Tottenham Hotspurs Thread

hizo ni hasira zako wewe shabiki bado hasira za wachezaji kwa kocha, muda si mrefu utasikia wamegombana nae.
Siyo watagombana naye, tayari kuna wachezaji washagombana naye. Jose ni serial winner anayehitaji wachezaji wanataka kushinda. Wachezaji wavivu kama akina Danny Rose ni lazima tu atagombana nao.

Ndombele pia alileta U-Pogba akapigwa benchi mpaka akaamua kupevuka acheze kwa bidii. Angalia sasa namna anavyokuwa mzuri uwanjani both with and without the ball.

Winks pia wiki kadhaa zilizopita alimwambia kocha kuwa anataka kucheza mara kwa mara baada ya kusugua benchi. Kocha alimwambia wembe ni ule ule; bidii. Dogo kaanza kukaza saa hizi kamnyang'anya tena namba bwana Sissoko.

Sema wengi mnao-mdiss Jose ni kwamba tu hamuwezi ku-cope na viwango vyake: Mentality, attitude, hard work, nk
 
Shida ya mashabiki wa spurs ni ubishi.

Hamjashinda mechi yoyote tangu lini?
 
Kane anachezeshaje timu katika 3 4 3 ambayo yeye ni CF?

Au wewe ulivyoona jana ulijua Kane anakaa namba ngapi?
 
Kane anachezeshaje timu katika 3 4 3 ambayo yeye ni CF?

Au wewe ulivyoona jana ulijua Kane anakaa namba ngapi?
Hii inamaanisha haujajua Spurs inachezaje ikiwa na Kane msimu huu.

Kwenye game ya jana Spurs ilikuwa ikicheza 3 4 3 inapokuwa na mpira ambapo Kane alikuwa akicheza mbele kidogo ya Hojbjerg na Ndombele akijaribu kuwapenyezea Son na Bergwijn waliokuwa wakimendea uwazi nyuma ya CBs wa Looserpool.

Hiyo ndiyo namna Kane anavyotumika kumchezesha Sonny (na Bergwijn!?).

NB: Jana timu isipokuwa na mpira ilikuwa ikicheza 5 3 2 na 4 4 2 kutegemeana na movement za triggers wa Looserpool (Mane na Mo Salah). Ambapo kwenye 4 4 2 kwa mfano, mbele walibaki Sonny na Kane huku Bergwijn akienda kwenye wing(back) ya kulia na Doherty akicheza kushoto.

Wajinga wakizidi kupress na kuturudisha nyuma, Doherty alirudi nyuma na kutengeneza back 5 ambapo sasa Kane na Bergwijn wana switch Kane anarudi nyuma kidogo.
 
Bado sijaona ni wapi Kane anachezesha timu.

Umeelezea tu timu inatransit vipi ikiwa na mpira na ikiwa haina which is basic na ni obvious kwamba wing backs wakirudi kukaba backline itakua na watu 5.

Anyway, kama nyinyi mashabiki mnaamini kane ni mchezesha timu hata anapowekwa CF mimi ni nani niwapinge?
 
hebu subiri.

nimesoma mara nyingi nyingi ndiyo nimeona ulicholenga.

kwamba Kane alikua mtoa pasi kwa son na huyo mwingine?

unajua kuna 3 4 3

halafu 3 4 1 2

halafu kuna 3 4 21

halafu kuna 3 5 2

Na jana mlicheza 3 4 3 means
CB,
LWB, CMF, CMF, RWB
RMF (begsomething), CF (Kane), LMF (Son)

ila huyu CF ndiye akawa anawapelekea mpira RMF na LMF?

we jamaa ni hatari.
 
Hapa ili turahisishe tuiite 3 4 1 2

Sikutaka kuiita hivyo kwa kuwa kilikuwa kitu kisichodumu hata kwa dakika mbili. Mchezo wa jana ulikuwa ukihusisha formation nyingi sana ndani ya muda mfupi kutegemeana zaidi na positioning ya Mane na Mo Salah.

Pia simaanishi kuwa Kane ni mshambuliaji mchezeshaji mzuri. Jose analazimika kufanya hivyo kwa kuwa namba 10 wetu wote pancha! Mmoja kashindwa ku-cope na mchezo wa kocha (Dele Alli) na mwingine kila uchao majeruhi (Lo Celso).

Ndombele huwa mzuri pia pale ila tatizo ni kuwa akicheza mbele tunakosa mtu wa kuziba pengo lake pembeni ya Hojbjerg. Winks na Sissoko ni wa kawaida sana.
 
Ikiwa 3 4 1 2 hiyo 1 hukaa AM ambapo kwa timu yenu Ndombele ni AM.

2 ni Strikers ambao ni Son na Kane.

Ndombele anajua kuchezesha timu kuliko wote kwa kikosi cha jana ingekua ajabu jukumu hilo agewe kane.

Isingewezekana kocha atumie 3 4 1 2 halafu 1 awe Kane ingekua ni maajabu.

Unasema kwamba formation ilibadilika kulingana na position ya mane na salah hii 3 4 3 inakaba kati na pembeni hata kabla wing backs hawajarudi lakini kwa jana haikua hivyo.

Ndiyo maana nikasema hamna beki.

Uko sahihi kwamba siyo lazima na nyinyi mshinde kwa 4 2 3 1 ila ndiyo formation ambayo spurs wapo comfortable nayo na wanaijua.
 
Ila Mou angemsajili Ings ingekuwa poa sana, ana nguvu, mpiganaji na anafunga. Harry Kane si rahisi kucheza msimu mzima, yuko soft sana. Pili kuna haja ya kasajili beki za kueleweka, kiukweli huwa siamini kabisa defense inayoongozwa na Eric Dier.
 
Ila Mou angemsajili Ings ingekuwa poa sana, ana nguvu, mpiganaji na anafunga. Harry Kane si rahisi kucheza msimu mzima, yuko soft sana. Pili kuna haja ya kasajili beki za kueleweka, kiukweli huwa siamini kabisa defense inayoongozwa na Eric Dier.
Dier siku zote tangu zamani ni DM. Anachezeshwa tu kama beki cz hatuna beki wa maana. Yule dogo radon naona ni mzigo mzito sana.
 
Ila Mou angemsajili Ings ingekuwa poa sana, ana nguvu, mpiganaji na anafunga. Harry Kane si rahisi kucheza msimu mzima, yuko soft sana. Pili kuna haja ya kasajili beki za kueleweka, kiukweli huwa siamini kabisa defense inayoongozwa na Eric Dier.
Ings walimfukuzia sana dirisha lililopita sema huyu bwana Levy huyu ni bahili sijawahi ona. Huyu Vinicious aliyesajiliwa kwa mkopo sioni akitusaidia sana kipindi hiki Kane hayupo. Ila ngoja tusubiri Jose magic.
 
Kwa mujibu wa CEO wa Inter ni kwamba Eriksen haondoki. Hivyo tujiandae kumalizia msimu bila namba 10 wa kueleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…