Toyota Crown Athlete - ‘the Japanese Benz’

Jemedaree

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2021
Posts
676
Reaction score
2,024
Moja ya gari pendwa hapa mjini

Ni Executive sedan Inakupa kila kitu comfort,luxurious,performance&reliabilty!!

Ukiona nyingi ujue zinapendwa na affordable

Utagundua hata TRA wamezipandishia ushuru hii imepelekea hata resale value yake kuongezeka hivi

Karibuni wapenzi na wamiliki wa crown kene thread!


Everybody deserves a Crown [emoji146]

Drop your experience and picture [emoji1484]

[mention]Extrovert [/mention] our brand ambassador [emoji23][emoji91]





 
Hayo madude siyakubali. Sijui kwanini. Nadhani nimeathirika kisaikolojia najikuta nazichukia sana Saloon cars, hasa baada ya kukaa sana vijijini na kila mtu kuziita "Taxi".

Yani unaweza ukawa na chuma lako Mark X limesimama hatari. Ukipita nalo Mpitimbi au kule Kigonsera kila mwanakijiji anakupa jina, " Yule blaza mwenye taxi kapita sasa hivi" [emoji23][emoji23]

All in all, crown zimekuja kama upepo tu wa kisuri suri kama zilivyokujaga Verossa, Baloon na Mark X.. Fashion yake itapita na zitaanza kuonekana kama mtumba tu!
 

Gari sikuzote zinakuja kama upepo na kupotea
Lkn jitahidi upepo upitie kwako brother [emoji23]

Hata nyumba zina upepo piaa
Angalia nyumba za miaka ya 90’s pale magomeni ,manzese then compare early 90s msasani,mikocheni afu cheki mijengo ya 20s kule mbezi beach halafu maliza na miaka hii ya kuanzia 2015 kule Mbweni hata Goba tu
 
Upo sahihi kabisa. Basi tu mm sina flavor na hizo saloon cars. Gari yangu ya kwanza ilikua Grand Mark 2 gx100. Sikuwahi kuenjoy saaana! Always mishe zangu ni vijijini, kila wakati nilikua naonekana kama naendesha taxi tu!

Nikauza nikanunua Nissan Wingroad, pale naweza sema nilikula nayo maisha, na ilinifanya nipende hizi station wagon na SUV cars. Ingawa wingroad nilipata nayo majanga nikauza (kuna thread yake humu niliielezea)

Kwa sasa nipo na hii Harrier tako la nyani and I can't complain [emoji120]
 

Nmekupata Vizuri mkuu

Kuna sehemu umenichanganya
Kwani kuna tofauti ya saloon na sedan?
 
Umekosea kitu kimoja tu. Hizo ulizosema zimepita ni gari moja. Yaani Mark2,Verossa then ikageuka Mark X. Ila Crown ni Crown haitapotea kama Verossa au Mark 2. Crown itaendelea kuwepo zikija new models tu.

Kibongobongo watu wametoka grs180/182 wameingia grs200 na zitaemdelea hivyo bila kupotea Jina na nembo ya Crown. It's a flagship for Japanese sedan.
 

True say

Crown ni kama Rav 4,Prado au LC

Watu watakuwa wana upgrade to new model

Lakini haitapotea kirahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…