Tozo mpya 17, mwendelezo wa maumivu kwa Mtanzania

Tozo mpya 17, mwendelezo wa maumivu kwa Mtanzania

2025 CCM imekwisha, waTanzania watapongezwa kwa kupata kiongozi mpya asiyetokana na CCM. Je ni sababu gani zitawafanya waTanzania kuchukua hatua hiyo:
  • Uchovu wa ndani ya CCM kufanya siasa kutokana na kutenda maovu, ugandamizi, kukamua wananchi kodi kupita kiasi huku viongozi wao wakijiongezea mishahara minono, magari ya kifahari ya kuwahudumia, majumba na marupurupu mengi. Mfano wa kuchoka ni gazeti la UHURU kuonesha kuchoka kutetea serikali ya CCM huku mhariri wake mkuu wa gazeti ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM MNEC. Kifupi CCM imeshindwa kufanya ushawishi kitu ambacho ndiyo msingi wa chama chochote cha siasa
  • Kila mtanzania akiangalia matendo ya CCM wanaona ni kama "eneo la jinai" yaani Crime scene mfano tozo za miamala, miradi ghofu ndege za Air Tanzania , SGR reli mpya, Stiegler's gorge, kesi za kubambikia, wafungwa wa kisiasa, matumizi mabaya ya vyombo vya usalama n.k
  • Makada na wanachama wa CCM waliopo serikalini wenye mamlaka yaani mawaziri, wakuu wa mikoa, RAS, maDC, DAS, DED wamekuwa watesi kwa waTanzania na siyo watumishi.
  • Wananchi kutambua kuwa hawana wawakilishi wao waliowachagua kupitia uchafuzi wa uchaguzi 2020 wa wabunge, madiwani, wenyeviti wa Mitaa na Vijiji. Hivyo kifupi hawana viongozi waliowachagua wao.
Kinachofuata ni kuwa 2025 wananchi wote bila kujali vyama vyao au itikadi hawatakichagua chama-ruhani cha CCM kwa kuwa CCM hakina tena vinasaba / DNA ya sifa za kuwa chama cha kisiasa.
Unawajua kitengo wewe wanatumika kwenye chaguzi hizi ndoto ota tu.
 
Kale ka wimbo kenu wacha waisome namba, huwa ni katamu sana mnapokaimba kwenye vikao na mikutano yenu, mkija kwenye uhalisia huku Uswazi tunakoishi, na nyie pia mnaisoma namba kikamilifu, hamko exempted na mikodi na matozo mnayoyaasisi kila uchao
Usilazimishe tufanane.... endelea kuisomaa
Mi10 tena kwa SSH 📍🔨
 
Back
Top Bottom