Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Habari wakuu,

Miamala yote ya fedha ya kibenki itayofanyika kupitia simu itaanza kukatwa tozo. Mathalan unataka kuhamisha fedha kutoka kwa Helena mwenye akaunti namba XX kwenda kwa Huruma mwenye Account namba XY na ukatumia simu kufanya mchakato huo utawajibika kuichangia Serikali katika ujenzi wa madarasa, zahanati na mengineyo waliyoyasema.

Kwanini Serikali wasingetumia pesa za kununulia ndege zisizozalisha na gharama za kufanya royal tour kufanya yote wanayotaka kufanya. Ni muda wa kufikiria kupunguza matumizi badala ya kututoza kodi mara mbilimbili kuongeza mapato kufanya matumizi yasiyo na kipaumbele au umuhimu.

Bye bye sim banking
Tutajaza fomu na kuingiza hela kwenye akaunti ya mtu. Kwaheri simbanking. Tutakutumia kucheki balance tu. Nayo wakiitoza tozo hatutacheki.
 
Kuna watu mlitutambishia sana mawakala na hivyo vi account vyenu vya Benki
 
Huyu Raisi kunawatu wanampotosha ili iwe rahisi kumwondosha kitini.kuna utabiri humu JF Huenda ukatimia.
 
Ndiyo faida ya kuwa nchi yenye wananchi mafala. Viongozi wanatumbua na wananchi wanakamuliwa! Tutakiona cha mtema kuni kama hatutakuwa wakali.
Me nakubali kabisa sie ni mafala kabisa mkuu,tena ni wajinga.I wish ningekuwa natokea South Africa
 
Utawala umewajia kwa ndondokela ndo maana hawajitambui. Nakumbuka ktk mahojiano mahala jk aliwahi kusema yy alitamani tu kuwa raisi hata kama hakuna la maana ambalo angelifanya, the same kwa huyu wa kuupiga mwingu.. Wote ni watu ambao ingekuwa west Africa nchi ishabinuliwa hii ila kwa hapa bongo bado sana.
 
Habari wakuu,

Miamala yote ya fedha ya kibenki itayofanyika kupitia simu itaanza kukatwa tozo. Mathalan unataka kuhamisha fedha kutoka kwa Helena mwenye akaunti namba XX kwenda kwa Huruma mwenye Account namba XY na ukatumia simu kufanya mchakato huo utawajibika kuichangia Serikali katika ujenzi wa madarasa, zahanati na mengineyo waliyoyasema.

Kwanini Serikali wasingetumia pesa za kununulia ndege zisizozalisha na gharama za kufanya royal tour kufanya yote wanayotaka kufanya. Ni muda wa kufikiria kupunguza matumizi badala ya kututoza kodi mara mbilimbili kuongeza mapato kufanya matumizi yasiyo na kipaumbele au umuhimu.

View attachment 1927435
Kuanzia sasa sifanyi muamala kwa njia ya simu labda iwe very emergency kwa sasa ni mwendo wa ATM with my handgun on action mode kwa ajili ya usalama
 
Jana asubuhi namtumia pesa mdau kijijini akiwa na line ya voda mi nikiwa na tigopesa niliona hii issue ni sio,ni WIZI kama wizi mwingine ambapo Serikali ikishirikiana na sekta binafsi(Banks na Makampuni ya simu) Kuwaibia wanyonge.Nilikuwa nimtumie mdau kama laki 1 (100,000 tsh) . Mi asubuhi kucheck sina pesa kwenye tigopesa hivyo ikabidi nihamishe 110,000 toka CRDB kwenda tigopesa.

Kucheck gharama ya muamala huo kwa benk ni tsh 6500 hv. Yaani 5400 na VAT 940. Sasa ikafika hatua ya kutuma tigo pesa kwenda mpesa ikanicost tena tsh 4500. Hapo jumla sh 11,000. Kama gharama ya kuhamisha benk CRDB to tigopesa na tigopesa kwenda Mpesa. Ilibidi nitume 106,000 ili naye aweze kutoa hiyo 100,000.

So jumla ya kuhakikisha mdau anapata 100,000 nilitumia 11,000 ya awali na 6000 jumla 17,000. Hii ni zaidi ya riba ya kukopeshana kwenye mabenki kwa mwaka mzima. Gharama nilioingia ni 17% ya laki 1 ndani ya dk 2 tu za kufanya muamala huo. Wakati mtu angekopa laki 1 angelipa laki 1 na riba elfu 15 ndani ya mwaka mzima.

Kwa hili hatari iliyopo ni kwamba watakaothirika ni ndugu zetu ambao wanatutegemea kwa namna moja au nyingine. Mfano ikiwa Huna pesa kabisa ingebidi ubalance hiyo laki itoshe kila kitu. So huenda yule mdau angepokea 83,000 na kushindwa kutimiza lengo na kama lengo ni matibabu, ada ya shule n.k hapo inakuwa hatari zaidi.

Hatari nyingine ni kwamba tunarudi nyuma miaka 20 hivi. Maana itabidi watu waingie ndani benki kutoa akaunti moja na kuingiza akaunti nyingine na hivyo hatari ni kuwa lengo la kujenga zahanati, madarasa halitatimia kwa kuwa miamala hiyo haina tozo na mwakani itabidi turudi kufuta hili.

Najua kukosea huwa kupo kwa kilabinadamu Including serikali. Wangesawazisha hili mapema kwa kukusanya kidogo mfano 1000 au 500 kwa transactions na namba ya miamala ingekuwa mingi miamala ambayo inafanyika na lengo lingetimia bila kumuumiza mtu wa chini. Hili hawajachelewa ila wakiendelea hivi watapoteza vyote ikiwemo trust kwa wananchi na pesa wanaotegemea kukusanya.
Pole, lakini umejitia kwenye gharama zisizo za lazima, iltakiwa utume direct kutoka benk kwenda kwenye Mpesa (kwa mlengwa mwenyewe)
 
Tumekimbilia banki na huko Mwigulu kesha haribu. Huyu mtu clueless kabisa kuendesha modern economy.Arudi kijijini kufuga ngombe.
Sema yy ni.muwasilishaji tu ila waamuzi ni wakubwa kwake hivyo ni.jambo la kuilamu serikali kupitia yeye waliye mpa dhamana hiyo
 
Pole, lakini umejitia kwenye gharama zisizo za lazima, iltakiwa utume direct kutoka benk kwenda kwenye Mpesa (kwa mlengwa mwenyewe)
Nimeshajaribu miamala ya namna hiyo haikamiliki utaishia kurudishiwa pesa zako tu tena baada ya masaa 24 na CRDB na transaction cost umelipia. Yaani kutoa smibanking kwenda kwenda kwenye namba tofauti na ile uliyosajilia simbanking.
 
Nimeshajaribu miamala ya namna hiyo haikamiliki utaishia kurudishiwa pesa zako tu tena baada ya masaa 24 na CRDB na transaction cost umelipia. Yaani kutoa smibanking kwenda kwenda kwenye namba tofauti na ile uliyosajilia simbanking

Duh pole .Tangu kuanza kwa tozo za miamala , mi nimekuwa nikituma pesa moja kwa moja kwa muhusika kutoka CRDB kwenda Kwenye Mpesa, Tigopesa, nakadhalika , bila kufeli kwa muamala wowote.
 
Back
Top Bottom