Tozo katika mabenki-Bank transaction Tax, kodi hii ipo Nchi nyingine duniani!

Tozo katika mabenki-Bank transaction Tax, kodi hii ipo Nchi nyingine duniani!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Hizi kodi zinauma.
Lakini imebidi nifanye kautafiti kidogo kuchunguza kama Mwigulu kalewa madaraka au la!

Tozo katika Mabenki ipo nchi nyingine nyingi tu duniani, ni kodi hii kwa ujumla inaitwa Bank Transaction Tax.

Kodi hii haichagui mnene au mfupi, tajiri au masikini, mwenye kipato na asiye na kipato.

Alimradi umeitumia benki upitisha malipo au mdeni, basi tozo(levy) inachajiwa kwa kila transaction.

Tatizo lililopo ni kiasi cha tozo hiyo.

Tozo hatuzipendi lakini tufanyeje?
 
Weka hela zako kwenye ardhi ukiwa unafukia hakikisha mtu asikuone

Unataka mbinu nyingine

Kina mama wairudie ile benk kongwe ya fundo la kanga kiunoni

Nipo nawafikiria hawa wavaa crop top
 
Bila shaka unaongelea Nchi ambazo ukianguka barabarani ambulance inakuja na kupatiwa huduma bila kuulizwa malipo kwanza, sisi hapa utakatwa hiyo hela kiroho safi na ukifika kwenye huduma za Serikali/afya unahudumiwa kiroho mbaya.
 
Mi naona kama umechanganya mafaili kidogo. Kwasababu kuna tozo ya benki na tozo ya serikali. Yaani bank tangu hapo kabla walikuwa wanakata kiasi fulani wakati wa kutoa, kama ilivyokuwa kwenye mitandao ya simu, sasa Serikali nao wanakata tozo kwenye hiyohiyo hela ambayo tayari benki wamekata na watawalipa serikali gawio lao.

This is double taxation!
Kukata kodi au tozo zaidi ya mara moja kwa kipato hichohicho ni wizi!
 
Hizi kodi zinauma.
Lakini imebidi nifanye kautafiti kidogo kuchunguza kama Mwigulu kalewa madaraka au la...
Watu tunaangalia tija ya hizo tozo ....siyo kuwepo duniani ...hizo nchi unazo sema duniani zimejenga miundombinu, maviwanda, vyuo nk hapa Tanzania mama yenu anakusanya kodi kwa ajili ya MAFISADI TU NA SIYO KWA AJILI YA WANANCHI
 
Mi naona kama umechanganya mafaili kidogo. Kwasababu kuna tozo ya benk na tozo ya serikali. Yaani bank tangu hapo kabla walikuwa wanakata kiasi fulani wakati wa kutoa, kama ilivyokuwa kwenye mitandao ya simu, sasa serikali nao wanakata tozo kwenye hiyohiyo hela ambayo tayari benk wamekata na watawalipa serikali gawio lao.

This is double taxation!
Kukata kodi au tozo zaidi ya mara moja kwa kipato hichohicho ni wizi!
Ni kweli, lakini tozo hii ni kwa ajili ya serikali kujipatia mapato.

Haina uhusiano na mapato ya benki.
 
Halafu hizo nchi hata kama zipo, wananchi wake hawana maisha kama ya kwetu. Tanzania bado ni nchi maskini!
Huko kuna wananchi wanaishi na kuku nyumba moja?

Huko kuna wananchi wanaishi kwenye nyumba kama hizi?

Acheni kabisa kulinganisha Tanzania na nchi nyingine kwenye suala la tozo na bando. Tujilinganishe kwenye masuala ya maendeleo na tofauti kubwa kati ya walionacho na wasionacho! Tozo na kodi zaidi ya mara moja ni wizi!
Screenshot_20220822-104905_1.jpg
 
Bila shaka unaongelea Nchi ambazo ukianguka barabarani ambulance inakuja na kupatiwa huduma bila kuulizwa malipo kwanza, sisi hapa utakatwa hiyo hela kiroho safi na ukifika kwenye huduma za Serikali/afya unahudumiwa kiroho mbaya.
Hizo hazina hizo kodi, nimewahi kuwa hizo nchi bank charge ni ya mwezi tu hamna zaidi ya hapo, withdrawal and transfer is free.
 
Hizo Kodi ni kweli zipo hasa nchi za Ulaya lakini hizo nchi ni za Dunia ya kwanza na karibia Kila mwananchi ana Kazi na kipato kizuri. Sasa usilinganishe nchi tajiri na nchi masikini, hapa Wananchi ndiyo wanaumia. Pia Serikali kwa hizi tozo ni wizi wanawaibia Wananchi.
 
Hzo azina hzo kodi nmewahi kuwa hzo nchi bank charge ni ya mwez tu amna zaidi ya apo withdrawal and transfer is free
Austria, Belgium, France, Greece, Hungary, Iceland, Latvia, the Netherlands, Poland, Portugal, Slovakia, Slovenia, Sweden, and the United Kingdom all levy bank taxes. Almost all of these countries implemented the levy between 2009 and 2012, with Greece (1975) and Poland (2016) the only exceptions.

