jose hahitaji kikosi kikali kubeba knockout cups. Anachohitaji ni kikosi chenye balance ya kiwango flani tu na wachezaji wanaomtii. Rejea alivyotwaa Europa na Carabao mwaka 2017 na kile kikosi cha United ambacho makocha wengi tu wakubwa wangeshuka nacho daraja. Siku ya fainali na Ajax, wachezaji watano wa kikosi cha kwanza walikuwa na magongo!