kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ingekuwa sawa kama ongezeko la tozo za miamala na mafuta kwa wanyonge lingelenga kwenda kununua meli kubwa za uvuvi ili tuvue kisasa kwenye kina kirefu, kununua matrekta kwa wakulima ili walime mashamba makubwa, kuchimba madini ya kimkakati kama chuma au kusambaza nishati ya gesi nchini ili watu wasikate miti.
Unapojenga zahanati kila kijiji utahitaji pia kupeleka watumishi, vifaa tiba, madawa na kujenga nyumba za watumishi huko vijijini. Tatizo leo sio kuwa na zahanati kila kijiji, bali ni kuziboresha hizi zilizopo ili zitoe huduma zilizokusudiwa (quality badala ya quantity).
Pesa za kujenga vituo vya afya na shule zilikuwepo ila vipaumbele vya viongozi ilizielekeza kwenye miradi ambayo haigusi wananchi moja kwa moja kama vile kujenga Ikulu kubwa ya kufa mtu, kujenga ukuta melelani, kujenga national park kule Burigi, safari za viongozi ndani na nje ya nchi, kujenga majengo ya wizara na ofisi mpya wakati majengo hayo yapo. Kuhamia Dodoma ni sawa na ni jambo jema, lakini kutumia fedha nyingi kuhamia dodoma wakati watu hawana maji, shule, barabara, umeme, majosho, mbolea, na zahanati zenye watumishi, vifaa tiba na dawa ni kejeli kubwa kwa wananchi ambao wanatakiwa kuongezewa tozo za miamala na mafuta eti kujijengea vitu hivyo.
Binafsi sioni uhusiano uliopo kati ya kuhamia dodoma na upatikanaji wa maji, zahanati, madarasa, umeme, nyumba za watumishi, vifaa tiba na watumishi kwa wananchi wote nchini na hasa vijijini.
Mheshimiwa Mwigulu anataka kutuaminisha kuwa pesa ya kodi, tozo na mauzo ya mazao na madini kama korosho, kahawa, pamba, dhahabu, bandari na uchukuzi, mikopo, misaada na huduma mbalimbali tunazotoa kama nchi sio za kujengea madarasa na zahanati hadi tukamue watu kwenye miamala, mafuta na umeme.
Tusidanganyane jamani, tukutane 2025