Tozo mpya 17, mwendelezo wa maumivu kwa Mtanzania

Tozo mpya 17, mwendelezo wa maumivu kwa Mtanzania

Kale ka wimbo kenu wacha waisome namba, huwa ni katamu sana mnapokaimba kwenye vikao na mikutano yenu, mkija kwenye uhalisia huku Uswazi tunakoishi, na nyie pia mnaisoma namba kikamilifu, hamko exempted na mikodi na matozo mnayoyaasisi kila uchao
Kuna ambao wako exempted! Huwezi kuumia kama daily unaingiza 300k ukiwa umekaa tu
 
Kumbe wewe Ni nesi. Bora wewe uko ndani. Mimi Ni mlinzi nyumbani kwa mbunge mmoja mzembe mzembe Kuna baridi Dodoma njombe kumesingiziwa.
Umeassume ni nesi simply kwasababu ana id ya kike
 
2025 CCM imekwisha, waTanzania watapongezwa kwa kupata kiongozi mpya asiyetokana na CCM. Je ni sababu gani zitawafanya waTanzania kuchukua hatua hiyo:
  • Uchovu wa ndani ya CCM kufanya siasa kutokana na kutenda maovu, ugandamizi, kukamua wananchi kodi kupita kiasi huku viongozi wao wakijiongezea mishahara minono, magari ya kifahari ya kuwahudumia, majumba na marupurupu mengi. Mfano wa kuchoka ni gazeti la UHURU kuonesha kuchoka kutetea serikali ya CCM huku mhariri wake mkuu wa gazeti ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM MNEC. Kifupi CCM imeshindwa kufanya ushawishi kitu ambacho ndiyo msingi wa chama chochote cha siasa
  • Kila mtanzania akiangalia matendo ya CCM wanaona ni kama "eneo la jinai" yaani Crime scene mfano tozo za miamala, miradi ghofu ndege za Air Tanzania , SGR reli mpya, Stiegler's gorge, kesi za kubambikia, wafungwa wa kisiasa, matumizi mabaya ya vyombo vya usalama n.k
  • Makada na wanachama wa CCM waliopo serikalini wenye mamlaka yaani mawaziri, wakuu wa mikoa, RAS, maDC, DAS, DED wamekuwa watesi kwa waTanzania na siyo watumishi.
  • Wananchi kutambua kuwa hawana wawakilishi wao waliowachagua kupitia uchafuzi wa uchaguzi 2020 wa wabunge, madiwani, wenyeviti wa Mitaa na Vijiji. Hivyo kifupi hawana viongozi waliowachagua wao.
Kinachofuata ni kuwa 2025 wananchi wote bila kujali vyama vyao au itikadi hawatakichagua chama-ruhani cha CCM kwa kuwa CCM hakina tena vinasaba / DNA ya sifa za kuwa chama cha kisiasa.
Nikukumbushe tu ccm haitegemei kura kuwepo madarakaani...zile ni geresha tu
 
Hiv hizo tozo ni kwamba hizo shughuri zilikuwa hazilipi kodi mwanzoni ama? Mbona wanatengeneza mazingira ya kuua uwekezaji kwa kuwajazia makodi
 
Hii nchi aliyekuwa analipa kodi haswa ni mtumishi kwa kutumia paye. Imagine unalipwa mshahara wa mil 3 paye pekee ni 720k kwa mwezi zidisha kwa mwaka. Sasa ni mfanyabiashara gani wa kati analipa kodi hiyo? Kodi zitozwe na zitumike ipasavyo, sio mambo mtu anafanya ubadhirifu wa bil 100 faini mil 8 huu unakuwa utani.
 
Rais hazungukwi na yoyote anajizunguka mwenyewe tu.

Katika nchi hii ukiondoa tozo za halmashauri hakuna jambo lolote linalohusu fiscal policy ambalo litafanyika bila kupita kwenye Baraza la mawaziri ambako rais ni mwenyekiti wake.


Mstake kumuondoa rais kwenye responsibility yake kama anazungukwa halafu katulia tu hiyo ni acquiescence na ni uzembe wake mwenyewe.
 
Hii nchi aliyekuwa analipa kodi haswa ni mtumishi kwa kutumia paye. Imagine unalipwa mshahara wa mil 3 paye pekee ni 720k kwa mwezi zidisha kwa mwaka. Sasa ni mfanyabiashara gani wa kati analipa kodi hiyo? Kodi zitozwe na zitumike ipasavyo, sio mambo mtu anafanya ubadhirifu wa bil 100 faini mil 8 huu unakuwa utani.
Ulianza kwa kujenga hoja vizuri mwishoni ukaharibu focus. Au ulimpa mtu mwingine amalizie?
 
Nitarudi ngoja nihudumie wagonjwa kwanza

Nimerudi sasa saa 2 asubuhi USSR

Nadhani wakati tunapata haya maumivu kwa hizi kodi ni vizuri tujiulize maumivu yetu yanasababishwa na nini haswa!?
1 Kwa sababu tunaonewa na kuchukiwa sana na serikali yetu?
2 Ni sababu hatuko tayari kwa mabadiliko kwa kile tulichozoea?
3 Au sisi ndio nchi ya pekee duniani kulipa hizi kodi? Na kama kwingine zipo wanalipa kiasi gani?

Cc BAK Deceiver SN.BARRY
Extrovert
 
Sababu hatuna control na hizo tozo zinazokusanywa yani.

Bora mfuko huo ungekuwa wa wananchi wenyewe kama wanavyoita za kizalendo ili hata zikianza kutolewa hizo hela tuwe na wawakilishi wetu tujue kinatoka kiasi flani kwenda kufanya jambo flani! Hapo manung’uniko yangu yatakoma ila sio hela tuwakusanyie mafisadi wa CCM wao wadokoe wanavyojiskia!
 
Back
Top Bottom