Toyota 1G-FE 2.0L VVTi engine

Ni kweli Mkuu, japan lazima ubadilishe T/B gari ikifika laki 1 km. Lakini Mimi nilitamani kujua viashiria gani hutokea kwa gari yenye T/B iliyochoka? Je, gari kupoteza nguvu Na kuzimika ghafla ni viashiria vya T/B kuchoka?
Kwanza Gari huwa linazimazima bila sababu hasa ukikanyaga E/P ukiwasha linawaka na hamna sign yoyote ile, utaendaaaaa then gari linakuwa na miss/ Nguvu hupugua then sign kwenye display/dash board hutokea, kunakialama/symbol/picha yenye mfano wa engine itatokea/ zingine huandika neno 'check engine'. Hapo sasa siku zako zinahesabikaa mimi nime experience kwenye Gari yangu Lexus IS200.
 
Pole saana mkuu. 1G-FE BEAMS ndio tatizo lake hilo. Wanaiita interference engine. Yaani haifai kabisa kupitisha km 100,000 bila kubadilisha timing belt. Tafuta fundi mzuri akague vizuri. Maana kuna wakati inaharibu na pistons. Ila kama ni valves peke yake, badilisha valves, ila kama ni pistons pia, bora utafute engine nyingine used. Maana hiyo 38k x24 valves ni laki 9 na bado ufundi, wakati 1G unaweza kuipata kwenye hali nzuri kabisa kwa 1.5m au chini.
 
Ahsante sana mkuu Mashine ipo barabarani, nilipata fundi mzuri, ufundi nikalipa laki moja, overhaul gasket kit laki moja na arobaini na tano, grinder pest kopo moja, gasket maker moja, nikanunua na valve inlet/exhaust kwa elf nane nane kila moja hizi valve c original zinatoka Korea sema zipo vzuri sana. Nimeijaribu gari hadi Kibaha naona inafunguka kama kawa, Cylinder head, Piston pamoja na valve seat hazikuharibika hata kidogo, so nilifanya half overhaul.
 
Safi saana. Ndio raha ya 1G. Vipuri vinapatikana saana. Hiyo itakupeleka km za kutosha.
 
Ivi 1G-FE na 1GE ipi bora,na ipi unaeza tune/upgrade kwa urahisi kupata more performance?
 
Mkuu nina tatizo kama lako mkuu, huyu fundi mzuri niunganishe naye
 
Aqui nashukuru kwa comment zenu,mi nipo kwa service ya 1G FE,ila sasa bado sijajua ni wapi hapa Dar nipate genuine spark plugs.Mwenye kujua anisaide.
 
Siku hizi Toyota wametugeuka. Yaani salon zao nzuri nzuri zote zina engine kubwa. Mark x, Crown zote zinaanzia kwenye engine ya 4GR (cc2500) na kuendelea. Camry pia inaanzia cc2400
Nunua Platz, Allion ama Premio boss, wana 1NZ engine ya cc1490. Hawajakukacheni mazima bado kwani hizi ni economical cars. Hao kina Crown na Mark X ni luxury segment lazma ulipie comfort kwa kupigwa sheli!
 
Aqui nashukuru kwa comment zenu,mi nipo kwa service ya 1G FE,ila sasa bado sijajua ni wapi hapa Dar nipate genuine spark plugs.Mwenye kujua anisaide.
Tafta za Iridium hutokaa ujute.
 
Nunua Platz, Allion ama Premio boss, wana 1NZ engine ya cc1490. Hawajakukacheni mazima bado kwani hizi ni economical cars. Hao kina Crown na Mark X ni luxury segment lazma ulipie comfort kwa kupigwa sheli!
Hizo gari zinamuonekano mzuri. Sijawahi kuzitumia, nitakuja zitafiti kidogo nizijue vizuri.
 
Hizo gari zinamuonekano mzuri. Sijawahi kuzitumia, nitakuja zitafiti kidogo nizijue vizuri.
Za ukweli sana, hasa premio ni toleo la Corona, huwa ni semi-luxury sedans za Toyota toka kitambo tofauti na corolla ambazo ni basic sana.
 
Za ukweli sana, hasa premio ni toleo la Corona, huwa ni semi-luxury sedans za Toyota toka kitambo tofauti na corolla ambazo ni basic sana.
Okay. Ambacho sina hakika ni kama ziko fun to drive. Vile zipo nyingi mtaani, nitaomba kuijaribu niijue.
 
Kwenye fun to drive i'm not sure. I usually find inline 4's kama vyombo vya usafiri tu no thrills mayne. Hizo fun maybe kwenye V6's kama Crown, Mark X ama Lexus maybe utaweza zipata
Hapo kuna point. Inline 4 nyingi sio kivile. Labda 3 series kidogo, maana hata GT86 ni boxer engine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…