Toyota Altezza Gita (Wagon) Thread: Karibuni tujuzane ubora na udhaifu wa gari hizi

Toyota Altezza Gita (Wagon) Thread: Karibuni tujuzane ubora na udhaifu wa gari hizi

so haiji na turbocharger toka kiwandani?kuweka turbo charger ni gharama kiasi gani?
Yes, kutoka kiwandani haina turbocharger. Bei nafikiri inategemea na aina ya kit unayoweka na fundi anayekuwekea. Kuna kits zinaanzia 2m 3m na kuendelea. Japo hizo za bei ndogo ni usumbufu.tu. Bora ubaki na 2JZ
 
2JZ ukiongezea turbocharger mbili hapo horse power inaweza ikaongezeka hata kwa 300 hp
Hehehee, 300hp ni kidogo mno aise. 2JZ unaweza ukaitune mpaka ukaikimbia wenyewe. Ni moja kati ya engine zinazovumilia power boost saana. Jamaa huwa wanafikisha mpaka 1000hp. Ila kwa kits nzuri za kawaidia, unaweza kupata 400hp na zaidi kirahisi kabisa.
 
una maoni gani kuhusu Supra.hii nimeona engine code wameweka ni 2JZ nadhani ndo ile ile 2JZ GE.(nirekebishe kama nimekosea hapo).cc ni 2990 ila wheel drive wameweka dash sijaelewa wamemaanisha nini.cheki hapo chiniView attachment 1523189View attachment 1523191View attachment 1523192View attachment 1523193View attachment 1523194View attachment 1523195
Mkuu, hilo dude kama unaliweza bei yake, chukua. Hilo ndio limetangaza jina ya 2JZ duniani. Kuna ambazo sio turbocharged, ndio 2JZ GE. Ila pia zipo ambazo ni turbocharged kutoka kiwandani. Ndio zina GTE
 
Mkuu, hilo dude kama unaliweza bei yake, chukua. Hilo ndio limetangaza jina ya 2JZ duniani. Kuna ambazo sio turbocharged, ndio 2JZ GE. Ila pia zipo ambazo ni turbocharged kutoka kiwandani. Ndio zina GTE
hizo turbocharged toka kiwandani zitakuwa balaaa.bongo kuna mnyama watu wanamiliki Supra?
 
Hehehee, hata mie mwanzo nilikuwa nakichukia kwa kweli. Ila with time nimegundua kinavutia. 2JZ safi saana. Kwanza ile engine kwa kweli, huwa haina shida za ajabu ajabu. Ukizoea mafuta yake, utaifurahia saana.
engine za 2JZ zinapatikana mtaani?
 
Kama haupo vizuri kimfuko chukua Altezza ya kawaida cc2000 yenye six cylinder engine ya 1G FE hii kidogo wese nafuu...

Usichukue ile ya four cylinder yenye injini y 3S yamaha yale majini
1GFE inawezekana ukafanya modifications kuweka turbo?
 
Subaru model ipi boss?
Impreza
FB_IMG_1596338227505.jpeg
 
Back
Top Bottom