Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Waendlee hivyo hivyo, sisi tutaishia kulalamka humu and nothng we can do.. mama Samia naomba ulete tozo zingine zaidi maana watu walkuposti sana kwenye siku zako 100 za kwanza km Rais..mama pliiiz endlea,unaupiga mwingi sana...
 
Mwenyewe nimetumiwa huu ujumbe na airtel sema ambacho sielewi mpaka sasa ni kwamba hizi tozo zote ni kwa ajili ya government au haya makampuni nayenyewe yameona yajiongeze sio!

Kama ni za government mbona kuna hizi ambazo zishaanza kuwa implemented au kiasi kinachopatikana hakitoshi? kama hakitoshi si wajenge tu hiyo miradi taratibu kwani wakianza kujenga hizo sijui hospitali kwa kanda mfano waanze pwani or whatever zone then waende hivo taratibu

Kwani tuna haraka ya kwenda wapi wajomba au kuna mtu kapewa promise tz inabidi iwe vipi kipindi fulani anyway wanasema when you are lost speed is useless

Serikali inayoongeza kodi na tozo kwa wananchi wake walioko kwenye hati hati za janga la Corona inapaswa kujiangalia na kujitambua iko kwa maslahi ya nani.

Cc: Jumbe Brown
 
Waziri wa fedha hatakiwi kutokea mkoa masikini ataumiza sana Wananchi wake maana anataka yeye na kundi lao ndio wale matunda ya Nchi..
 
Last week nimetoka kuchonga kibubu, bora kushindana na chumaulete za mtaani. kuliko hawa wa TOZO
 
Hakika huyu anaupiga mwingi tena mwingi sana keshakuja na tozo kubwa kwenye miamala yote ya benki

Huyu mama atatuua narudia tena atatuua na bado siku si nyingi tutatangaziwa tozo mpya kwenye mitandao ya kijamii

Navyosikia hasira ni basi tu,najikaza tu hapa natamani hata nitu.... lakini wacha nivumilie tu.

Yaani kwa lugha rahisi wewe na huyo mshauri wako na ulompa dhamana bwana tozo ndo akili zenu zimeishia hapa?

Hivi nchi yetu ina bahati mbaya gani kupata watu wa ajabu ajabu namna hii?
IMG-20210908-WA0019.jpg
 
Hakika huyu anaupiga mwingi tena mwingi sana keshakuja na tozo kubwa kwenye miamala yote ya benki

Huyu mama atatuua narudia tena atatuua na bado siku si nyingi tutatangaziwa tozo mpya kwenye mitandao ya kijamii

Navyosikia hasira ni basi tu,najikaza tu hapa natamani hata nitu.... lakini wacha nivumilie tu.
Serikali imegundua njia rahisi sana ya kupata fedha, kupitia vitu ambavyo hata wananchi masikini hawawezi kuviepuka.

Huko nyuma, bia ilikuwa inaongoza kwa makusanyo ya kodi, lakini baada ya kuona mabilioni ya fedha kupitia miamala, serikali imeamua kujinufaisha kwa hiki chanzo bila kujali kwamba inakandamiza watu wa chini zaidi kuliko hata wale wa juu.

Serikali imeamua kupuuza kabisa ukweli kwamba msingi wa tozo au kodi ni kipato, na miamala sio kipato. Huwezi kutoza kodi sehemu ambayo hakuna kipato au faida, lakini serikali haijali kwa kuwa inajua Watanzania, kama kawaida yao hawatafanya lolote

Kodi iliyotakiwa kulipiwa kwenye miamala ilipaswa kuwa fedha ambayo benki au kampuni za simu zinatoza kwa kutoa huduma za mialama, kwa kuwa sehemu hiyo ndio "faida" kwao watoa huduma, lakini sio kumtoza mtu tozo kwa kuwa tu anampatia mtu mwingine fedha na hakuna kilichozalishwa.

Hizi tozo zinakiuka msingi na sheria ya kodi, na hivyo zinapingika katika mahakama ya katiba
 
Ivi mtalalamika mpaka lini?? Unafkiri nchi kupata uhuru ni kulalamika kila siku mitandaoni bila actions, mna kila sababu ya kufanya maamuzi mbuzi hawa watawanyanyasa mpaka lini?? Viongozi wenu wanatekwa na kupigwa marisasi, wanafungwa na kupewa kesi za kigaidi hamjajifunza kitu tu?? Nchi kupata uhuru na maisha mazuri haiji kwa kukaa kimya, ccm haitotoka madarakani kwa box la kura yaani hio sahauni kabisa, kazi kwenu, nyinyi wananchi mko wengi sana mkiamua hata kwa gharama mnaweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulipa kodi sawa ni wajibu wa mwananchi, ila sasa tuangalie hizo kodi na tozo zinamuathiri vipi mwananchi wa hali ya chini,tuoneeni huruma kidogo. Wengine tunatuma hela kwenda account nyingine ili tutoe mishahara yetu maana kadi zilishachukuliwa na wakopeshaji wetu wapendwa.
 
Hizi tozo inabidi ccm waziangalie upya zitawanyima kura huko mbeleni.
 
Back
Top Bottom