Tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198 zafungiwa kwa kutangaza Mapenzi ya jinsia moja

Tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198 zafungiwa kwa kutangaza Mapenzi ya jinsia moja

Hawana uwezo wa kufunga account hasa hizo za twitter, facebook na instagram maana wamiliki wa hizi tovuti ni wa nchi zinazoheshimu hao mashoga. Hapo watakuwa wanadanganyana kwakuwa wengi huko bungeni hawajui kitu kuhusu tehema. Labda tovuti fulani fulani lakini sio account za watumiaji.
META wanalinda policy zao.. mojawapo ni haki za hawa jamaa
 
Fuatilia yanayojiri Bungeni kwenye Bunge cha 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 8 leo Aprili 17, 2023.

SERIKALI YACHUKUA HATUA KUFUNGIA TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII
Akizungumzia hatua zilizochukuliwa kupambana na wanaotangaza mapenzi ya jinsia moja, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 vikoa zaidi ya 2,456 vimefungiwa

Awali, Anatropia Lwehikila Theonest aliuliza swali Bungeni kuwa Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu mapenzi ya jinsia moja? Ambapo Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul amesema “Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa kinatafsiri Ndoa ni mahusiano ya hiyari kati ya Mwanaume na Mwanamke

Ameongeza “Pia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kufungo cha maisha jela au kisichopungua miaka 30 jela.”

MIUNDOMBINU YA DAR HALI NI MBAYA, MVUA ZIKINYESHA KAZI HAZIFANYIKI
Mbunge wa Segerea, Bonnah Ladislaus Kamoli amesema “Mvua ikinyesha Kisarawe maji yanakuja Ilala, hasa katika majimbo ya Segerea, Ukonga na Ilala kutokana na miundombinu mibovu.”

“Mfano juzi Wananchi wa Kata ya Vingunguti na Mnyamani wameshindwa kutoka ndani hadi tulipoomba msaada wa kampuni inayotengeneza barababa kusaidia kuondoa maji.”

Kwa kweli Mungu ni hakika atakuwa upande wetu kwenye hii vita. Tuwaombee sana viongozi wetu Mungu awape ujasiri wa kusema HAPANA kwa ushenzi huu wa ndoa za jisia moja toka nchi za magharibi!!.
 
Hawana uwezo wa kufunga account hasa hizo za twitter, facebook na instagram maana wamiliki wa hizi tovuti ni wa nchi zinazoheshimu hao mashoga. Hapo watakuwa wanadanganyana kwakuwa wengi huko bungeni hawajui kitu kuhusu tehema. Labda tovuti fulani fulani lakini sio account za watumiaji.
Iko namna!! Kama vipi tufungie hizo tovuti za facebook, twitter na instagram! Maisha yetu hayategemei mitandao hiyo!
 
Iko namna!! Kama vipi tufungie hizo tovuti za facebook, twitter na instagram! Maisha yetu hayategemei mitandao hiyo!
Hii inawezekana na pia wananchi wapigwe marufuku kutumia VPN or deep web.
Korea ya kaskazini ukigundulika umedownload VPN ni jela
 
Back
Top Bottom