Toyota Rumion 2008 vs 2010; nichukue ipi wakuu?

Habari ya wakati huu wakuu.

Mwenzenu nimeamua kuchukua Rumion ila sasa nimekuta kuna toleo la 2007-2008 na toleo la 2010-2015.

Haya matoleo mawili nimeona yana tofauti ndogo za muonekano; show ya mbele, ndani kwenye dashboard hasa sehemu ya AC na ndani kwa nyuma. Sijui kuhusu uimara, perfomance na changamoto zake kulingana na matoleo hayo mawili.

Naombeni mnishauri nichukue ipi kwa kuzingatia uzoefu wenu.
View attachment 2071197
2010View attachment 2071198
2008

UPDATE 17 April 2022

Gari limefika tangu March mwanzoni. Niliamua kuchukua la 2008 kwa sababu ya bajeti. 2010 ushuru wake ulikuwa juu.

Gari zuri halina shida. Utulivu barabarani, space kubwa ya kutosha na lina mziki mkubwa sana, hakuna haja ya kuongeza speaker za ziada.

Changamoto yake kuu ilikuwa kugusa chini. Hata tofali la block likilazwa huvuki. Ni kama ilivyo kwa Nissan Fuga, Wish, Alphad, IST, Vitz n.k.

Nimeshaitatua hiyo changamoto kwa kuliinua. Hakuna kilichobadilika kimuonekano na utendaji na haligusi tena.

Asanteni nyote mliochangia mawazo.
Mpaka unaipata mkononi umetumia kama hela ngapi mkuu?
 
Safi mkuu ukishalipata itupe mrejesho wa wadau mara sijui bampa limeshuka chini etc..Mungu akijaalia nataka nije nikae humo nami
Nimeshatoa update mkuu. Cheki post ya kwanza
 
Habari ya wakati huu wakuu.

Mwenzenu nimeamua kuchukua Rumion ila sasa nimekuta kuna toleo la 2007-2008 na toleo la 2010-2015.

Haya matoleo mawili nimeona yana tofauti ndogo za muonekano; show ya mbele, ndani kwenye dashboard hasa sehemu ya AC na ndani kwa nyuma. Sijui kuhusu uimara, perfomance na changamoto zake kulingana na matoleo hayo mawili.

Naombeni mnishauri nichukue ipi kwa kuzingatia uzoefu wenu.
View attachment 2071197
2010View attachment 2071198
2008

UPDATE 17 April 2022

Gari limefika tangu March mwanzoni. Niliamua kuchukua la 2008 kwa sababu ya bajeti. 2010 ushuru wake ulikuwa juu.

Gari zuri halina shida. Utulivu barabarani, space kubwa ya kutosha na lina mziki mkubwa sana, hakuna haja ya kuongeza speaker za ziada.

Changamoto yake kuu ilikuwa kugusa chini. Hata tofali la block likilazwa huvuki. Ni kama ilivyo kwa Nissan Fuga, Wish, Alphad, IST, Vitz n.k.

Nimeshaitatua hiyo changamoto kwa kuliinua. Nimeweka spensa (nimeandika kama inavyotamkwa) kwa Tsh. 60,000 (vifaa na ufundi). Hakuna kilichobadilika kimuonekano na utendaji na haligusi tena.

Asanteni nyote mliochangia mawazo.
Spensa umeweka za nini?

Si angalau ungenunua tairi ya size kubwa kidogo kuliko kuweka spensa
 
Mkuu tairi na rim mpya ni zaidi ya 2M. Kwa kuwa nilichokuwa natafuta ni kuinua gari na kwa 60,000 spensa zimetatua nikaona poa tu.

Mkuu, kwanini unashuri tairi na rim size kubwa badala ya spensa? Naomba kujifunza.
 
Back
Top Bottom