Mimi ninayo cresta 1g FE( kavu) huu ni mwaka wa 10 ina 198000km haijawahi kufunguliwa engine, hata hiyo timing cover haijawahi funguliwa, cha ajabu hata plug sijawahi badilisha,hata AC sijawahi ongeza,kipupwe bado kama nipo Mufindi,hata belts zote kwenye pulleys sijawahi badilisha, mpaka hii engine naishangaa, ndio gari ninayoitegemea kwa safari zangu za ghafla kokote Tanzania, haijawahi kuniangusha, haijawahi kunilaza njiani, mimi ni kuamua tu nikalale wapi, nikitoka dar, ni kuamua tu nikalale wapi, kahama au nitoboe mpaka Bukoba, Hii injini ni ngumu sana, ila natumia ,oil ya castrol 5w-30 toka nimenunua gari Yokohama Japan mwaka 2008, pia natumia CAT coolant ya General Motors.
***ONYO**** usiweke maji ya bomba au ya kisima kwenye rejeta ya gari yako,