Toyota Land Cruiser 70s - Series Moja ya Gari bora zaidi kuwahi kuundwa

Toyota Land Cruiser 70s - Series Moja ya Gari bora zaidi kuwahi kuundwa

Gari za urithi hizi, unaendesha unaliacha homeboy wako nae anaendeleza gurudumu analiendesha tu lipo moja la Mshua serikali walilinunua 1990 jipya akaja akalinunua 2000 toka serikalini kwenye minada yao!

Mpaka sahizi lipo tu anadunda nalo ukipiga hesabu ni almost 40 years toka litoke kiwandani! Lilitumika kumpeleka bibi hospitali na msibani kijijini 1992! Likaja kutumika kwenye msiba wa maza 2001!

Limebeba history sana hilo gari mzee hawezi liuza!
Na huenda likapeleka na maiti yako kijijini.. HAahaha Utani pembeni. Ukinunua hii gari unajikuta ina historia kwenye familia kama jina la ukoo. vizazi na vizazi watalikuta na kulitumia kama hawatoingia tamaa ya kuliuza. Sasa hawa wanaonunua PASSO ata mwanao hawezi jua kama ulishamiliki chuma.
 
Huyo rafiki yako ni bumunda kweli!

Unauzaje usafiri kama huo?

Hizo gari haziwahi hata kushuka bei!

Alafu waasi wengi wanazipenda sana sababu ya nguvu.

Injini yake ni 4.0L
Kimfaacho mtu chake yaani anunue yeye auze gari yake unamwita bumunda...gari inashuka bei kutokana na toleo jipya kufika la zamani litakua old model itashuka bei sasa hivi wanaita dash board kubwa ndio zipo sokoni kuliko dash board ndogo za mwaka 2009 kurudi chini hakuna gari isiyoshuka bei...
 
Tunasifu hili gari kutokana na maisha na mazingira duni tunayoishi...ila katika mazingira anayostahili kuishi binadamu hili gari sio.
Labda la kubeba kuni huko porini..
Umenichekesha sana mkuu upo sahihi maana pia magari ni changamoto sana hasa ukipata sumbufu haya imeonekana yanakubali mazingira yote..
 
Hii gari mjapani alicheza kivyake.. Mwanzo aliyumba alipoinyima lock-diff ila alipokuja kuipa lock-diff ndo ulikua mwisho wa kusema Landrover ndo gari ya tope na haikwami. kwa sasa kila chaka watu wanapiga chini TDi wanahamia kwny L/C kwa sababu ya upatikanaji wa spare na hata bei za spare zake sio mkasi tofauti na hizi LR. Kuna B number ya mwanzo kabisa ila ikiwaka ukiskia saut n kama macho panzi DQZ izi gari zingatia tu service utaendesha adi ufe hujawai shusha gear box wala fungua engine.
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Australia ni wale wale tu mkuu...lilikuwa bara la wahalifu(gereza) la Waingereza.

Wana maeneo mengi sana ambayo kuyafikia ni changamoto, inabidi watumia haya magaripori.
Hizo ni hadith tuu mkuu wale wapo mbali na hayo ni magari na pia sokoni bei yake ni moja ya magari bei zipo juu kwenye minada ya SA hayo magari ya miaka ya karibuni yapo bei juu mno...hiyo Cruiser iliyogongwa inaweza kuwa sawa bei na Range Rover isiyogongwa ya mwaka huo huo...kuuza hiyo gari ni rahisi kuliko gari yeyote Nchi yeyote kuanzia hapo hapo SA tunasema hela ipo kwenye ATM wakati wowote unachukua na mnadani zinakua chache zinagombaniwa mno
 
Na sometimes gari ni dereva siku Moja nilikuwa na cruiser hard top me nimeketi pemben engine hio hio 1 Hz tulipata jigi na brevis tuliisumbua sana ila kitu nilicho note ni kuwa jamaa wa brevis alikuwa muoga kupita maelezo kwenye Kona anapunguza mwendo kabisa
Sio muoga alikua anafata kanuni sahihi za kuendesha chombo cha moto unataka akate na mia mumuokotee porini mje mseme alikua sio muoga tena...
 
Australia ni wale wale tu mkuu...lilikuwa bara la wahalifu(gereza) la Waingereza.

Wana maeneo mengi sana ambayo kuyafikia ni changamoto, inabidi watumia haya magaripori.
Daah yaani nchi yenye uchumi wa 12 kwa ukubwa dunia mzima inaongelewa Kama Chato vile.
 
Na huenda likapeleka na maiti yako kijijini.. HAahaha Utani pembeni. Ukinunua hii gari unajikuta ina historia kwenye familia kama jina la ukoo. vizazi na vizazi watalikuta na kulitumia kama hawatoingia tamaa ya kuliuza. Sasa hawa wanaonunua PASSO ata mwanao hawezi jua kama ulishamiliki chuma.
Hahahahah kweli mzee baba gari ina history
 
hello wakuu! je ni rahisi kufanya mod ya kubadili LC 80 yenye 1hdt kwenda 1HD-FTE? najua kunakuwa na gain ya power & torque, is it a worthwhile project? reliability inakuwaje?
 
Hizi mashine hata likipata ajali vip unalikuta linawaka.. Ahsante Land Cruiser...
 

Attachments

  • 20230213_145155.jpg
    20230213_145155.jpg
    989.4 KB · Views: 45
  • 20230213_145137.jpg
    20230213_145137.jpg
    965.7 KB · Views: 40
  • 20230213_145144.jpg
    20230213_145144.jpg
    1 MB · Views: 37
hiyo yote utakosea kuipa heshima mashine ya 1HZ ile ni jiko la gesi baba..
ogopa gari inakaa silence wiki 2 bila kuizima...
ni gari naitumia sana!!shida yake macho panzi usiipige nayo side ways tuu..inakutoa utumbo chapu.
ni gari ya uhakika wa kufika nayo popote muda wowote.

Uzuri wa 1hz hata ikiwa imetembea zaidi ya km 300000 bado inadunda tu kama mpya. Uzingatie service tu
 
Back
Top Bottom