Toyota 1G-FE 2.0L VVTi engine

Siku hizi Toyota wametugeuka. Yaani salon zao nzuri nzuri zote zina engine kubwa. Mark x, Crown zote zinaanzia kwenye engine ya 4GR (cc2500) na kuendelea. Camry pia inaanzia cc2400
zinakula mafuta sana kwa matumizi ya Dar bhana, Natamani sana ATHLETE ila kwa safari za kutoka kibamba hadi sinza daily majanga
 
Kuna Premio new model, kuna corolla newodel body zipo kama Crown au Brevis, hatar
 
Hivi kuna siku Mhaya naweza kujificha kweli !!! Hebu angalia hiyo thread jinsi ilivyojaa Uhaya.
 
Ni kweli, kuhusu plugs kwa sasa nafikiria kubadilisha, ila nasita Kwa sababu sina uhakika wa kupata genuine plugs,je naweza kuzipata wapi? Pia hata timing belt genuine naweza kupata wapi hapa Dar?
Nakushauri agiza plug Dubai ndo utapata Og
 
zinakula mafuta sana kwa matumizi ya Dar bhana, Natamani sana ATHLETE ila kwa safari za kutoka kibamba hadi sinza daily majanga
Athlete imekaa vizuri saana. Sema ndio hivyo. Ni engine kubwa. Zinafaa saana kwenye safari. Kuna jamaa yangu alikuwa nalo, engine ya cc3000 3GR, anasema linatumia vizuri mafuta ukiwa highway kuliko hata ya cc2500
 
Kuna Premio new model, kuna corolla newodel body zipo kama Crown au Brevis, hatar
Premio sijaipanda wala kuiendesha. Ila Corolla ndani ni ndogo aise. Hazina nafasi ya kutosha kama kina Crown au Mark X. Nahisi pia sio comfortable kama hizo. Ila nyingi ni cc1500. So kwenye mafuta, hizo zinafaa kuliko kina Crown, Mark X
 
Athlete imekaa vizuri saana. Sema ndio hivyo. Ni engine kubwa. Zinafaa saana kwenye safari. Kuna jamaa yangu alikuwa nalo, engine ya cc3000 3GR, anasema linatumia vizuri mafuta ukiwa highway kuliko hata ya cc2500
SASA MI SAFARI KWA MSIMU AU KAMA NANUNUA NABADILISHA INJINI NA BELL-HOUSE YA GEARBOX
 
Premio sijaipanda wala kuiendesha. Ila Corolla ndani ni ndogo aise. Hazina nafasi ya kutosha kama kina Crown au Mark X. Nahisi pia sio comfortable kama hizo. Ila nyingi ni cc1500. So kwenye mafuta, hizo zinafaa kuliko kina Crown, Mark X
Kuna raha ya kuendesha 6 cylinder asikwambie mtu. Gari ndio itakupig kwenye mafuta ila compesation yake ni ile luxury unayoipata na engine inavyoitika ndio raha ya mark x, brevis au crown.
Ila naskia 4GR V6 engine kwenye mark x na Crown zipo optimised kwenye ulaji wa wese. Hazili sana kama inline 6 zile Jzx series 1Jz na 2Jz kwenye brevis.
 
Kiukweli watu wote waliotumia gari zenye engine kubwa, inline 6 au v6 wanazisifia saana kuliko zenye engine ndogo. Nilisoma review za 4GR, kweli wanasema iko efficient kuliko 1JZ na 2JZ. Ndio maana inatumika mpaka leo kwenye gari za Toyota
 
Kabisa. Mara nyingi gari za Japan zikifika km elfu 90 mpaka laki moja, wanabadilisha timing belt. Sasa sisi tunaponunua used na km elfu 70 au 80 tunasahau kubalisha. So ikifika laki naki na kitu mara nyingi lazima ikate.

Ni kweli Mkuu, japan lazima ubadilishe T/B gari ikifika laki 1 km. Lakini Mimi nilitamani kujua viashiria gani hutokea kwa gari yenye T/B iliyochoka? Je, gari kupoteza nguvu Na kuzimika ghafla ni viashiria vya T/B kuchoka?
 
