Mkuu
Dumbuya , Nami nina tatizo kama la mleta mada.
Kwenye silence/iddle, engine inatoa mlio wa kugonga hivi, yaani kama mlio wa kugonga hodi. Asubuhi hapana, ila usiku napomaliza mizunguko.
Na pia saahivi gari imepungua power ya kukimbia kwenye mpando hasa nikiwa nimebeba watu.
Pia nimegundua nikifika speed 120, mlio/muungurumo unakuwa juu sana. Nafunga vioo full AC muda wote, lakini muungurumo nausikia. Nilidhania labda ni matairi kuisha ndiyo inasababisha huo muungurumo. Nimeweka tyre nne zote mpya, lakini bado muungurumo wa gari unakuwa upo juu kwenye high way speed.
Speed chini ya 120 ama juu ya 120, muungurumo unapungua kidogo.
Pia, kwa mara ya kwanza nimeona oil kupungua kiasi kidogo.
Odometer inasoma km 125,000 hadi sasa.
Mwaka jana niliondoa masega ya kwenye eksozi, baada ya gari kuwa inaishiwa nguvu mlimani. Na kweli tulipoondoa masega, gari ilirudi upyaaa kwenye power, na muungurumo wa eksozi ukabaki kawaida tu with very minor difference.
Service nazingatia sana. Natumia engine oil ya TOTAL 5W30 (quartz 9000) full synthetic.
Gearbox oil nishabadilisha mara 1, niliweka ATF type IV ya toyota as recommended kwenye dipstick.
Ni Toyota IST ncp61 (1490 CC).
CC:
chilubi . ,
Kichuguu ,
Boeing 747 ,
LEGE ,
ProBook