Toyota Altezza Gita (Wagon) Thread: Karibuni tujuzane ubora na udhaifu wa gari hizi

inaonekana 2JZ GTE ndo mnyama mkali kwa upande wa altezza
 
Kweli kabisa. 1G ni smooth tu vile ni inline 6. Ila 3S ina nguvu zaidi. Hizo turbocharged zinafaa saana kama unaendesha gari for fun. Ni umasikini tu unatusumbua, ila kuendesha gari lenye nguvu kuna raha yake aise
lazima nimpate huyo mnyama turbocharged 2JZ GTE
 
Kweli kabisa. 1G ni smooth tu vile ni inline 6. Ila 3S ina nguvu zaidi. Hizo turbocharged zinafaa saana kama unaendesha gari for fun. Ni umasikini tu unatusumbua, ila kuendesha gari lenye nguvu kuna raha yake aise
mzee altezza ipi yenye nguvu unaikubali?bila shaka ni turbocharged 2JZ GTE
 
powerseats na seat heaters ndo nini mzee?
Powerseats ni seats ambazo unafanya adjustment kwa button ya umeme. Unagusa button seat inasogea au kulala. Sio zile za kuvuta chuma fulani kama nondo hapo mbele ya seat ili kuisogeza.

Seat heater unagusa button seat inapata joto. So wakati wa baridi angalau unakalia seat yenye joto.
 
unamaanisha nini unaposema altezza inafurahisha kuendesha?
Ni sport saloon. Yaani walivyoitune kuanzia gearbox inavyobadilisha gia, suspension system, tairi, seat ya dereva, uzito wa steering, ukiendesha unapata burudani. Unajisikia uko connected na gari na barabara. Hasa barabara yenye kona kona. Ni tofauti saana na saloon nyingine kama kina Premio na nyingine.
 
suspension ya altezza ipoje? vipi kwenye ile kunesa nesa?
 
thank you for the information
 
Saloon RS200 yenye engine ya 3S GE ina nguvu ya kutosha. Hasa manual nafikiri ni 210hp. Inakaribiana na yenye 2JZ yenye 215hp. Ila yenyewe mafuta inatumia vizuri zaidi.
2JZ ukiongezea turbocharger mbili hapo horse power inaweza ikaongezeka hata kwa 300 hp
 
 
una maoni gani kuhusu Supra.hii nimeona engine code wameweka ni 2JZ nadhani ndo ile ile 2JZ GE.(nirekebishe kama nimekosea hapo).cc ni 2990 ila wheel drive wameweka dash sijaelewa wamemaanisha nini.cheki hapo chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…