Kiukweli watu wote waliotumia gari zenye engine kubwa, inline 6 au v6 wanazisifia saana kuliko zenye engine ndogo. Nilisoma review za 4GR, kweli wanasema iko efficient kuliko 1JZ na 2JZ. Ndio maana inatumika mpaka leo kwenye gari za Toyota
Engine kubwa makini sana, gari inakuwa na nguvu hata ukitaka manouvers safi
 
Ni kweli Mkuu, japan lazima ubadilishe T/B gari ikifika laki 1 km. Lakini Mimi nilitamani kujua viashiria gani hutokea kwa gari yenye T/B iliyochoka? Je, gari kupoteza nguvu Na kuzimika ghafla ni viashiria vya T/B kuchoka?
Gari linazima ghafla, inakuwa kama vile imechemsha. Na haiwaki tena. Ukijaribu kuwasha inakuwa kama umeishiwa mafuta, self-starter inastua tu halafu haliwaki. Ila kwa engine kama 1G ikikata ukiwa kwenye mwendo utasikia vyuma vinagonga kabisa kwenye engine na gari litazima ghafla
 
Premio sijaipanda wala kuiendesha. Ila Corolla ndani ni ndogo aise. Hazina nafasi ya kutosha kama kina Crown au Mark X. Nahisi pia sio comfortable kama hizo. Ila nyingi ni cc1500. So kwenye mafuta, hizo zinafaa kuliko kina Crown, Mark X
Unaijua corolla x? Au corolla police?

Zina nafasi km crown
 
Hivi kuna siku Mhaya naweza kujificha kweli !!! Hebu angalia hiyo thread jinsi ilivyojaa Uhaya.
Hapo uhaya uko wapi, yaliyoelezwa hapo ni kujaribu kubadilishana mawazo juu ya matunzo ya gari.

1: kutunza gari ni uhaya?
2:kuweka coolant kwenye gari ni uhaya?
3:kubadilisha plugs ni uhaya?
4:Gari kutofunguliwa engine 189000km+ ni
Uhaya?

Wewe inakufaa facebook, humu wanachangia great thinker tu.!!!!!
 
Ni kweli Mkuu, japan lazima ubadilishe T/B gari ikifika laki 1 km. Lakini Mimi nilitamani kujua viashiria gani hutokea kwa gari yenye T/B iliyochoka? Je, gari kupoteza nguvu Na kuzimika ghafla ni viashiria vya T/B kuchoka?
Kuna gari zibakupa warning kwenye dashboard ila.nyingine ndio lazima kufuata utaratibu wa kubadili kila 100K km.
 
Hizo zenye kutoa warning ni safi saana. Hata hizi tunazotumia inawezekana zinatoa taarifa kwenye ile display ya Navigation. Shida zimeandikwa kwa Kijapan. Niliwahi kuona alarma ya oil filter na engine oil na 5000km. Nikajua lazima inanikumbusha kufanya service.
 
Uzi mtamu sana,ila sijajua ufundi wa ku adili engine au majibu ya waliowahi badili engine mauzoefu,ujanja na majanga ningependa kuyajuA.
 
Kwa uzoefu wangu, engine ikileta shida kuwa wakatu fundi anaweza kushauri kufanya overhaul au kununua engine nyingine. Kununua engine ni gharama zaidi lakini nafikiri ndio njia bora zaidi kuliko kufanya overhaul labda kama utabahatika kupata fundi mzuri na spare parts genuine.
 
1G-FE VVTi 6 cylinder/piston ni engine nzuri sanaaa, but majuzi timing belt ilinikatikia mitaa ya majumba sita, ikapindisha valave zoote ishirini na nne kwenda kkoo naambiwa valve moja ni Tsh elf 45 mwisho wa bei ni Tsh 38 elf. Ila najilaumu mwenyewe kwakuwa check engine iliwaka sikugundua, wanashauri ukifikia km 100,000 hata kama check engine haijawaka ni bora kubadirisha Timing belt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…