Dont waste your time, Crown inaweza kusumbua gari za Kijerumani zenye cc chini ya 2000 non-turbo, tena itasumbua mbio fupi, ikipatikana stretch imenyooka hata hizo za cc2000 crown inakaa. Kuna siku naenda Tanga na Crown maeneo ya Kabuku usiku kama saa tano ghafla naona kuna taa amazing za gari ndogo ziko nyuma yangu. Tangu nimetoka Dar hakuna gari ilikuwa inanisogelea au kuresist nikitaka kupita. Baada ya kuona hizo taa nikaanza kukaza, kila nikikukuruka jamaa yupo tu 160/170 jamaa yupo nikaona isiwe tabu ngoja nione gari gani, nikalegeza mguu jamaa akatanua kucheki Audi A4 2.0T nikamuacha aende.