Mkuu Crown ni full-sized luxury sedan, gari ikishakuwa ni luxury lazima itakua bora, kuanzia features, comfortability, interior design n.k , Mark X ni midsize sedan...
Crown ina sensors za kutosha, safety features kwenye crown zipo nyingi kuliko Mark X, mfano chukua crown athlete/royal saloon ya 2010 tu ulinganishe safety features na mark x ya same year, mfano crown features kama Radar Collision Avoidance System, Pedestrian Detection System, Artificial Intelligence-Adaptive Suspension System n.k, umeme kwenye crown sio wa mgao, crown ina featues nyingi ambazo Mark X haina.
Mfano gari ikiwa na adaptive suspension system, hizo ni sensor na microprocessors zinakuwa zinafuatilia tairi za gari zinavyopita kwenye bara bara, sensors zinatuma hizo taarifa kwenye computer na gari ina adjust springs na shocks in real time ziendane na hali ya barabara ili kuleta smooth driving experience, sasa hii ya crown inatumia AI. Kwa hii feature tu inaelezea nani ni mshindi kwenye comfortability.
Kusema namba za ajali ndio kipimo cha comfortability ya gari unakosea, crown ipo very comfortable nahisi kuwa comfortable zaidi inapelekea mtu kutokua makini.
Kuna kipindi kuna mtu alinipa gari yake kwa muda, ilikuwa range rover old model flani, sasa kuna siku kuna msichana mmoja nikampa aendeshe mi nimekaa pembeni mbele, kuna kitu nilikua naperuzi kidogo, ilikua ni kasafari ka umbali kidogo, gari inatembea tupo sehemu barabara imenyooka, sijui ilikuaje nikaja kutazama kwenye speedmeter gari inasoma 90, ile Range ilikuwa imeandikwa kwa miles/hour, nikamuambia unatembea na speed kubwa mno ndipo akashtuka nikamuambia hii ni miles/h, hapo alikuwa zaidi ya 140km/h, lakini cha ajabu gari ilikua imetulia tuli, very comfortable yani, kiasi kwamba hata yeye mwenyewe yule manzi hakufahamu, comfortability wakati mwingine inaponza. Sasa umekula pombe unakutana na comfortability ya crown, bro what do you expect.
Crown ipo comfortable lakini huwezi sema inafikia comfortability ya Lexus LS, Mark X ipo comfortable lakini haifiki kwa crown.
Tofauti na hapo ni ushabiki maandazi tu.