Hizo nchi kiujumla zimekuwa kama welfare states.
 
Mambo yangekuwa mwakemwake watu Wala wasingeongea kitu ila kwa kuwa Mambo ni matope ngja watu walie, akili zitakaa sawa tu...Mimi naamini kabisa sisi Kama siyo wagonjwa basi tumefungwa akili.
 
Hizi kodi zinauma.
Lakini imebidi nifanye kautafiti kidogo kuchunguza kama Mwigulu kalewa madaraka au la!

Tozo katka Mabenki ipo nchinyingine nyingi tu duniani, n kodi hii kwa ujumla inaitwa Bank Transaction Tax.

Kodi hii haichagui mnene au mfupi, tajiri au masikini, mwenye kipato na asiye na kipato.

Alimradi umeitumia benki upitisha malipo au mdeni, basi tozo(levy) inachajiwa kwa kila transaction.

Tatizo lililopo ni kiasi cha tozo hiyo.

Tozo hatuzipendi lakini tufanyeje?
Nya-no-ko-o-o
 
Tatizo hujijui kama ni mjinga, Ulaya kuna kodi kubwa kuliko kwetu, Sasa jiulize mishahara na huduma za jamii tunalingana?

Ukisikia kufikiri Kwa kutumia nakalio ndio huku Sasa, aibu kama hizi mumuachie Msigwa ahaibike mwenyewe maana analipwa mshahara Kwa ajili ya kuongea propaganda za serikali, je wewe unalipwa nini?
 
Hizi kodi zinauma.
Lakini imebidi nifanye kautafiti kidogo kuchunguza kama Mwigulu kalewa madaraka au la!

Tozo katka Mabenki ipo nchinyingine nyingi tu duniani, n kodi hii kwa ujumla inaitwa Bank Transaction Tax.

Kodi hii haichagui mnene au mfupi, tajiri au masikini, mwenye kipato na asiye na kipato.

Alimradi umeitumia benki upitisha malipo au mdeni, basi tozo(levy) inachajiwa kwa kila transaction.

Tatizo lililopo ni kiasi cha tozo hiyo.

Tozo hatuzipendi lakini tufanyeje?
Tozo vs Kodi
 
Serikali tayari inachukua kodi kwenye makato ya benki yanayofanywa katika kila muamala.Hizi tozo ni wazo ovu na uvivu au kushindwa kutafuta chanzo cha mapato...dunia nzima inapambana na double taxation ...wizara imeamua kuharibu mfumo wa fedha huku BOT inaangalia bila kuchukua hatua yoyote
 
Hizi kodi zinauma.
Lakini imebidi nifanye kautafiti kidogo kuchunguza kama Mwigulu kalewa madaraka au la!

Tozo katka Mabenki ipo nchinyingine nyingi tu duniani, n kodi hii kwa ujumla inaitwa Bank Transaction Tax.

Kodi hii haichagui mnene au mfupi, tajiri au masikini, mwenye kipato na asiye na kipato.

Alimradi umeitumia benki upitisha malipo au mdeni, basi tozo(levy) inachajiwa kwa kila transaction.

Tatizo lililopo ni kiasi cha tozo hiyo.

Tozo hatuzipendi lakini tufanyeje?
Kiingereza kigumu soma tena uone zinavyokatwa bila kuwepo na kodi nyingine na nchi nyingine wamezifuta
 
Kiingereza kigumu soma tena uone zinavyokatwa bila kuwepo na kodi nyingine na nchi nyingine wamezifuta
Hebu jiridhishe hapo.
The 2007-2008 financial crisis triggered a global debate on whether, and if so how, taxation can be used as an instrument to stabilize the financial sector and to generate revenue to partially cover the costs associated with the recent and potential future crises.

Three approaches were mainly discussed, namely

  • financial stability contributions (levied on financial institutions’ liabilities and/or assets)
  • financial activities taxes (levied either on financial institutions’ profits or remunerations)
  • financial transaction taxes (levied on trade in financial instruments such as stocks, bonds, derivatives, and currencies)
Today’s map shows which European OECD countries implemented financial stability contributions, commonly referred to as “bank taxes.”

What is a Bank Tax? Compare bank Taxes in Europe. The 2008 financial crisis triggered a global debate on whether taxes can be used as way to stabilize the financial sector (financial institutions).
 
ilimradi maendeleo tanayaona hakuna shida kabisaaa......tozo iendelee tena nashauri ziangaliwe njia nyingine za kuchangia maendeleo yetu, badala ya kuchangia harusi na masharehee mengine sasa tunaweza kuchangia 1200 maendeleo ya barabara zetu, hospitali, maji n.k

Mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe.
tusitegemee kujengewa nchi yetu na mataifa mengine.

wala tusifikirie eti jinsi awamu ya 1 hadi ya 6 walivyo ongoza lazima ifanane na awamu hii ya 5, kila kiongozi anamaono yake ya kutuletea maendeleo.

Tutaendelea kulipa tozo bila shida yoyote.

wanao pinga tozo ni wahuni wachache wenye matatizo ya afya ya akili.
 
Back
Top Bottom